Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Prof. Mabula Mchembe akifungua Mkutano wa Maafisa Afya mazingira uliofanyika Jijini Dodoma.
Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, ambae pia ni Mkurugenzi wa huduma za Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi akiwasilisha maelekezo ya Mganga Mkuu wa Serikali kwa Maafisa Afya mazingira katika ufunguzi wa Mkutano wa tathmini wa Maafisa Afya mazingira uliofanyika Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe TAMISEMI Dkt. Paul Chawote akitoa neno kwa Maafisa Afya mazingira (hawapo kwenye picha) walio hudhuria Mkutano wao wa tathmini, uliofanyika Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Maafisa afya mazingira nchini Bw. Evans Simkoko akitoa salam za Maafisa Afya mazingira kwa Mgeni rasmi ambae ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya (hayupo kwenye picha) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa tathmini wa Afya mazingira uliofanyika Jijini Dodoma.
Maafisa Afya kutoka maeneo ya mipaka wakifuatilia kwa makini neno kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya (hayupo kwenye picha) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa tathmini wa Afya mazingira uliofanyika Jijini Dodoma.
Maafisa Afya mazingira wakifuatilia kwa makini neno kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya (hayupo kwenye picha) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa tathmini wa Afya mazingira uliofanyika Jijini Dodoma.
TIMIZENI WAJIBU WENU KWA WELEDI NA MAADILI.
Na Rayson Mwaisemba, WAMJW- DOM.
KATIBU Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara kuu ya Afya Prof. Mabula Mchembe amewataka Maafisa Afya ngazi zote kufanya kazi zao kwa weledi na kufuata maadili wakati watimizapo majukumu yao katika jamii.
Prof. Mchembe ameyasema hayo, wakati akifungua Mkutano wa Maafisa Afya mazingira wenye kauli mbiu ya "Zingatia mahitaji ya Jinsia kwa usafi wa mazingira endelevu " uliofanyika Jijini Dodoma.
"Tusimamie maadili sana, usitende kitu kwa kufikiria kwamba unamfanyia fulani, natambua changamoto zipo katika baadhi ya sehemu, lakini tunahitaji kutimiza wajibu wetu kwa maadili na uwaminifu wa hali ya juu" alisema Prof. Mchembe.
Pia, Prof. Mchembe amewataka Maafisa Afya mazingira kusimamia usafi katika maeneo ya huduma za vyoo katika jamii, hususan katika ofisi na vituo vya daladala ambavyo huudumia Jamii kwa kiasi kikubwa ili kuikinga Jamii dhidi ya magonjwa ya milipuko.
Aidha, Prof. Mchembe amewaagiza Maafisa Afya mazingira nchini kusimamia usafi na ubora wa vyakula katika maeneo yote yanayotoa huduma za vyakula, yakiwemo maeneo ya migahawa na hoteli ili kuikinga jamii na magonjwa ya tumbo na kuhara.
Mbali na hayo Prof. Mchembe ametoa wito kwa Maafisa afya mazingira kujiepusha na vitendo vya Rushwa wakati wa wakitimiza majukumu yao na kuhakikisha usafi wa mazingira unaendelea kufuatwa katika ngazi zote za Jamii.
"Tuachane na Rushwa, inawezekana baadhi ya sehemu unafika pale, unapewa 10,000 au unapewa bia mbili au tatu unaondoka zako, kitu ambacho hakina maana, sasa kama wewe ni Mtaalamu wa Afya simama kwenye maadili yako" alisema Prof. Mchembe.
Hata hivyo, Prof. Mchembe amewaagiza Maafisa afya mazingira nchini, kusimamia udhibiti wa takataka zinazotokana na utoaji wa huduma za afya ili kuendelea kuikinga jamii dhidi ya maambukizi yatokanayo na taka hizo.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, ambae pia ni Mkurugenzi wa huduma za Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi amewaagiza Waganga wakuu wa mikoa kutoa elimu mara kwa mara kwa watendaji wao juu ya maadili badala ya kusubiri kuchukua hatua baada ya kosa kujitokeza.
"Kutoa elimu mara kwa mara kuhusu maadili, badala ya kusubiri kuchukua hatua kwa Maafisa Afya au wana taaluma wenu, wanapokiuka au kufanya makosa mbali mbali " alisema Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Subi.
Aliendelea kusema kuwa, baadhi ya maeneo hususan mijini bado kuna hali ya usafi wa mazingira usioridhisha, na kuelekeza kuanza kampeni ya usafi wa mazingira ya muda wa miezi miwili, huku akiwataka kuanza oparesheni hiyo kwa kuzingatia Sheria na kanuni za afya ya mwaka 2009.
Hata hivyo, Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali amewaagiza Maafisa Afya mazingira, kukagua suala la usafi wa mazingira kwenye shule, mabweni, maofisi na maeneo yote yenye mikusanyiko ili kuhakikisha usafi wa mazingira unapewa mkazo ili kuikinga jamii dhidi ya maambukizi ya magonjwa ya mlipuko.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Maafisa afya mazingira nchini Bw. Evans Simkoko ameiomba Serikali kuipa kipaumbele kada ya Maafisa Afya mazingira kwenye ajira mpya, ili kuongeza ufanisi katika utoaji huduma kwa wananchi, kisha kuikinga Jamii dhidi ya maambukizi ya ugonjwa ya milipuko.
Mwisho.

PolyTrack is a low-poly racing game playable directly in your browser, no download required. The gameplay is fast-paced, with creative tracks, perfect for short bursts of entertainment or practicing reflexes. Anyone who enjoyed TrackMania will find it familiar.
JibuFutaIt's encouraging to see health leaders emphasizing integrity and accountability in public service. Promoting ethical practices and continuous education can strengthen trust in the healthcare system. After reading community news like this, I like taking a short break with Crossy Road , a classic arcade game that's perfect for relaxing before getting back to the day.
JibuFutaEver find yourself needing a quick mental break, a game that’s easy to pick up but surprisingly engaging? Look no further than Block Blast. This unassuming puzzle game, available at Block Blast , offers a delightful blend of strategy and satisfaction, perfect for a few spare minutes or a longer, relaxing session. Forget complex storylines or high-stakes competition; Block Blast is all about the simple joy of clearing blocks and watching your score climb.
JibuFutaBasketball Stars helps players develop critical abilities like hand-eye coordination, reaction time, and strategic thinking in addition to being fun. Players must assess their opponent's motions, anticipate their next move, and react fast in every battle. To win, it becomes crucial to know when to attack, defend, or try challenging shots.
JibuFutabasketball stars