Dkt. Askwar Hilonga akiwakaribisha Viongozi wa Wizara wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kinga Dkt. Leonard Subi na wengineo wakati walipotembelea Chuo Kikuu cha Nelson Mandela Jijini Arusha. |
Picha ya pamoja katika ofisi ya Kaimu Mkuu wa chuo cha Nelsona Mandela Jijini Arusha. |
Mbunifu wa Teknolojia ya Nano Filter Dkt. Askwar Hilonga akiwaonesha viongozi sehemu ambayo ubunifu huo ulipoanzia katika chuo cha Nelson Mandela. |
Mifupa ya wanyama inayotumika katika Teknolojia ya Nano Filter kuchuja na kutibu maji kwa ajili ya matumizi. |
Mkurugenzi wa Kinga Dkt. Leonard Subi akiangalia chengachenga za mifupa inayotumika na teknolojia ya Nano Filter katika kuchuja na kutibu maji ya kunywa. |
Dkt. Hilonga akitoa maelezo kwa viongozi wa Wizara wakati walipotembelea maonesho ya Sabasaba kwenye banda la Nano Filter. |
Teknolojia ya Nano Filter iliyofungwa katika moja ya Shule Jijini Arusha. |
Baadhi ya Wananchi waliofika katika ofisi hiyo kwa ajili ya kujaziwa maji. |
Picha ya pamoja ya viongozi wa Wizara wakiwa na Baadhi ya Wafanyakazi wa Nano Filter nje ya ofisi zao. |
Teknolojia ya Nano Filter ikiwa imefungwa katika Maonesho ya Nanenane Jijini Arusha. |
Viongozi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kinga Dkt. Leonard Subi wamemtembelea
mbunifu wa teknolojia ya kusafisha maji ambaye pia ni mhadhiri wa Chuo Kikuu
cha Nelson Mandela kilichoko Arusha Dkt. Askwar Hilonga.
Katika ziara hiyo Dkt. Hilonga amewaonesha viongozi hao Teknolojia
iitwayo Nano Filter yenye uwezo wa kusafisha maji, kuondoa bacteria na virusi, huondoa
fluoride na madini yote ambayo hayatakiwi kwa binadamu na kuyafanya maji kuwa safi
na salama kwa watumiaji na kwa gharama nafuu zaidi.
Dkt. Hilonga ana tuzo 17 kutoka taasisi na mashirika
mbalimbali kutokana na ubunifu huo huku tuzo yake kubwa ikiwa ni ile aliyoipata
kwenye kikao cha dunia cha masuala ya afya (World Health Assembly)
kilichofanyika Jijini Geneva, Uswisi mwezi Mei mwaka huu.
0 on: "TEKNOLOJIA YA NANO FILTER YAWAVUTIA VIONGOZI WA WIZARA JIJINI ARUSHA"