Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Alhamisi, 19 Julai 2018

WAZIRI UMMY ATEMBELEA HOSPITAL YA RUFAA MKOA TABORA KITETE

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu Kulia akipata maelezo juu ya Chumba cha Upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Kitete mkoani Tabora kutoka kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora  Dkt. Gunin Komba kushoto wakati wa ziara yake mkoani humo.


Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akimsalmia mama aliyejifungua mapacha Bi. Debora Erasto (29) mkazi wa Ullyankulu mkoani Tabora wakati wa ziara yake mkoani humo.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akimsalmia mama aliyejifungua mapacha Bi. Debora Erasto (29) mkazi wa Ullyankulu mkoani Tabora wakati wa ziara yake mkoani humo.



Ijumaa, 13 Julai 2018

MARUFUKU KUAJIRI WATOA HUDUMA NGAZI YA JAMII NJE YA ENEO HUSIKA.

- Hakuna maoni

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akiongea na Wananchi wa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu wakati wa ufunguzi wa mradi wa Tuwatumie ambao unawaajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika vijiji vyote vya halmashauri hiyo chini ya ufadhili wa AMREF

Wadau mbalimbali wa sekta ya afya walifuatilia hotuba ya mgeni rasmi(hayupo pichani) aliyekaa kushoto ni Niall Morris Mkuu wa Arish Aid,Dar.Aisa Muya -Kaimu Mkurugenzi Mkazi Amref Tanzania(katikati) na kulia ni Dkt.Helen Senkoro Mkurugenzi wa Benjamin Mkapa Foundation

Wananchi waliojitokeza kushuhudia ufunguzi wa mradi huo ambapo watoa huduma hao watakua kiungo kati ya wananchi na vituo vya kutolea huduma.

Waziri Ummy Mwalimu akifungua mradi huo


MARUFUKU KUAJIRI WATOA HUDUMA NGAZI YA JAMII NJE YA ENEO HUSIKA. 

NA WAMJW-SIMIYU. 

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imepiga marufuku kuajiri watoa huduma wa afya ngazi za jamii kutoka nje ya Halmashauri husika. 

Katazo hilo limetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa mradi wa TUWATUMIE uliofanyika mkoani Simiyu wilaya ya Itilima. 

"Nataka kuwaambia viongozi wa Mkoa na Wilaya nchi nzima pamoja na taasisi zisizo za kiserikali ni marufuku kuajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii (CHW) kutoka nje ya  makazi yao ili kusiwe na  kutotofautiana kimazingira,kwani wenyeji wanajua tamaduni na mila za wakazi wanapotoka" alisema Waziri Ummy. 

Waziri Ummy amesema kuwa watoa huduma ngazi ya jamii wanatakiwa kuwa kipaumbele katika kukinga kuliko kutoa tiba ili kupunguza idadi ya wagonjwa na kuokoa fedha. 

"Nataka kuwaambia wahudumu wa afya ngazi ya jamii wanatakiwa kuweka kipaumbele kinga kuliko tiba kwani mimi ni Waziri wa Afya na sio Waziri wa wagonjwa,siwezi kusubiri watu wale ,nitawatumia CHW kuwakinga ama kuwazuia wanaoumwa kupata matibabu" alisema Waziri Ummy. 

Alisema nchi ipo kwenye mikakati ya kufikia malengo endelevu ya millennia ya kumfikia kila mtanzania kwa wakati na popote,hivyo kwa kuanza CHW wanaanza eneo la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Amref Tanzania Dkt. Aisa Muya amesema kuwa asilimia 50 ya miradi yao wanatumia watoa huduma za afya ngazi ya jamii . 

Aidha, Dkt. Muya amesema kuwa wametoa mafunzo kwa watoa huduma  2,265 na mradi huo utawaajiri watoa huduma 2,015 mbapo Wilaya ya Itilima watakuwa 102 na Misungwi 113 ambao wataenda kwenye vijiji vyote vya wilaya hizo. 

Dkt. Muya amesema kuwa matarajio ya mradi huo ni kuwatumia watoa huduma hao kama kiungo kati ya jamii na vituo vya kutolea huduma za afya. 

TAARIFA KWA UMMA

- Hakuna maoni



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO


KUITWA  KAZINI

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kuwataarifu wote walioomba nafasi mbalimbali za Ajira za Kada ya Afya tarehe  11 Mei  hadi  26  Mei, 2018  kuwa  walioorodheshwa  katika tangazo hili wamechaguliwa na kupangiwa vituo vya kazi kama jedwali linavyoonyesha kwenye Tovuti ya Wizara ya  Afya  www.moh.go.tz.

