Na Englibert Kayombo WAMJW - GEITA
Mganga
Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi amesema juhudi za kila mwananchi mmoja mmoja
zinahitajika ili kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa kubadili mtindo
bora wa maisha, ulaji wa chakula bora pamoja na kufanya mazoezi.
Prof.
Makubi amesema hayo akiwa kwenye kikao cha viongozi ndani ya Mkoa wa Geita
kilichofanyika mkoani huyo kujadili miundombinu ya sekta ya afya na elimu.
“Sasa
tumeingia katika vita nyingine ya kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza,
magonjwa haya hayana dalili ya kukushtua kwenda Hospitali, haya ni hatari zaidi
kuliko yale magonjwa ya kuambukiza” amesema Prof Makubi.
Amesema
dalili magonjwa yasiyo ya kuambukiza huwa hazijitokezi kwa haraka zaidi hivyo
mtu huwa anajiona kuwa yuko salama ili hali akiwa mgonjwa ambapo dalili huja
baadae kwa uzito mkubwa na mtu huwa amechelewa kuanza kupata matibabu.
“Magonjwa
ambayo ni ya kuambuzika yana dalili, utajisikia homa au uchovu, magonjwa yasoyo
ya kuambukiza hayana hizo dalili za kukushtua kwenda hospitali, utaanza kuona
matatizo baadae na kugundua moyo au figo imefeli, hizo ndo dalili za kwanza”
amefafanua Prof. Makubi
Prof.
Makubi amesema ni lazima tuelewe magonjwa hayo kama vile presha, moyo,
kisukari, kufeli kwa figo na kifua ni hatari kuliko hata yale ya kuambuza
yakiwemo Malaria, Ukimwi na Kifua Kikuu ambapo mtu asipojitambua mapema kufanya
vipimo, kubadilisha tabia, mwenendo wa chakula huishia kuathirika kiuchumi yeye
na familia yake kwa kuwa magonjwahayo yana gharama kubwa za matibabu.
“Usijitambua
mapema kufanya vipimo, kubadilisha tabia na mwenendo wa chakula utajikuta uko
kijana wa umri wa miaka 30 hadi 50 unapata matatizo ambayo yatakufanya ushindwe
kushikiri katika majukumu yako ya uzalishaji na kuiingiza serikali katika
gharama kubwa ya kukuhudumia” amesema Prof. Makubi
Amesisitiza
wananchi kubadili mtindo wa maisha, mwenendo wa chakula na kuzingatia kufanya
mazoezi ya mara kwa mara ili kupambana na magonjwa hayo ambayo yameshika kasi
hasa kwa vijana na watu wazima.
“Zamani
tulikuwa tunafanya mazoezi, tunalima, tunaendesha baiskeli, kutembea sasa hivi
hatufanyi hivyo na ndio maana tumejikuta tunapata haya matatizo ya magonjwa yasiyo
ya kuambukiza kwa haraka sana, tufanye mazoezi na kubadilisha mtindo wa maisha
yetu tunayoishi sasa na kuzingatia mwenendo bora wa vyakula vyetu” amesisitiza
Prof. Makubi
Aidha
amewataka viongozi hao kuendelea kutoa elimu ya afya kwa wananchi ili kuweza
kubadilisha mtindo wa maisha na wananchi hao waanze kwenda hospitalini kufanya
vipimo ili kutambua dalili za haraka za magonjwa hayo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi.
Robert Gabriel amewataka wananchi kuzingatia mtindo bora wa maisha na kufanya
mazoezi ya mara kwa mara ili kuepukana na magonjwa hayo
“Tumeambiwa maisha yamebadilika, mazoezi ndio
mpango mzima wa afya, tumekuwa ‘busy’ mno kila siku kwenye magari maisha
yamebadilika na magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza huja na mtetemo mkubwa na
kupona huwa ni shida, tukumbushane na kubadilika ili tuweze kupambana na
magonjwa hayo” Amesisitiza Mkuu wa Mkoa wa Geita.
Mhe. Robert Gabriel ametoa wito kwa wananchi
kufanya mazoezi ya mara kwa mara na kubadili mtindo wa maisha kuepukana na
magonjwa hayo ambayo amesema huathiri uchumi wa familia na nchi kuingia gharama
kubwa ya matibabu.
Mwisho
The fact that you included sources in your post is another excellent touch, in my opinion.It's crucial to always support your statements with reliable data.I think it's important to take into account different perspectives on this issue.All viewpoints ought to be acknowledged, regardless of what they say, in my opinion.
JibuFuta