Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 13 Februari 2019

SERIKALI YAANZISHA HUDUMA ZA KIBINGWA MATIBABU YA MOYO DODOMA.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (aliye mbele) akizindua rasmi maabara ya uchunguzi na tiba ya magonjwa ya moyo (Cathlab) katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma walio kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce chandika.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akielekezwa namna magonjwa ya moyo yanavyochunguzwa katika maabara ya uchunguzi na tiba ya moyo Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini  Dodoma

Picha ya pamoja Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na wataalam wa uchunguzi na tiba ya magonjwa ya moyo kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Dsm.

Mashine ya uchunguzi na tiba ya moyo (Cathlab) katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Zainab Chaula akisisitiza jambo kwenye halfa ya uzinduzi wa Maabara ya uchunguzi na tiba ya magonjwa ya Moyo. 

Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika akisisitiza jambo kwenye halfa ya uzinduzi wa Maabara ya uchunguzi na tiba ya magonjwa ya Moyo. 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo kwenye halfa ya uzinduzi wa Maabara ya uchunguzi na tiba ya magonjwa ya Moyo. 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisalimiana na wananchi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma alipoenda kuzindua Maabara ya Uchunguzi na Tiba ya Magonjwa ya Moyo (Cathlab)

Na WAMJW – Dodoma. 

Katika azma ya kuboresha huduma za kibingwa za matibabu, Serikali kupitia Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma imeanzisha huduma za matibabu ya moyo kwenye maabara ya uchunguzi na tiba ya magonjwa ya moyo kwa kutumia mashine maalum (Cathlab).

Maabara hiyo ya tatu nchini na ya pili kwenye taasisi ya serikali inatarajiwa kutoa huduma za uchunguzi na tiba ya magonjwa ya moyo ndani ya muda mfupi hivyo kuhudumia wagonjwa wengi ndani ya muda mfupi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa maabara hiyo, mgeni rasmi Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa kufunguliwa kwa maabara hiyo ni mafanikio makubwa kwa serikali katika kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi hivyo kupunguza idadi ya wagonjwa waliokuwa wakisafiri kwenda mbali kufuata huduma za matibabu.

“Huduma za kibingwa zimepunguza idadi ya wagonjwa waliokuwa wanasafiri au kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu kwa asilimia 95 kutokana na uboreshaji wa huduma za afya ndani ya nchi” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali imekuwa ikiwajengea uwezo wataalam wa afya nchini ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi jambo ambalo limezaa matunda kwa kuwa wagonjwa wengi hivi sasa wanapata matibabu ndani ya nchi.

Hata hivyo Waziri Ummy ametoa ufafanuzi wa upatikanaji wa rufaa ya matibabu nje ya nchi na kusema kuwa Serikali haijazuia rufaa za matibabu nje ya nchi bali ni lazima kujiridhisha kwanza huduma za matibabu hazipatikani hapa nchini kabla ya kutoa rufaa.

“Hakuna daktari tuliyemkataza kutoa rufaa nje ya nchi, sasa hivi tuna uwezo wa kutoa huduma za matibabu ya kibingwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni lazima daktari awe amejiridhisha na kuthibitisha kwamba matibabu hayo hayapatikani hapa nchini kabla ya kutoa rufaa” alisema Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy ameupongeza uongozi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa na Taasisi ya Jakaya Kikwete kwa kuwa wabunifu na kushirikiana kutoa huduma bora za matibabu ya moyo kwa wananchi na kuzitaka hospitali na taasisi nyingine za afya kuiga mfano wao katika kuboresha huduma za afya nchini.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amewataka wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya ili waweze kupata bima ya afya ambayo itawasaidia kupata huduma za matibabu kwa uhakika. Waziri Ummy amesema kuwa ni muhimu kwa watanzania kuwa na bima ya afya ambayo itawapunguzia gharama za matibabu huku akiwataka wananchi kujiwekea malengo na kukata bima ya afya ambayo gharama zake ni nafuu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula amesema kuwa ipo haja ya kuwathamini madaktari wazalendo ambao wamekuwa wakijitoa kuokoa maisha ya wagonjwa. Dkt Chaula amesema kuwa Serikali itaendelea kuwekeza katika wataalam wa afya nchini ili kuweza kuwa na madaktari bingwa wengi wanaotoa huduma za kibingwa hapa hapa nchini pamoja na kuwekeza kwenye miundombinu na vifaa.

