Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Ijumaa, 30 Agosti 2019

HOSPITALI YA MLOGANZILA YAZIDI KUIMARISHA HUDUMA.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Tawi la Mloganzila Dkt. Julieth Magandi (aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya utendaji wa Hospitali hiyo kwa mwaka 2018/19 kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Huduma na Maendeleo ya Jamii jana Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba (aliyesimama) akisema jambo kwneye kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jana katika kumbi za Bunge Jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisema jambo kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge, Huduma na Maendeleo ya jamii  kilichofanyika jana katika kumbi za Bunge Jijini Dodoma.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Huduma na Maendeleo ya Jamii wakiwa kwenye kikao kujadili taarifa ya utendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Tawi la Mloganzila jana Jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Huduma na Maendeleo ya Jamii wakiwa kwenye kikao kujadili taarifa ya utendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Tawi la Mloganzila jana Jijini Dodoma.


Wataalam kutoka Wizara ya Afya na taasisi zake wakisikiza uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Tawi la Mloganzila kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Huduma na Maendeleo ya Jamii jana Jijini Dodoma.

Na Englibert Kayombo, WAMJW - Dodoma

Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Tawi la Mloganzila jana umewasilisha taarifa ya utendaji kwa mwaka 2018/19 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge Huduma na Maendeleo ya Jamii.

Akiwasilisha taarifa hiyo Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt. Julieth Magandi amesema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja tangu hospitali hiyo kuwa chini ya usimamizi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)huduma za matibabu katika hospitali hiyo zimeimarika huku idadi ya wagonjwa waliopata huduma katika hospitali hiyo ikiongezeka.

“Mara baada ya kukabidhiwa Hospitali ya Mloganzila kwa Muhimbili juhudi mbalimbali zimefanyika kuhakikisha kwamba huduma nzuri inatolewa, kuongeza idadi wagonjwa pamoja na kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali nyinginezo ikiwemo Muhimbili.

Dkt. Magandi alitaja juhudi hizo kuwa ni pamoja na kutumia wataalam wa Muhimbili kutoa huduma Mloganzila, kuongeza upatikanaji wa damu, dawa na kutoa motisha kwa wafanyakazi ili kuwaongezea hamasa ya kazi pamoja na kukekea lugha mbaya pamoja na rushwa.

“Hatua zilizochukuliwa zimepelekea kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa ambao wengi wao wameonyesha kuridhika na huduma tunatozitoa” alisema Dkt. Magandi.

Kwa upande wake Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alisema kuwa Hospitali ya Mloganzila itaendelea kuwa chini ya Bodi ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. “Msimamo wetu ni kwamba hizi ni Hospitali mbili tofauti, lakini chini ya menejimenti moja ya Bodi ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili” alisema Waziri Ummy.

Pamoja na kuanzishwa kwa Hospitali ya Mloganzila, lakini uendeshaji wa hospitali hapo awali haukuwa mzuri” alisema Waziri Ummy na kuendelea “Hospitali ile ina vitanda 608 lakini wagonjwa waliokuwa nao ni chini ya asilimia 30 kwahiyo Hospitali hiyo ilikuwa haiendeshwi kwa ufanisi.

Katika kipindi cha mwaka 2018/19 Hospitali ya Mloganzila imeweza kuwahudumia wagonjwa 85,532 wa nje, wagonjwa 8,480 wa ndani na 2,781 ambao walifanyiwa upasuaji.

MWISHO

0 on: "HOSPITALI YA MLOGANZILA YAZIDI KUIMARISHA HUDUMA."