Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 19 Agosti 2019

CHMTs MWANZA ZAAGIZWA KUSIMAMIA MIONGOZO YA KUKINGA NA KUDHIBITI MAAMBUKIZO

Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa Huduma Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Chrisogone Justine German akitoa mafunzo kwa Watoa huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya Mkoa  wa Mwanza wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga dhidi ya magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata  taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC sstandard)

Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Joseph Hokororo akifafanua jambo mbele ya Watoa Huduma na Watumishi wa Sekta ya Afya Mkoa wa Mwanza wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga dhidi ya, kwa kufuata kanuni za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC standard ).

Afisa kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Alex Sanga akielekeza umuhimu wakufuata taratibu kwa mgonjwa wakati wa kumuudumia (IPC Standard) kwa Watoa Huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya Mkoa wa Mwanza.


Baadhi ya Watoa  huduma za Afya kutoka Halmashauri za Jiji la Mwanza wakifuatilia Mafunzo kwa makini ya jinsi yakujikinga dhidi ya maambukizi kwa kufuata kanuni na taratibu (IPC Standard) wakati wa kumuudumia mgonjwa.

Baadhi ya Watoa Huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya kutoka Halmashauri mbali mbali jijini Mwanza wakifuatilia kwa makini  Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga dhidi ya magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC Standard)

Picha ya pamoja ikiongozwa na Maafisa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiwa na Watoa huduma kutoka Halmashauri mbali mbali za Mwanza baada ya kumaliza mafunzo ya namna ya kujikinga na kudhibiti  magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa Mkoani hapo.



CHMTs MWANZA ZAAGIZWA KUSIMAMIA MIONGOZO YA KUKINGA NA KUDHIBITI MAAMBUKIZO

Na Rayson Mwaisemba WAMJW- MWANZA

Timu za uendeshaji huduma za Afya za Halmashauri (CHMTs) za Mkoa wa Mwanza zimeelekezwa kusimamia miongozo ya kukinga na kudhibiti maambukizi (Magonjwa) wakati wanatoa huduma za Afya kwa Wagonjwa.  

Hayo yamejiri wakati wa Semina ya mafunzo ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti  magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa, iliyofanyika Jijini Mwanza ikiwa ni moja kati ya mikoa iliyo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.

Kwa upande mwingine mafunzo hayo yametumika kama njia ya kusambaza muongozo mpya wa namna ya kujikinga na kudhibiti  maambukizo (IPC Guidline), ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ikiwa ni njia ya kuboresha huduma za Afya nchini. 

Katika mafunzo hayo imedaiwa kuwa Tanzania ipo kwenye hatari ya kupata wagonjwa wa Ebola kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu na ukaribu na Nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo ambako Mlipuko unaendelea.

Inakadiriwa kuwa watu Bilioni 2.5 Duniani wapo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola, huku kati yao 60% ikiwa ni watu kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara, huku nchi za Sudan, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zikiripoti kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo ambao ulisnza tangu 1976.

Kulingana na Taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) inakadiriwa kuwa Wagonjwa 1790 wapoteza maisha tokea mlipuko huo ulipojitokeza Agosti 2018 Wagonjwa 2577 wamethibitika kuwa na Ugonjwa wa Ebola, huku Wagonjwa 1790 wakipoteza maisha tokea mlipuko huo ulipojitokeza Agosti 2018, huku Wataalamu wa Afya 131 walipata maambukizi, ambapo 41 kati yao wamepoteza maisha.

Hata hivyo, Serikali ya Tanzania tayari imekwisha kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha utayari wa kukabiliana na tishio la Ugonjwa huo ili kuhakikisha hauingii nchini, ikiwemo kuelimisha jamii njia za kujikinga na Ugonjwa ili kuzuia usiingie nchini, na kutoa Elimu kwa Watoa huduma za Afya juu ya kumuhudumia mtu mwenye dalili za Ebola endapo atatokea.

Katika mafunzo hayo, Watoa huduma wameaswa kuzingatia taratibu za kujikinga na kudhibiti maambukizo (IPC Standard precautions) kwa kadri Miongozo inavyoelekeza wakati wote wa kutoa huduma kwa Wagonjwa, jambo litalosaidia kuwaepusha kupata maambukizi, au kumsaidia mgonjwa kupata maambukizi mapya wakati wa matibabu.

Akitoa mafunzo hayo, Afisa kutoka Kitengo cha Uhakiki Ubora Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Joseph Hokororo amesema kuwa Watoa Huduma za Afya wapo katika hatari kubwa za kupata maambukizi ya ugonjwa huu, endapo hawatofuata miongozo na taratibu za utoaji huduma kwa kadri ya muongozo huu

“Mara kwa mara ni muhimu kuwa na tahadhari wakati unahudumia Wagonjwa, hususan kunawa mikono kabla na baada ya kutoa huduma kwa wagonjwa na wasio wagonjwa kwani Watoa huduma mpo kwenye hatari kubwa sana yakupata maambukizo” alisema Dkt. Joseph Hokororo.

Ameendelea kusema kuwa, Shirika la Afya Duniani (WHO) inakusudia kuzuia Ugonjwa wa Ebola kwa kuimarisha huduma za uchunguzi na kusaidia nchi zilizo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.

Pia alisisitiza kuwa Dunia imekumbwa na tatizo la Usugu wa vimelea vya magonjwa ambukizi dhidi ya dawa (antimicrobial resistance), hivyo amesisitiza juu ya umuhimu mkubwa wa kufuata taratibu za kutoa huduma (IPC Standard) ili kusaidia kutokomeza vimelea hivyo.   

Akitoa mafunzo kwa Watoa Huduma za Afya, juu ya namna ya kukinga maambukizi wakati wa kujifungua, Afisa kutoka Kitengo cha Uhakiki Ubora Wizara ya Afya Dkt. Chrisogone German amesema kuwa ni muhimu kwa Watoa huduma kufuata viwango vya kukinga na kudhibiti maambukizo (IPC Standard) ili kudhibiti ya ugonjwa wakati wa kutoa huduma ikiwemo kuhakikisha kunawa mikono kabla ya kufanya kazi za kuhudumia wagonjwa.

Aliendelea kusisitiza kuwa, si jambo zuri kwa Watoa huduma za Afya, kufanya mambo kwa mazoea, hali inayopelekea kufanya kazi kwa mazoea na kujikuta kunasambaa maambukizi kutoka kwa mtu anaepokea huduma za Afya au kinyume chake 

Mwisho.

0 on: "CHMTs MWANZA ZAAGIZWA KUSIMAMIA MIONGOZO YA KUKINGA NA KUDHIBITI MAAMBUKIZO"