Awali akitoa salamu zake, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi, ametoa rai kwa wananchi kuzingatia mtindo bora wa maisha, kufanya mazoezi na kula chakula bora ili kuepukana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza yakiwemo kisukari, presha na shinikizo la damu.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika amesema kuwa maabara hiyo imegharimu kiasi cha Tsh Bilioni 5 na inatarajiwa kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo hivyo kupunguza adha ya wagonjwa kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za matibabu ambapo awali zilikuwa zikipatikana Dar Es Salaam kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete pamoja na Hospitali nyingine moja isiyo ya kiserikali.

Dkt. Chandika amesema kuwa wataendelea kushirikiana na wataalam kutoka Taasisi ya Moyo ya jakaya Kikwete ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi huku akiiomba serikali kuongeza wataalam ili kuboresha zaidi upatikanaji wa huduma za afya.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi amesema kuwa hadi kufikia jioni jumla ya wagonjwa 13 kutoka Dodoma na mikoa ya jirani tayari walishakuwa wamefanyiwa uchunguzi katika maabara hiyo ambapo kati yao  wagonjwa wanne wakitakiwa kwenda JKCI kwa uchunguzi na tiba zaidi.

Aidha Prof. Janabi alitumia nafasi hiyo kuishukuru Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kuwapa nafasi na heshima kubwa ya kuja kushirikiana katika kutoa huduma za matibabu kwa wananchi.

Mwisho


Jumanne, 12 Februari 2019

DKT. NDUGULILE AKASIRISHWA NA KASI YA UJENZI WA MAABARA YA AFYA YA JAMII

Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifanya ukaguzi wa chumba kwa chumba ili kujidhisha na maendeleo ya ujenzi wa jengo la Maabara ngazi ya tatu yenye uwezo wa kuchukua vipimo vya magonjwa hatari Duniani kama Virusi vya Ebola, Mabag n.k, unaojengwa  katika eneo la Mabibo jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongoza katika ziara ya kukagua ujenzi wa jengo la Maabara ngazi ya tatu yenye uwezo wa kuchukua vipimo vya magonjwa hatari Duniani kama Virusi vya Ebola, Mabag n.k, leo katika eneo la Mabibo jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (Wakwanza Kulia) akipata maelezo ya mradi ulipofika kutoka kwa Meneja Mradi (Wapili kutoka kushoto) wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa jengo la Maabara ngazi ya tatu yenye uwezo wa kuchukua vipimo vya magonjwa hatari Duniani kama Virusi vya Ebola, Mabag n.k, leo katika eneo la Mabibo jijini Dar es salaam.

Muonekano wa jengo la Maabara ngazi ya tatu lenye  uwezo wa kuchukua vipimo vya magonjwa hatari Duniani kama Virusi vya Ebola, Mabag n.k, jengo hilo lililokamilika kwa 90%, linajengwa katika eneo la Mabibo jijini Dar es salaam.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile baada ya ukaguzi wa ujenzi wa jengo la Maabara ngazi ya tatu yenye uwezo wa kuchukua vipimo vya magonjwa hatari Duniani kama Virusi vya Ebola, Mabag n.k, unaojengwa  katika eneo la Mabibo jijini Dar es salaam.


DKT. NDUGULILE AKASIRISHWA NA KASI YA UJENZI WA MAABARA YA AFYA YA JAMII.

Na WAMJW - DSM
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amekasirishwa na kasi ndogo ya ujenzi wa Maabara  ya Afya ya Jamii ngazi ya tatu, inayoshughurikia magonjwa hatari ya mlipuko kama vile Ebola, Mabag, Kipindupindu hali inayopelekea  kuchelewesha utoaji wa huduma hizo kwa Wananchi.

Hayo yamejiri leo wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa jengo hilo lililo eneo la Mabibo jijini Dar es salaam  ili kujidhihirishia thamani ya pesa zilizotumika na kiasi cha ujenzi wa jengo hilo ulipofika.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa haoni sababu ya msingi iliyopelekea kuchelewa kukamilika kwa ujenzi wa Maabara hiyo kwani fedha zote zipo, hivyo kukasirishwa kwa kasi ndogo ya ujenzi wa Maabara hiyo ulioanza tangu mwaka 2016.

" Nitoe asikitiko yangu kwamba, kazi hii imechukua muda mrefu sana, tangia 2016, wenzetu waliozipata fedha hizi wengi wamekwisha kamilisha kazi zao, sisi Tanzania bado tunasua sua, kibong'oto, Temeke, Mawenzi na hapa, najambo linalonisikitisha sana fedha tunazo" alisema Dkt. Ndugulile

pia, Dkt. Ndugulile amesema kuwa ujenzi wa Maabara hiyo utaisaidia Serikali kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho inakipeleka nje ya nchi kwaajili yakupima sampuli za magonjwa hayo, hivyo kukamilika kwa Maabara hiyo kutaifanya Tanzania kuwa moja kati ya nchi chache barani Afrika inayotoa huduma hizo.

