Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumamosi, 4 Novemba 2017

SERIKALI ITAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI KWA WANAOTAKA KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA AFYA,





Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi  kwa wadau wa maendeleo nchini wanaotaka kuwekeza kwenye sekta ya Afya.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan wakati wa Matembezi ya Hisani yenye lengo la kukusanya Fedha zitakazo saidia kugharamia mafunzo ya uuguzi na ukunga katika viwanja vya Green ground jijini  Dar es salaam.
Mh. Samia Suluhu amesema Serikali imekwisha weka mikakati thabiti ikiwemo kuongeza viwanda vya kutengeneza Dawa na Vifaa tiba ili kuongeza upatikanaji na uboreshaji wa huduma muhimu za Afya kwa binadamu. 
“Waziri wa Afya muongeze jitihada za kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa kina mama, mfanye tafiti na mchunguze kifo chochote cha mama na mtoto wakati wa kujifungua” 
Aidha, Makamu wa Rais alitaka kila kifo cha mama wakati wakujifungua lazima kijadiliwe vizuri na ikionekana kama kulikuwa na uzembe hatua zichukuliwe kama itakavyostahili.
Awali akimkaribisha Makamu wa Rais, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alisema katika kuimarisha uzazi salama kwa kina mama, upatikanaji wa dawa zote za uzazi salama umeimarika na zinapatikana kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali.
“Hivi sasa ukipita katika vituo vyetu vya Afya  vya Serikali angalau  utakuta dawa zote muhimu  tunashukuru kwa kazi kubwa unayofanya ya kuzungumzia umuhimu wa kuboresha huduma za Afya nchini. 
Katika matembezi  yaliyofanyika mwaka jana shilingi Bilioni 290 zilikusanywa na kuwekwa kwenye fungu la kusomesha  wakunga 75 kwa ngazi ya cheti.

MAKAMU WA RAIS MH. SAMIA SULUHU AFUNGUA MATEMBEZI YA HISANI YENYE LENGO LAKUKUSANYA FEDHA KWAAJILI YA MAFUNZO YA UUGUZI NA UKUNGA.


Mgeni rasmi Mh. Samia Suluhu akiongoza matembezi ya Hisani yenye lengo la kukusanya Fedha zitakazo saidia kugharamia mafunzo ya uuguzi na ukunga mapema leo.









Meza Kuu ikiongozwa na Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu mapema leo katika Matembezi ya Hisani yenye lengo la kukusanya Fedha zitakazo saidia kugharamia mafunzo ya uuguzi na ukunga katika viwanja vya Green ground jijini  Dar es salaam. Kushoto kwake ni Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu (MB).
Wadau kutoka taasisi mbali mbali wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mh. Samia Suluhu (hayupo kwenye picha) katika Matembezi ya Hisani yenye lengo la kukusanya Fedha zitakazo saidia kugharamia mafunzo ya uuguzi na ukunga.





 

Mgeni rasmi Makamu wa Rais Mh, Samia Suluhu akikabidhi cheti kwa mmoja kati ya wadau alieshiriki kukamilisha kwa shughuli hiyo ya Matembezi ya Hisani yenye lengo la kukusanya Fedha zitakazo saidia kugharamia mafunzo ya uuguzi na ukunga, yaliyofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu (wakulia) akimuonesha zawadi Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu (wakwanza kushoto) aliyokabidhiwa kutoka Shirika la Amref katika siku ya Matembezi ya Hisani yenye lengo la kukusanya Fedha zitakazo saidia kugharamia mafunzo ya uuguzi na ukunga.




Picha ya Pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Mh. Ummy Mwalimu (MB) wakati wa Matembezi ya Hisani yenye lengo la kukusanya Fedha zitakazo saidia kugharamia mafunzo ya uuguzi na ukunga yaliyofanyika mapema leo viwanja vya Green ground jijini  Dar es salaam.



