Na WAMJW – Mwanza.
Amesema hayo akiwa kwenye kikao kazi na timu ya uongozi wa
afya ndani ya Mkoa wa Mwanza kilichofanyika Wilayani Misungwi kujadali mikakati
ya uboreshaji wa huduma za afya mkoani humo.
“Kwanini tushindwe kuchangia uboreshaji wa huduma za afya,
lazima tuwe na moyo wa kujitoa kuchangia, hizi ni mali zetu sote sisi pamoja na
watoto wetu sote tutatibiwa huko” Ni lazima sasa Hospitali zetu zianze kuwa na
jicho la kutoa huduma huku zilijenga uwezo wa kifedha na kupunguza utegemezi
toka serikali, bila kuathiri huduma kwa wananchi wasio na uwezo wa kulipia..
amesema Prof. Makubi.
Amesema hatuwezi kuitegemea Serikali na wafadhili pekee
kutuletea Maendeleo ya huduma za afya katika maeneo yetu hivyo na watumishi
wanapaswa kushiriki katika kuboresha huduma hizo katika maeneo waliyopo.
Aidha Prof. Abel Makubi alitumia nafasi hiyo pia kuendesha shughuli
ya michango kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za afya ndani ya Mkoa huo ambapo
juma ya Tsh 6,850,000/= fedha ambayo itaenda kutumika katika ujenzi wa jengo
kwa ajili ya huduma kwa watoto waliolazwa mahututi (NICU)
Prof. Makubi amesema kuwa Mkoa wa Mwanza una uhitaji mkubwa
wa huduma hiyo hivyo ufinyu wa eneo katika Hospitali ya Bugando unasababisha
watoto walio wagonjwa kukosa huduma kwa wakati.
“Hospitali ya Budango inaendelea kupata wingi wa watoto
ambao hawajafikia umri wa kuzaliwa na wengi wakiletwa bugando kunakuwa na shida
ya kupata eneo la kuwahudumia, kwa michango hiyo itasaidia kuboresha huduma
hizo kwa kuongeza eneo” amesema Prof. Makubi
Hata hivyo Prof. Makubi amesisitiza suala la uongozi imara
kwa viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia taasisi za afya na
kuwasisitiza kuwajibika ipasavyo katika utumishi wao kwa kuhakikisha
watumishi walio chini yao wanatoa huduma bora kwa wananchi.
Mwisho
0 on: ""WATUMISHI WA AFYA MSHIKIRI KATIKA KUCHANGIA MAENDELEO YA SEKTA YA AFYA" - MGANGA MKUU WA SERIKALI"