Aidha, Dkt Ndugulile ameonekana kutoridhishwa na usimamizi wa ujenzi wa Maabara hiyo, hivyo kutoa onyo katika matumizi ya fedha za ujenzi wa Maabara hiyo, hii ni kutokana na kufanya marekebisho ya mara kwa mara wakati ramani ya jengo hilo ipo.

"Fedha tunazo nyingi kupita maelezo, na ndiomaana mnaishia kuzitumia vibaya, matumizi ya hovyo yanapitishwa kwa haraka sana, lakini matumizi ya msingi yanasuasua, sasa niombe kwa niamba ya Kazi zote, hizi fedha tuliziomba kwa matumizi mahsusi kujenga hizi Maabara na isolation centers, naomba nitakaporudi haya tuliokubaliana mtimize" alisema Dkt Ndugulile

Kwa upande mwingie Dkt. Ndugulile amewata viongozi wa Wizara ya Afya kutokuwa kikwazo katika taratibu za ujenzi wa Maabara hiyo, ili kuepusha lawama kutoka kwa Wakandarasi, jambo litalosaidia katika kasi ya ujenzi wa Maabara hiyo.

"Taratibu za ndani, sisi kama Wizara naomba zisiwe kikwazo kwakweli, kwasababu gharama za mradi mnazijua, uendeshaji tunaujua, na tulikuwa tunazifahamu, fedha tunazo zakutosha, mzipitishe katika taratibu zake zote ili hawa Wakandarasi wasije kutulalamikia" Alisema Dkt. Ndugulile

Mwisho.

TANZANIA MBIONI KUNUFAIKA NA TEKNLOLOJIA YA SELI SHINA


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa IPP Dkt. Reginald Mengi (kulia) kwenye mkutano wa wadau wa afya Jijini Dar Es Salaam.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akisalimiana na wadau wa sekta ya afya.

Na Mwandishi Wetu - Dar Es Salaam.

Teknolojia ya Seli Shina (Sterm Cell) ambayo inatumia chembechembe za seli za mwanadamu kutibu kiungo chochote katika mwili husika, inatajwa kuwa na uwezo mkubwa wa kutibu magonjwa mpaka yasiyoambukiza yakiwemo saratani zote, utindio wa ubongo, seli mundu, kisukari, ualbino na kupooza.

Akizungumza kwenye mkutano wa kwanza wa kimataifa wa wataalamu wa tiba za magonjwa ya binadamu jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa IPP, Dk. Reginald Mengi, alibainisha tiba hiyo ya seli shina ina uwezo mkubwa na tayari imethibitika duniani kumrudisha mtu aliyefika hatua ya uzee kuwa kijana mwenye afya njema.

Dk. Mengi kupitia kampuni yake ya IPP - Utafiti, Teknolojia na Ugunduzi, akishirikiana na wataalamu mbalimbali duniani, amesema ataanzisha maabara hiyo jijini Dar es Salaam, ambapo hatua iliyofikiwa mpaka sasa ni upatikanaji wa vibali kutoka serikalini.

Alisema kuanzishwa kwa maabara hiyo hakuna maana kwamba anapingana na uumbaji wa Mungu kuwa ni lazima binadamu afe, lakini lengo ni kuhakikisha wale wanaopitia maumivu na tabu kubwa kutokana na kukosa tiba ya magonjwa yanayowasumbua yakiwemo yanayotokana na umri mkubwa wanapata tiba hapa hapa nchini.

Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, alisema serikali haina tatizo juu ya hilo, kwa sababu ni maendeleo makubwa kwenye sekta ya afya nchini na kumtoa hofu Dk. Mengi kuwa vibali hivyo vitapatikana haraka.

Lakini pia alisema kuwa serikali imetumia nguvu kubwa kuboresha sekta ya afya kwenye uboreshaji miundombinu na kuanzisha tiba mpya ambazo awali hazikuwepo hapa nchini ikiwemo upandikizi wa figo, uongezaji wa bajeti, upandikizi wa ini na ute wa mifupa 'Bone Marrow'.

Alisema tiba ya seli shina ni ya kisasa, ikiwa na uwezo mkubwa wa kutibu mtu kutokana na seli zake mwenyewe lakini alitahadharisha kuwa kwenye kila hatua ya tiba hiyo lazima maadili yazingatiwe na miiko ya kitabibu kama zinavyoelekeza kanuni za kada hiyo kote duniani.