Ijumaa, 3 Novemba 2017

TFDA IMETAKIWA KUBORESHA UDHIBITI WA UINGIZAJI WA VYAKULA NA DAWA KIHOLELA

- Hakuna maoni




Na WAMJWW
Mamlaka ya Chakula , Dawa na Vipodozi TFDA imetakiwa kuboresha udhibiti wa uingizaji wa  Dawa, Vipodozi na Chakula nchini  kiholela ili kulinda afya ya Watanzania .
Hayo yamesemwa  na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa kuzindua CHETI CHA MFUMO WA UHAKIKI UBORA WA HUDUMA KATIKA KIWANGO CHA KIMATAIFA CHA ISO 9001-2015 leo jijini Dar es Salaam.
“Dawa ni kitu nyeti sana, hatuwezi kuruhusu dawa feki kuingia nchini, mnafanya kazi nzuri sana katika nyanja hii  na muendelee na mpango huu ili kudhibiti uingizaji wa vyakula visivyokidhi viwango na mahitaji ya watanzania, ” alisema Dkt.  Ndugulile.
Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa TFDA wanatakiwa kuzingatia muongozo wa kupitisha vyakula na vipodozi kwenye mipaka ya nchi kwa kuzingatia ubora na viwango vilivyoweka katika kudhibiti uingizaji mbovu wa vyakula.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bw. Hiiti Silo amesema kuwa ili kuendelea kukidhi matakwa ya wateja na mahitaji yao wameamua kuendana na kiwango cha kimataifa na kuwaita ISO kuja kuhakiki ambapo wamefanikiwa kukidhi na kupata cheti.
“Shirika la Viwango la Kimataifa ISO limehakiki ubora wa huduma zetu katika kukidhi mahitaji na matakwa ya watumiaji wa huduma zetu na kutupatia cheti kinachoturuhusu kutoa huduma nchini” alisema Bw. Silo.
Aidha Bw. Silo amesema kuwa wapo bega kwa bega na Serikali ya awamu ya tano ianyoongozwa na Rais Dkt. John pombe Magufuli katika kusogeza mbele gurudumu la afya hapa nchini kupitia taasisi  ya TFDA.

WAZIRI UMMY ASEMA WANANCHI WASIUZIWE DAMU

- Hakuna maoni


Na WAMJWW.
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  ameendelea kusisitiza kuwa wananchi hawapaswi kununua damu kwani huduma hiyo ni bure kwa watanzania wote katika hospitali zote.
Hayo amezungumza leo jijini Dar es salaam  wakati wa  uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait katika Taasisi ya Mifupa MOI ambapo uliuzuliwa na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania.
“Watanzania wanahoitaji huduma ya kuongezewa damu wapewe bure marufuku kwa watoa huduma za vituo vya afya pamoja na hospitali zote kuuza damu hiyo kwani inatoka kwa wananchi wenyewe” alisisitiza Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa wananchi wanatakiwa kujitokeza katika kuchangia damu ili kuweza kuwa na hifadhi ya kutosha na kufanya kazi kwa wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo kwa wakati sahihi bila ya usumbufu wowote katika kuokoa maisha ya watanzania.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema  kuwa anayo furaha kutimiza miaka miwili tangu kuingia kwa Serikali ya awamu ya tano kwa kupiga hatua katika sekta ya afya hasa katika kupunguza rufaa za nje na kuwa na utaalamu wa matibabu ya kibingwa kama vile upandikizaji wa figo, vifaa vya usikivu( Coclea Impant) na kutibu magonjwa ya moyo.
Kwa upande wake Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem amesema kuwa  wameamua kuchangia kiasi cha fedha cha shilingi Milioni 200 katika kutengeneza Benki hiyo ya damu MOI ili kuweza kusaidia kuboresha sekta ya afya nchini.
“Mbali na kiasi hicho cha fedha pia tumetoa Dola za Kimarekani 500 ili kuweza kusaidia  walemavu mbalimbali katika kulejesha hali zao za kawaida hapa nchini” alisema Bw. Al-Najem.
Aidha katika uzinduzi huo wa Benki ya damu Balozi Al-Najem alijitolea damu unit moja ili kuweza kuchangia benki hiyo ya taasisi ya Mifupa MOI ili kuweza kuhamasisjha na wananchi wengine waweze kuchangia damu kwa msaada wa wagonjwa wengine.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Lwezimula alisema kuwa katika kuhakikisha Matibabu ya kibingwa yanapiga hatua nchini waliamu kuanzisha kambi za matibabu kuanzia mwaka 2000 na kufanya taasisi zingine za afya kuiga mfano huo.
“Tunataka kuhamasisha matibabu ya kibingwa kufanyika nchini pamoja na uchangiaji damu kwani damu hiyo haitatumika MOI peke yake bali hata kwenye Taasisi zingne na vituo vya Afya nchini kote” alisema Dkt. Lwezimula.
Sambamba na tukio hilo Kikundi cha Kutayarisha Madereva wa Magari Makubwa  Wanawake (WOW) Afrika Mashariki walijitolea kuchangia damu ili kuweza kusapoti benki hiyo kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo ya damu.
“Tumehamasika kuja kuchangia damu ili kuweza kutoa mfano kwa wanachi wengie waweze kujitolea katika uchangiaji huu wa damu ili kujenga taifa lenye watu wenye afya bora” alisema Mkurugenzi wa WOW Bw. Martin Gabone.
- Hakuna maoni

Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliyesimama akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa nchini MOI wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es salaam, Kulia ni Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem.




Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem aliyesimama akiongea na baadhi ya  wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa nchini MOI wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es salaam , katikati waliokaa ni Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na anayefuata ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Lwezimula.




Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem kulia akimkabidhi zawadi ya mchango mkubwa katika Wizara ya Afya Mhe. Ummy Mwalimu kushoto wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es salaam.





Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizindua Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es salaam akiwa na Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem.






Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem akichangia damu katika Benki ya damu mpya iliyozinduliwa na Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi huo uliyofanyika leo jijini Dar es salaam.





Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa MOI  Dkt. Respicious Lwezimula aliyesimama akiongea na baadhi ya  wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa nchini MOI wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es salaam, kulia aliyekaa ni Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.




Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa nchini MOI wakimsikiliza kwa makini ni Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es salaam.





Mwanachama wa Kikundi cha Kutayarisha Madereva wa Magari Makubwa  Wanawake (WOW) Afrika Mashariki Bi. Rehema Mwangolombe akiwa katika maandalizi ya kuchangia damu  damu katika Benki ya damu mpya iliyozinduliwa na Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi huo uliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

DKT. FAUSTINE NDUGULILE AZINDUA CHETI CHA MFUMO WA UHAKIKI UBORA WA HUDUMA KATIKA KIWANGO CHA KIMATAIFA CHA ISO 9001-2015.

- Hakuna maoni
Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati akizindua CHETI CHA MFUMO WA UHAKIKI UBORA WA HUDUMA KATIKA KIWANGO CHA KIMATAIFA CHA ISO 9001-2015 tukio lililofanyika katika viunga vya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.





Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa maelekezo mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA)  Hiiti Sillo wakatikati na Mwenyekiti wa Bodi ya TFDA Dkt Ben Moses.







Picha ya pamoja ya meza kuu ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakiwa wameshishika cheti cha mfumo wa Uhakiki Bora katika Kiwango cha Kimataifa Cha Iso 9001-2015.







Meneja Uchunguzi wa Dawa na Vipodozi Dkt. Yonah Hebron akitoa maelekezo mbele ya Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile wakati akitembelea maabara katika viunga vya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, kulia kwa Naibu Waziri ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA)  Hiiti Sillo.





Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakwanza kushoto akisindikizwa na Mkurugenzi Mkuu TFDA wapili,  Mwenyekiti wa Bodi ya TFDA Dkt. Ben Moses wa tatu, na wa mwisho ni Meneja uchunguzi wa chakula  Dkt. Mziray.









Alhamisi, 2 Novemba 2017

SHIRIKA LA KIMATAIFA LA HELPAGE LAAHIDI KUWASAIDIA WAZEE WA TANZANIA





Na WAMJWW
Bodi ya Shirika la kimataifa la HelpAge yaahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili wazee wa Tanzania ikiwemo ukatili dhidi ya vikongwe.
Hayo yamesemwa na  Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mh. Arun Maira wakati alipokutana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu mapema leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam.
Mh.  Arun Maira ameipongeza Serikali ya awamu ya tano chini ya Raisi Dkt. John Magufuli kwa jitihada kubwa anayofanya  katika kusimamia ustawi na maendeleo ya Wazee hususani katika masuala ya huduma ya Afya.
Aidha Mh. Arun Maira aliahidi kuimarisha ushirikiano na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto  kwa kusaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa wazee kupitia utekelezaji wa mkakati wa kutokomeza mauaji ya Wazee mara tu utakapokamilika.
Mh. Arun Maira aliendelea kusisitiza kwamba changamoto hizi za Wazee ikiwemo suala la ukatili wataliweka kama moja ya vipaumbele katika mpango kazi wao  ili kuwezesha utekelezaji  huo.
Nae Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu aliwashukuru wajumbe hao wa bodi ya Shirika la kimataifa la HelpAge kwa kutatua changamoto mbali mbali zinazowahusu wazee  wa Tanzania  hususani katika kusaidia kampeni ya “Mzee kwanza”.
Mwisho Mh. Ummy aliiomba bodi hiyo kuweka nguvu zaidi katika suala la ulinzi wa wazee hususani  katika utekelezaji wa mkakati wa kuzuia mauaji na ukatili wa vikongwe kupitia mkakati wa kutokomeza mauaji ya wazee.

BAROZI WA JAPAN NCHINI AFANYA MAZUNGUMZO NA MH. UMMY MWALIMU (MB).



