Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 7 Agosti 2019

HABARI PICHA : ZOEZI LA UTAYARI KUKABILIANA NA UGONJWA WA EBOLA KATIKA WILAYA YA BUHIGWE MKOANI KIGOMA.

Na Englibert Kayombo, Kigoma


Watoa huduma za afya kutoka Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma wakiwa wamembeba mgonjwa anayehisiwa kuwa na ugonjwa wa ebola tayari kumpatia huduma ya kwanza katika zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa huo usiingie nchini.

Kufuatia nchi ya jirani (DRC) kuendelea kukabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola tangu Agosti mwaka 2018. Serikali ya Tanzania imeendelea kuchukua tahadhari za ugonjwa huo kwa kupima utayari wa Watoa huduma za Afya kwa mikoa iliyomo hatarini kuathiriwa na ugonjwa huo.

Serikali kupitia uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na wadau wa maendeleo; WHO, FAO, USAID, HRH2030, Shirika la Msalaba Mwekundu (RED CROSS), na USAID Global Health Supply Chain Programu, inaendelea na zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa huo katika Wilaya za Mkoa wa Kigoma.

Zoezi hilo linalenga kuwaimarisha watumishi hao katika maeneo maalum ikiwemo ya uratibu, utambuzi na ufuatiliaji wa wagonjwa iwapo atagundulika, matibabu ya wagonjwa, uchukuaji na usafirishaji wa sampuli na kuthibitisha maabukizi pamoja kuimarisha mifumo ya utambuzi wa masuala ya Afya kwa kila abiria wanaopita kwenye mipaka ya mkoa wa Kigoma.


Mwezeshaji wa zoezi la upimaji wa utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Christopher Mnzava akifafanua umuhimu wa kuzingatia muda wakati wa maandalizi ya kumhudumia mgonjwa anaehisiwa kuwa na ugonwja wa ebola kwa watoa huduma za afya Katika Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma.

Watoa huduma za afya mara baada ya kumhudia mgonjwa wa ebola wakiwa wamebeba mifuko maalum kwa ajili ya utunzaji wa mavazi na vifaa vilivyovyotumika kuhumdumia mgonjwa kabla ya kuyateketeza.

Dkt. Refaya Ndyamuba kutoka Shirika la Afya Duniani akielekea kukagua kituo kitachokutumika kuhudumia wagonjwa wa ebola katika Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma katika zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa ebola usiingie nchini linaloendelea Mkoani Kigoma.

Bi. Consolata Felix Muuguzi kutoka Wizara ya Afya(aliyesimama kulia) akikagua watoa huduma za afya katika Kituo cha hudumia wagonjwa wa ebola katika Wilaya ya Buhigwe namna wanavyosafisha kitanda kilichotumika kumbeba mgonjwa wa ebola katika zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa ebola usiingie nchini linaloendelea kufanyika mkoani humo.

"Mahema ya kuhudumia wagonjwa wa ebola yanatakiwa kuwa na hewa safi muda wote" Dkt. Refaya Ndyamuba kutoka Shirika la Afya Duniani akifungua sehemu ya kuingiza hewa kwenye hema linalotumika kuhudumia wagonjwa wa ebola wakati wa zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa huo katika Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma. 

Mtoa huduma za afya katika Wilaya ya Buhigwe akinawa kwa maji safi yaliyochanganywa na kemikali ya "Chroline" mara baada ya kutoka kumhudumia mgonjwa wa ebola wakati wa zoezi la tayari wa kukabiliana na ugonjwa huo


0 on: "HABARI PICHA : ZOEZI LA UTAYARI KUKABILIANA NA UGONJWA WA EBOLA KATIKA WILAYA YA BUHIGWE MKOANI KIGOMA."