Dk. Ndugulile alisema serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kwenye uboreshaji wa sekta ya afya ili kuhakikisha kunakuwa na kasi kubwa ya maendeleo kwenye eneo hilo lililo uti wa mgongo wa maendeleo ya sekta zingine zinazotengemea nguvu kazi ya binadamu kwenye ukuaji wake.

Kwa upande wake Dk. Michael Magoti ambaye ni Mratibu mipango wa IPP Utafiti, Teknolojia na Uvumbuzi, alisema mkutano huo wa kwanza wa kimataifa umejumuisha wadau wa tiba kutokana nchi za Marekani, Australia, India, Thailand, Vietnam na Egypt.

Alisema pamoja na maabara ya utafiti, Dk. Mengi kupitia kampuni yake ya IPP Utafiti, Teknolojia na Uvumbuzi ana mpango wa kuanzisha kliniki ya tiba kwa watoto wenye utindio wa ubongo ambayo itasaidia sehemu kubwa ya watoto wanaozaliwa na matatizo ya kiakili kwa kutumia matibabu ya seli shina hapa nchini.

Naye Profesa Dk. Kampon Sriwatanakul, raia wa Thailand ambaye pia ni mtaalamu mshauri wa teknolojia hiyo ya tiba kutoka IPP, alisema amejitoa kuja Tanzania kumsaidia Dk. Mengi kufikia ndoto yake ya kuwafikia mamilioni ya watu wenye shida za kiafya ambazo tayari wamekata tamaa ya kupona.

Alisema kupitia teknolojia ya tiba ya seli shina, wana uwezo mkubwa wa kutibu magonjwa mengi sugu ambayo kwa tiba za kawaida imeaminika kuwa hayawezekani kwenye hospitali nyingi kubwa zikiwemo zile za kimataifa zisizotumia teknolojia hiyo ya kisasa ya tiba.

Katika mkutano huo, jumla ya mada tisa zinazohusiana na tiba ya seli shina ziliwasilishwa na wataalamu waliobobea kwenye kada ya afya kutoka nchi kadhaa za Ulaya, Marekani na Asia.

Jumamosi, 9 Februari 2019

WAZIRI UMMY AWAONGOZA WATUMISHI WA SEKTA YA AFYA KATIKA ZOEZI LA UPANDAJI MITI

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akijiandaa kupanda mti, wakati  wa zoezi la upandaji miti katika Mazingira ya jengo la Wizara ya Afya lililo katika mji wa Serikali katika kata ya Mtumba jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akimwagilia maji mti wake aliopanda, wakati  wa zoezi la upandaji miti lililo fanywa na Watumishi wa Wizara ya Afya katika mji wa Serikali ulio kata ya Mtumba jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akimwagilia maji mti alioupanda katika Mazingira ya Wizara ya Afya, yaliyo katika Mji wa Serikali uliopo katika kata ya Mtumba jijini Dodoma.

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi akiweka mbolea katika mti wake, katika Mazingira ya jengo la Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto lililo katika mji wa Serikali uliopo katika kata ya Mtumba jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula (Wakatikati) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku  (Wakulia) na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi (Wakwanza kushoto)

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akifanya ukaguzi wa jengo la Wizara ya Afya lililo katika hatua ya mwisho, leo wakati wa zoezi la upandaji miti katika Mazingira ya jengo la Wizara ya Afya lililo katika mji wa Serikali katika kata ya Mtumba jijini Dodoma.

Muonekano wa jengo la Wazara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto lililo katika mji wa Serikali uliopo katika kata ya Mtumba jijini Dodoma,  jengo hilo liko katika hatua ya mwisho ya ujenzi,


Na WAMJW - DOM
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu leo amewaongoza Watumishi wa Wizara ya Afya katika zoezi la upandaji miti katika mji mpya wa Serikali ulio katika kata ya  Mtumba, tarafa ya Kikombo Jijini Dodoma.

Katika zoezi hilo Waziri Ummy ameagiza Watumishi wote waliohusika katika upandaji wa miti hiyo kuhakikisha wanaitunza vizuri isitawi, na ameagiza kila mtu kuchukua jukumu hilo.

"Hii miti ambayo tumeipanda sio tu miti ya kivuli na mapambo tu, bali imejumuisha miti ya matunda. Miti hii ambayo tunaipanda ili ikue na kustawi, lazima kila mtu, ambae amepanda mti wake kuhakikisha kwamba haufi" Alisema Waziri Ummy.

