Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha kujadili hali ya utoaji huduma za afya nchini ambacho kimewakutanisha Wakurugenzi wa Wizara pamoja na Taasisi zake kilichofanyika kwenye ukumbi wa hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel akieleza jambo wakati wa kikao kazi cha kujadili hali ya utoaji huduma za afya nchini ambacho kimewakutanisha Wakurugenzi wa Wizara pamoja na Taasisi zake kilichofanyika kwenye ukumbi wa hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha kujadili hali ya utoaji huduma za afya nchini Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel na kushoto kwake ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Edward Mbanga.
Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Taasisi za Wizara ya Afya wakifuatilia kwa makini neno kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima (hayupo kwenye picha) wakati wa kikao kazi cha kujadili maendeleo ya Sekta ya Afya, kilichofanyika kwenye ukumbi wa hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
Wakurugenzi wa Wizara ya Afya pamoja na Wakurugenzi wa Taasisi zake wakiwa katika kikao kazi cha kujadili hali ya utoaji huduma za afya nchini kilichoongozwa na Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima, kikao kimefanyika katika ukumbi wa hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
SERIKALI KUJA NA MFUMO WA TEHAMA WA UFUATILIAJI DAWA
Na. Catherine Sungura,WAMJW-Dodoma.
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto inatarajia kuanzisha mfumo wa Tehama kufuatilia mnyororo mzima wa utoaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vya umma vyote nchini.
Hayo yamesemwa leo na Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto wakati wa kikao kazi cha kujadili hali ya utoaji huduma za afya nchini ambacho kimewakutanisha Wakurugenzi wa Wizara pamoja na Taasisi zake kilichofanyika kwenye ukumbi wa hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
Dkt. Gwajima amesema kuwa, mfumo huo utasaidia kufuatilia utoaji wa dawa unaofanywa na watoa huduma za afya kwenye vituo vya umma , kwani Serikali haitaji upotevu wa dawa kwenye vituo vyake.
"Tunataka mfumo huu uunganishe vituo vyote pamoja na hospitali zote hadi za Taifa kwani huu ni ulimwengu wa Tehama,hivyo kama kiongozi anatakiwa kuona kila kitu pale alipo ili kuweza kurahisisha kutatua matatizo ya wananchi wetu na hivyo tutadhibiti upotevu wa dawa kwani imekua ni changamoto kubwa na sio kwamba dawa hamna".Alisema Dkt. Gwajima.
Hata hivyo, Dkt. Gwajima aliwakumbusha watoa huduma kutoa dawa kwa kufuata muongozo wa utoaji wa dawa kwa kuandika jina la dawa na sio jina la kampuni kwani kwa kufanya hivyo inasababisha kukosekana kwa dawa ilhali dawa zipo kwenye stoo.
Kwa upande mwingine, Dkt. Gwajima, ameagiza kufufuliwa na kukanza vikao mara moja kwa kamati za dawa kuanzia ngazi ya Taifa hadi Zahanati, ili kuweza kujadili dawa zote zinazotumika kwenye vituo vyao jambo ambalo litasaidia kugundua upotevu wa dawa kwenye vituo vya umma.
Naye, Naibu Waziri Dkt. Godwin Mollel amesema kikao kazi hicho kitasaidia kujua changamoto na kuzijadili kwa pamoja ili kuweza kuwasaidia wananchi kupata matibabu bora na huduma zingine kwenye taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo kwa urahisi.
Amesema kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita uwajibikaji na uadilifu umefanyika na hivyo nchi kufanya mapinduzi makubwa kwa kutumia mapato ya ndani, Serikali inayo uwezo wa kununua dawa,vifaa na vifaa tiba na kutoa matibabu kwa wananchi kwa gharama nafuu na hivyo itawaondolea wananchi mzigo mkubwa wa matibabu nchini.
Dkt. Mollel amewataka watumishi kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu ili kuondoa matatizo yalipo, kwani asilimia 75 ya matatizo hayo yanaweza kutatuliwa na wenyewe bila kutegemea mtu mwingine, hivyo kuwataka kuongeza kasi ya utendaji kazi na kutumia mapato vizuri ili kuweza kuboresha huduma za afya nchini na kuiongezea mapato Serikali na kusiwepo upungufu wa dawa kwa kuweza vipaumbele maeneo muhimu.
-MWISHO-
Me puedo conectar con tus ideas, que creo que son muy reveladoras. You gave the idea such a clear and detailed explanation. Estoy muy agradecido de que nos hayas enviado este excelente artículo. I am certain that many readers will find it very useful. Gracias por tomarse el tiempo de escribir un artículo tan educativo. Mucho he aprendido leyendo esto.
JibuFutaFantastically interesting post. It was an interesting read all the way through. Continue to publish high-quality content.
JibuFutaleyes de divorcio de nueva jersey adulterio
abogado de familia español
Great post on the government’s move towards adopting an ICT system! It’s exciting to see how technology is being integrated to improve efficiency and transparency. Implementing a modern system will likely streamline services and make interactions more accessible for everyone. I look forward to seeing the positive changes this technology will bring to governance and public service delivery. Thanks for sharing this insightful update! best divorce lawyers in arlington va
JibuFutaquick uncontested divorce in virginia