Na Englibert
Kayombo, WAMJW - Mwanza
Mganga Mkuu wa
Serikali Prof. Abel Makubi ametoa wito kwa Hospitali zenye wataalam wanaotoa
huduma za kibingwa kuwa na huduma za mkoa “Outreach Services” endelevu ili
wananchi walio mbali na huduma hizo nao waweze kuhudumiwa karibu na maeneo
waliyopo.
Prof. Makubi
ametoa amesema hayo akiwa katika ziara ya kikazi katika Hospitali ya Rufaa ya
Kanda ya Bugando ambapo alikwenda kujionea hali ya utoaji wa huduma na
kuzungumza na viongozi na kamati tendaji ya hospitali hiyo.
“Nitoe wito kwa
Hospitali zote za Kanda, Maalum na ya Taifa ambazo tunazo nchini, zianze ama
kama wameashaanza waendele kushuka chini kwenda kutoa huduma za mkoba kwenye
hospitali zetu” amesema Prof. Makubi
Prof. Abel
Makubi amesema kuwa Hospitali hizo zina wajibu wa kuwajengea uwezo wataalam
waliopo kwenye Hospitali ngazi ya chini yao kuanzia Hospitali za Rufaa za
Mikoa, Wilaya hadi ngazi ya chini ili waweze kutoa huduma kwenye maeneo yao na
kuwapunguzia gharama wananchi kwenda umbali mrefu kwa ajili ya kupata huduma za
matibabu.
Amesema kuwa
wananchi wengi hawapati huduma za kibingwa katika maeneo yao kutokana na
kukosokana kwa wataalam hao na pamoja na miundombinu ya vifaa wezeshi vya
huduma hizo katika Hospitali za Wilaya hivyo ni vyema wakawa na mipango ya
huduma hizo kwenye maeneo ya karibu na wananchi.
Prof. Makubi
amesema kuwa huduma za mkoa zinawasaidia pia wataalam waliopo kwenye Hospitali
za Wilaya kuongeza ujuzi wa kazi hasa kwenye kuwahudumia wananchi wenye uhitaji
wa huduma za kibingwa ambazo hazipatikani kwenye maeneo yao.
Aidha Prof.
Makubi ameipongeza Hospitali ya Kanda ya Bugando kwa kuwa na program endelevu
ya huduma za mkoa na kuwahimiza wasiache kutoa huduma hizo kwa wananchi huku
akizitaka Hospitali nyingine kuiga kutoka hospitali hiyo.
“Watu wanaona
umuhimu wa Bugando kwamba ipo pamoja na wao, kwa hiyo ni vizuri na nyie mkatimiza
huo wajibu wa kuendelea kushikamana na viongozi kuanzia ngazi ya Mikoa, Wilaya,
Vituo vya afya mpaka kwenye zahanati”Amesema Prof. Makubi
Amemtaka
Mkurugenzi pamoja na kamati tendaji ya hospitali hiyo na hospitali nyingine za
Kanda na Taifa kukaa pamoja kwa muda wa miezi 3 ijayo kuona ni jinsi gani
kuziendeleza huduma hizo za mkoba katika Mikoa 8” Amesisitiza Prof. Makubi
Kwa upande wake
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dkt. Fabian Massaga
amesema hospitali hiyo inaendela kutoa na kuboresha huduma zaidi ili wananchi
wengi waweze kupata huduma bora katika kanda ya ziwa.
Amesema
Hospitali hiyo imekuwa ikitoa huduma za mkoba pamoja na ‘camp’ za huduma za
kibingwa kwa wananchi hivyo kuwapunguzia gharama ya kwenda umbali mrefu kufuata
matibabu bugando.
Amebainisha kuwa
hospitali hiyo katika mwezi huu wa desemba kuazia tarehe 18 itaendesha ‘camp’
ya huduma za upasuaji wa moyo pamoja na upasuaji kwa watoto ambapo wataalam
bigwa wa huduma hizo kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bugando na Daktari
kutoka nchi ya Uganda.
0 on: "HOSPITALI ZENYE WATAALAM BINGWA ZATAKIWA KUTOA HUDUMA ZA MKOBA KWA WANANCHI WALIO MBALI NA HUDUMA"