Mbali na hayo, Waziri Ummy amemwagiza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula kutenga maeneo kwa ajili ya Watumishi kufanya mazoezi ikiwa ni mpango wa Serikali ya awamu ya Tano kupambana na Magonjwa yasiyo yakuambukiza.

"Mazingira ya hapa ni mazuri kweli kutembea, ukizunguka huu mji hukosi Kilomita 5, nitamwandikia Waziri  Jenister atusaidie kuwa na mabafu kwa ajili ya watu wanaofanya mazoezi kubadilisha nguo jioni, ni lazima sehemu za kazi ziwe rafiki kwa watu kufanya mazoezi" alisema Waziri Ummy.

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amempongeza Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula na kikundi chake kwa kuja na wazo la upandaji wa miti katika mji huo, na kuwa mfano wa kuigwa na Wizara nyingine.

Katika zoezi hilo lililojumuisha viongozi mbalimbali wa wizara, jumla ya miti 470 imepandwa katika awamu ya kwanza, lengo ikiwa ni kupanda miti 525. Miti 320 iliyopandwa ni ya matunda, na mingine ni kwa ajili ya mapambo na kivuli.

Jumatano, 6 Februari 2019

MAAMBUKIZI YA UGONJWA TRACHOMA YAPUNGUA KWA ASILIMIA 75 NCHINI





Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akihutubia wageni waliofika katika uzinduzi wa mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokua hayapewi kipaumbele hususan Vikope (Trachoma) katika ukumbi wa Hotel ya Morena jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi cheti Harran Mkocha ambaye ni Mkurugenzi wa Kongwa Trachoma Project kutambua mchango katika mapambano dhidi ya kutokomeza ugonjwa wa Trachoma nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa The Queen Elizabeth Diamond Trust Fund Dkt. Astrid Bonfield na kulia ni Balozi wa Uingereza Nchini Sarah Cooke.
Wataalamu mbalimbali kutoka Taasisi ya The Queen Elizabeth Diamond Trust Fund na SightServers Tanzania pamoja na wawakilishi kutoka Wizara ya Afya wakiwa katika picha ya pamoja katika kijiji cha Bahi-Makulu Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma kulipokua na zoezi la upimaji na matibabu ya ugonjwa wa Trachoma kwa wananchi mbalimbali wa maeneo hayo.
Madaktari wakimfanyia upasuaji mgonjwa wa Vikope (trachoma) ambaye alifikia hatua ya kuelekea upofu katika zahanati ya Bahi-Makulu wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipiga picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya SightServers Tanzania Bw. Gosbert Katunzi (Katikati), . Kushoto ni Mkurugenzi wa The Queen Elizabeth Diamond Trust Fund Dkt. Astrid Bonfield na kulia ni Balozi wa Uingereza Nchini Sarah Cooke.



NA WAMJW-DODOMA

Maambukizi ya ugonjwa wa vikope (Trachoma) yameonekana kupungua kwa zaidi ya aslimia 75 katika maeneo mbalimbali nchini.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa mpango wa taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokua hayapewi kipaumbele katika Ukumbi wa Hotel ya Morena jijini Dodoma.

Waziri Ummy amesema ugonjwa wa Vikope unawapata watu wa jamii ya kimasikini hasa wafugaji na pia jamii yenye changamoto ya upatikanaji wa maji safi.

“Trachoma ni ugonjwa ambao kwa kiasi fulani unahusiana na umaskini na unawapata watu wa jamii ya wafugaji lakini pia wakiwa na changamoto ya upatikanaji wa maji”. Alisema Waziri Ummy.

Aidha, waziri Ummy amesema katika kipindi cha miaka mitano serikali imekua ikishirikiana na serikali ya Uingereza kupitia taasisi ya UK aid na Queen Elizabeth Diamond Jubilee Trust katika kuhakikisha wagonjwa wa Vikope wanafikiwa na kupata huduma za matibabu pamoja na kufanyiwa upasuaji kwa wale ambao wanakaribia kupata upofu.

Waziri Ummy amesema bado kuna changamoto ya maambukizi katika wilaya nane ambazo ni Mpwapwa, Chemba, Kalambo, Songwe, Ngorongoro, Longido, Kiteto, na Simanjiro.

Hata hivyo katika kipindi cha miaka mitano wagonjwa wa Trachoma waliofanyiwa upasuaji wamepungua kutoka 160,000 mwaka 2010 hadi wagonjwa 17,000 mpaka mwezi Oktoba 2018, ambapo inatajwa kuwa ni hatua kubwa katika mafanikio ya kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huu.