Na WAMJWW 
Barozi wa Japan nchini Tanzania Mh.Masaham Yoshida  mapema leo amefanya mazungumzo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam, lengo likiwa ni kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili hususani katika masuala za huduma ya Afya.
Mh.Masaham Yoshida  ameahidi kuisaidia Sekta ya Afya kupitia mradi wa “SUMITOMO CHEMICAL PROJECT” wenye lengo la kuangamiza mazalia ya mbu kwa kutumia Viuwadudu, mradi huo umeanza kufanya kazi katika maeneo ya Nyanja ya juu Kusini katika Mkoa wa Mbeya. Hata hivyo Mh.Masaham Yoshida ameahidi kuendeleza ushirikiano huo na Serikali ya Tanzania.
Nae Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu ameshukuru ugeni huo kutoka Japan ulio na tija kwa taifa la Tanzania katika Sekta ya Afya  huku akisisitiza na kuweka  mkazo katika ushirikiano huo ili kusukuma gurudumu la maendeleo ya Sekta ya Afya nchini.



Jumatano, 1 Novemba 2017

WAWEKEZAJI WA NDANI WANAOTAKA KUJENGA VIWANDA VYA DAWA WAHIMIZWA KUFUATA VIGEZO VYA UZALISHAJI





Na WAMJWW 

Wawekezaji wa ndani wanao taka kujenga viwanda vya dawa wahimizwa kuhakikisha wanakidhi  vigezo vya uzalishaji wa dawa ili kuweza kuruhusiwa kufanya shughuli hiyo ya uzalishaji wa dawa.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati  AKIZINDUA MAABARA HAMISHIKA  ZAKUDHIBITI UBORA NA USALAMA WA DAWA MAPEMA leo katika viunga vya mamlaka ya dawa, chakula na Vipodozi (TFDA)
Aidha Mh. Ummy ameahidi kuongeza jitihada za kudhibiti ubora, usalama, na ufanisi wa bidhaa hasa dawa kwa kuimarisha mpango mahususi wa uchunguzi wa awali wa Dawa  mbao ulianza 2002 unaohusu uchunguzi wa Dawa muhimu za Kifua kikuu, Dawa za ARV, Dawa za Maleria pamoja na Viuwa sumu.
Kwa upande mwingine  Mh. Ummy amesisitiza athari za uwepo wa dawa zisizo na ubora katika jamii ikiwepo kuhathiri  uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa kiujumla kutokana na kmanunuzi ya  Dawa zisizo na uwezo wa uwezo wa kutibu mwisho hupelekea usugu wa Dawa katika mwili.
Waziri Ummy hakusita kuipongeza Bodi , Uongozi na wafanyakazi  wa TFDA kwa utendaji  mzuri wa  kazi huku akiahidi kuendelea mkuwaunga mkono kwa kushirikiana nao kwa ukaribu katika safari ya kumsaidia Raisi wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Magufuli.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA)  Hiiti Sillo alisema kuwa kutokana na kuongezeka kwa Maabara hamishika itasaidia kuwabaini na kuwakamata wahalifu wanaofanya biashara hiyo ambayo inahathiri jamii na uchumi kiujumla.
“Mwaka 2005 wastani wa dawa bandia ulikuwa 3.7 wa dawa zilizokuwepo huku takwimu za 2017 imeshuka  kwa chini ya 1%” , alisema Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA)  Hiiti Sillo,  huku akisema mafanikio hayo yanatokana na ufuatiliaji wa umakini unaofanywa na taasisi hiyo.
Bw. Hiiti Siilo aliendelea kwa kusema kwamba katika utekelezaji wa majukumu yake TFDA imepanga kupeleka maabara hizo katika ofisi za kanda ambazo hazikuwa na huduma hiyo ikiwemo ofisi ya Tabora, Hospitali ya Mbeya na  Mtwara huku nyingine zitapelekwa katika vituo vya Forodha Namanga,KIA mpakani, Silali (Tarime) na Mutukula (Kagera) bila kusahau Geita na Katavi, alisisitiza Bw. Sillo.

MH. UMMY MWALIMU (MB) AZINDUA MAABARA HAMISHIKA ZAKUDHIBITI UBORA NA USALAMA WA DAWA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maabara hamishika hizo, wakwanza kushoto ni mwakilishi kutoka WHO Dkt. Matthius Kamwa, watatu kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya TFDA Bi. Zainabu na wa mwisho ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Hiiti B. Sillo.







Meza kuu katika picha yapamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa maabara hamishika mapema leo katika ofisi za Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi.







Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya meza kuu na wageni wa alikwa, tukio lililojiri katika viunga vya Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA).







 Watumishi wa umma na wageni waalikwa wakiwa wakifuatilia kwa ukaribu taarifa iliyokuwa ikiwasilishwa na Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu(MB) hayupo kwenye picha, mapema leo katika uzinduzi wa Maabara hamishika uliofanyika katika ofisi za TFDA.







Mh. Ummy Mwalimu akipata maelekezo kuhusu Maabara hamishika hiyo wakati wa uzinduzi wa maabara hamishika mapema leo katika ofisi za Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi wa kwanza kushoto ni mwakilishi kutoka WHO Dkt. Matthius Kamwa.