Waziri Ummy amesema serikali iko katika hatua nzuri ya kuhakikisha inatokomeza maambukizi mapya ya Trachoma kwa kuendelea kutoa dawa katika wilaya nane zilizotajwa na kuwafanyia upasuaji wagonjwa ambao wamefikia hatua ya kupata upofu.

Naye balozi wa Uingereza nchini Bi. Sarah Cooke amesema serikali ya Uingereza kupitia taasisi ya Queen Elizabeth Diamond Jubilee Trust na shirika la SightServers itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kusaidia kutokomeza ugonjwa wa Trachoma nchini.

MWISHO

Jumanne, 5 Februari 2019

TUENDELEE KUSHIRIKIANA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Balozi Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima  waliohudumu Wizara ya Afya  kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile  akisisitiza jambo wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Balozi Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya  kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (kushoto) akiwa na Naibu wake Dkt. Faustine Ndugulile (kulia) wakifuatilia alichakuwa akiongea Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi (hayupo pichani) wakati wa hafla ndogo ya kuwaaga Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya  kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya  kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Idara ya Afya Dkt Dorothy Gwajima.

Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga  Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya  kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula, hafla ilofanyika katika ofisi za Wizara ya Afya jijini Dodoma.

Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Waziri Ummy  wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya  kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula. Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Wizara ya Afya jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisaini Biblia Takatifu aliyopewa kama zawadi Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya  wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Baozi Dkt Mpoki Ulisubisya Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya  kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula, hafla ilofanyika katika ofisi za Wizara ya Afya jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mhe.Ummy Mwalimu  akimkabidhi Zawadi Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa Hafla ndogo ya kumuaga yeye na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya  kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mhe.Ummy Mwalimu  akimkabidhi Zawadi Naibu Katibu Mkuu Idara ya Afya TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa Hafla ndogo ya kumuaga yeye na Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya waliohudumu Wizara ya Afya  kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula.

Wakwanza kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akifuatilia alichakuwa akiongea Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Balozi Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya  kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula (Wakatikati)  na (Wakwanza kishoto) ni Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Idara ya Afya Dkt Dorothy Gwajima.

Mkurugenzi wa MSD ambae pia ni mwakilishi wa Wakurugenzi wa Taasisi zote za Wizara ya Afya Laurean Bwanakunu akitoa salamu za taasisi zote za Afya wakati wa Hafla ndogo ya kuwaaga Dkt Mpoki Ulisubisya na Dkt. Dorothy Gwajima waliohudumu Wizara ya Afya  kabla yakuteuliwa katika nafasi nyingine, na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainab Chaula, hafla hiyo  imefanyika katika ofisi za Wizara ya Afya jijini Dodoma.


Na WAMJW - DOM
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo amewaongoza watumishi katika halfa fupi ya kumuaga rasmi aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Mpoki Ulisubisya ambae ameteuliwa kuwa Balozi, na aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Wizara ya Afya, ambaye amekuwa Naibu Katibu Mkuu Idara ya Afya TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima na kuwakaribisha Watumishi wapya wakiongozwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Idara ya Afya TAMISEMI Dkt. Zainab Chaula ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Afya na aliyekuwa Mganga Mkuu wa Dar es salaam ambaye kwa sasa ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara Tiba Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe

Katika hafla hiyo Waziri Ummy amewashukuru watumishi wote wakiongozwa na Dkt Mpoki Ulisubisya kwa ushirikiano waliouonesha katika kipindi chote walichofanya kazi Wizara ya Afya na kuwasihi kuendeleza uchapaji kazi ili kusukuma gurudumu la Maendeleo hususani maendeleo ya Sekta ya Afya.

Aidha, Waziri Ummy amewakaribisha Watumishi wote walioamia katika Wizara ya Afya, Waziri Ummy amesema kwamba licha ya mafanikio makubwa ambayo Sekta ya Afya imepiga, bado kuna changamoto nyingi ambazo zinapaswa kutatuliwa ikiwemo suala la uhaba wa watumishi, na upatikanaji wa Dawa na vifaa tiba.

Naye Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Fustine Ndugulile amewakumbusha Watumishi wa Sekta ya Afya juu ya uwajibikaji na kuwatoa hofu kuwa, kama Serikali milango yao ipo wazi muda wote, hivyo kwa yoyote mwenye wazo zuri la kujenga na kuipeleka mbele Sekta ya Afya asisite kuwaona.

Kwa upande wake, aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya amewashukuru Watumishi wote wa Sekta ya Afya wakiongozwa na Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu kwa ushirikiano waliomuonesha katika kipindi chote alichohudumu katika Wizara ya Afya, kisha kuahidi kuwa Balozi Mzuri huko atakoenda ili kuikuza Sekta ya Afya.

Naye, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula amewakumbusha Watumishi wa Sekta ya Afya juu ya umoja na ushirikiano baina yao, huku akisisitiza kila mmoja ni lazima ahakikishe anatimiza wajibu wake ili kusukuma mbele Maendeleo ya Sekta ya Afya.

Kwa upande wake, aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Wizara ya Afya ambae sasa ni Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Idara ya Afya Dkt Dorothy Gwajima ameahidi kuwa daraja zuri na imara baina ya Wizara ya Afya na TAMISEMI kutokana na kuzijua Wizara zote mbili kiundani na kuahidi kuendeleza mazuri yote yalioachwa na Dkt. Zainab Chaula.

Mwisho.


Jumatatu, 4 Februari 2019

WAUGUZI WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI KATIKA SEHEMU ZAO ZA KAZI


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa ameshika bango kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Kimataifa ya Uuguzi Sasa Kampeni inayolenga kuinua hadhi na muonekano wa kada ya uuguzi nchini.

Wadau wa Kampeni ya Uuguzi Sasa wakiwa wameinua mabango kuashiria kampeni hiyo kuzinduliwa rasmi.

Wauguzi wakisikiliza kwa umakini yanayoendela kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Uuguzi Sasa

Picha ya wadau wa kampeni ya uuguzi sasa waliojitokeza kwenue uzinduzi wa kampeni hiyo inayokenga kuinua hadhi na muonekano wa kada ya uuguzi nchini.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akimpongeza Mwalimu Mstaafu wa Kada ya Uuguzi  Mwl. justina Venant (kulia) kwa kumpatia cheti cha utumishi ulitukuka wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uuguzi Sasa.

Picha ya pamoja ya Viongozi na Watendaji wa Serikali pamoja na wadau wa Sekta ya Afya wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Uuguzi Sasa.


Na WAMJW - Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewataka wauguzi kutimiza wajibu wao na kutoa huduma bora wakati wa kazi kulingana na miongozo na maadili ya kazi ya uuguzi na ukunga.

Waziri Ummy ametoa agizo hilo leo Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kimataifa ya Uuguzi Sasa inayolenga kuinua hadhi na muonekano wa kada ya Uuguzi.

“Nataka kuona wauguzi wanafanya kazi kwa kuzingatia miongozo na maadili ya taaluma ya kada ya uuguzi na kuwa na heshima na utu kwa wagonjwa” alisema Waziri Ummy na kuendela “Nimefurahi kuona kwenye kampeni hii mmejipanga kuondoa changamoto zilizopo”

Aidha Waziri Ummy amewataka viongozi kuwatambua wauguzi ambao wamekuwa hawana kauli nzuri na kuwachukulia hatua ili kuondokana na vitendo vya wauguzi kutoa kauli za kebehi kwa wateja na kuwaasa wauguzi kuacha lugha za kebehi na zisizowafurahisha wateja kwani kufanya hivyo kuwachafua taswira ya wauguzi nchini.

Licha ya changamoto zilizopo Waziri Ummy hakusita kutoa pongezi kwa wauguzi ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika utoaji wa huduma za afya nchini. “Napenda kuwapongeza wauguzi wote kwa kazi mnayofanya, Kazi ya wauguzi wanne inafanywa na muuguzi mmoja, Kazi ya wakunga watano, inafanywa na mkunga mmoja” alisema Waziri Ummy.

Naye Rais wa Chama cha Wauguzi nchini Tanzania (TANNA) Bw. Paul Magesa amekiri kuwepo kwa baadhi ya wauguzi wasio na maadili katika kazi amabo wamekuwa wakitoa kauli mbaya kwa wagonjwa huku akiahidi kuwa kupitia chama anachoongoza changamoto hizo zitatatuliwa ndani ya muda mfupi.

Aidha Bw. Magesa alitumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali kwa kuongeza bajeti ya dawa nchini ambapo sasa dhana ya wauguzi kuwa ndio wezi wa dawa inaanza kufutika katika jamii.

“Hapo awali tulionekana sisi wauguzi ndio wezi wa dawa, tunaotumia vibaya dawa lakini ukweli ni kwamba dawa hazikuwepo, kitendo cha Serikali kuongeza bajeti ya dawa kimetusafisha sisi wauguzi” alisema Bw. Paul Magesa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Bw. Gustav Moyo amesema kuwa Kampeni ya Uuguzi Sasa imekuja wakati mwafaka kuja kutatua changamoto zilizopo muda mrefu ambazo zimekuwa zikikwamisha utendaji kazi wa wauguzi nchini.

Bw. Gustav amesema kuwa Uuguzi sasa ni kampeni ya kimataifa inayokusudia kuongeza hadhi na muonekano wa kada ya uuguzi nchini ambayo inalenga kuwawezesha wauguzi na wakunga kufikia na kumudu malengo ya afya ya karne ya 21 pamoja na changamoto zake.

CHANJO YA MLANGO WA KIZAZI HAIHUSIANI NA UZAZI WA MPANGO

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisisitiza jambo leo wakati akiongea na Waandishi wa Habari katika siku ya Saratani Duniani, iliyofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari Bunge jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mkurugenzi wa Ubora kutoka Wizara ya Afya Dkt. Mohammed Mohammed ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya.

Mkurugenzi wa Ubora ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mohammed Mohammed akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe leo katika  tamko la siku ya Saratani Duniani lililofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Bunge jijini Dodoma.

Waandishi wa Habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu  wakati akitoa tamko la siku ya Saratani Duniani, leo jijini Dodoma


 Waandishi wa Habari wakifuatilia tamko la Saratani lililosomwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo katika Ukumbi wa Idara ya habari Bungeni jijini Dodoma.

CHANJO YA MLANGO WA KIZAZI HAIHUSIANI NA UZAZI WA MPANGO.

Na WAMJW - DOM

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amewatoa hofu Wananchi kwa kusisitiza kuwa chanjo ya kuwakinga wasichana na Saratani ya Mlango wa kizazi haihusiani na uzazi wa mpango wala kumzuia msichana kuja kupata uja uzito baadae.

Ameyasema hayo leo wakati akiongea na Waandishi wa Habari katika siku ya Saratani Duniani, iliyofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari Bunge jijini Dodoma, huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni "NITAFANYA JITIHADA ZOTE KUPUNGUZA JANGA LA SARATANI DUNIANI".

Waziri Ummy amesema kuwa Chanjo ya Mlango wa kizazi ni salama na imethibitishwa na Shirima la Afya Duniani kwaajili yakuwakinga Wasichana dhidi ya maambulizi ya Saratani ya Mlango wa kizazi.

" Chanjo ya kuwakinga wasichana na saratani ya mlango wa kizazi haihusiani na uzazi wa mpango, ni chanjo ambayo imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani kwaajili yakuwakinga wasichana dhidi ya maambukizi ya Saratani ya mlango wa Kizazi" Alisema Waziri Ummy

Waziri Ummy amesema kuwa katika kila wagonjwa wa Saratani 100, takribani wagonjwa 31 ni wanawake wa Saratani ya Mlango wa kizazi, hivyo amewahasa wazazi na walezi nchini kuhakikisha wasichana wanaostahili kupata chanjo hii, wanaipata bila vikwazo vyovyote ili kutokomeza kabisa Saratani hii nchini.

"Katika kila wagonjwa wa Saratani 100, Wagonjwa takribani 31 ni wanawake wa Saratani hii ya Mlango wa kizazi, kwahiyo hatuna haja ya kuiogopa chanjo hii kwasababu ndio itayowakinga watoto wetu na maambukizi ya Saratani ya mlango wa kizazi" alisema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa  kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Tafiti za Saratani (IARC), zinaonyesha kwamba kwa Tanzania kunatokea mgonjwa 1 wa Saratani kwa kila watu 1000, hivyo Tanzania inakua na wagonjwa wapya wa Saratani 55,000 kwa mwaka na takribani wagonjwa 28,610 hufariki kwa mwaka, ambapo ni vifo asilimia 52 ya wagonjwa wapya. 

Aliendelea kusema kuwa Taarifa kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road zinaonesha kwamba kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa Saratani mwaka hadi mwaka, huku akisema kuwa Mwaka 2015  wagonjwa wapya 5,764, huku mwaka 2016  wagonjwa wapya 6,338, na mwaka 2017  wagonjwa wapya 7,091, pia mwaka 2018 wagonjwa wapya 7,649.

Kwa upande mwingine Waziri Ummy amedai kuwa Serikali imeanzisha huduma kwenye vituo 624 vilivyopo katika Halmashauri mbalimbali nchini ambapo jumla ya wanawake 375,522 walifanyiwa uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti mnamo mwaka 2017, ukilinganisha na wanawake 416,841 waliofanyiwa uchunguzi huo mwaka 2018. Kati ya hao, wanawake 16,147 waligundulika kuwa na mabadiliko ya awali mwaka 2017, na wanawake 18,341 mwaka 2018.