Waombaji  waliochaguliwa wanatakiwa kuzingatia kwa ukamilifu maelekekezo yafuatayo:

1).   Kuripoti  Ofisi  za Wizara  ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dodoma katika  muda  wa  siku  kumi  na  nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili, kwa ajili ya kukamilisha taratibu za Ajira Serikalini.  Ambao hawataripoti ndani ya siku kumi na nne (14) nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine wenye sifa.  Aidha, wakati wa kuripoti kila aliyechaguliwa atapaswa kuwasilisha vyeti halisi (Original Certificates) ambavyo nakala zake zilitumiwa wakati wa kuomba ajira zao, ikiwa pamoja na:-

a)      Vyeti halisi vya Elimu ya Sekondari, Vyeti vya Taaluma, Usajili wa Baraza/Bodi ya Kitaaluma na cheti cha kuzaliwa.

b)     Nakala ya picha mbili ndogo (passport size). Picha ziwe na muonekano kamili wa sura na ziwe zimepigwa si zaidi ya miezi mitatu iliyopita.

2)      Waombaji  wote  ambao  majina  yao  hayakuonekana  katika  tangazo  hili  watambue  
kuwa hawakupata nafasi hiyo, hivyo wanashauriwa  wasisite  kuomba  mara  nafasi  nyingine za  kazi zitakapotangazwa.

3)  Waombaji waliopangiwa  Kada ya Uhudumu wa Afya majina yao yatatangazwa baadae.


Imetolewana:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Afya
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
13 Julai, 2018

Alhamisi, 12 Julai 2018

SERIKALI KUFUTA TOZO YA USAJILI,KUHUWISHA NA KUSHIKILIA USAJILI KWA WAWEKEZAJI WA NDANI.

- Hakuna maoni




Waziri wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akikagua shughuli za ujenzi wa jengo la wodi ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou toure wakati alipotembelea kukagua shughuli za ujenzi wa jengo hilo jijini Mwanza.

 Waziri wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kushoto wakati alipotembelea kukagua shughuli za ujenzi wa jengo la Mamlaka hiyo jijini Mwanza. Kulia ni Mkurugenzi wa Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya afya Dkt. Mohammed Mohammed.

 Waziri wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akipata maelezo juu ya sukari zinazopimwa ubora wake  kutoka kwa Mkuu wa Maabara wa TFDA  Kanda ya Ziwa Bw. Salum Kindoli wakati alipotembelea kukagua shughuli za ujenzi wa jengo la Mamlaka hiyo jijini Mwanza.

Waziri wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia  akipata baadhi ya maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya afya Dkt. Mohammed Mohammed kushoto wakati alipotembelea kukagua shughuli za ujenzi wa jengo la Mamlaka hiyo jijini Mwanza.

Baadhi ya mafundi wakiendelea na shughuli za ujenzi wa wa jengo la wodi    ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou toure jijini Mwanza.


SERIKALI KUFUTA TOZO YA USAJILI,KUHUWISHA NA KUSHIKILIA USAJILI KWA WAWEKEZAJI WA NDANI.
NA WAMJW-MWANZA
SERIKALI kupitia wizara ya afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imefuta tozo ya usajili , kuhuwisha pamoja na kushikilia usajili wa bidhaa zao kwa wawekezaji wa ndani kupitia Mamlaka ya chakula na Dawa TFDA .
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea kuangalia ujenzi wa jengo la TFDA ambalo linajengwsa Jijini Mwanza ili kusogeza huduma kwa wananchi wa mkoa huo.
“Ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kukuza nchi kupitia uchumi wa viwanda hivyo TFDA msiwe kikwazo kwa wawekezaji hao hivyo kuanzia leo nafuta tozo za kusajili bidhaa,kuhuwisha bidhaa na tozo ya kushikilia usajili wa bidhaa”, alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa kuendana na juhudi hizo pia Serikali  imefuta tozo ya udhibiti  ya thamani ya 0.25 za dawa,vifaa na vifaa tiba zinazoingizwa kwenye hospitali za Umma kutoka kwa wafadhili.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa TFDA ina wajibu wa kusimamia Tanzania isiwe jalala la bidhaa zisizo na ubora kwa watanzania hivyo wanatakiwa kuweka afya ya wananchi mbele kuliko manufaa binafsi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bi. Agness Kijo amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo ukikamilika utasaidia kuhudumia huduma za kimaabara kwa bidhaa zinazoingia nchini kwani itakuwa sio lazima tena kwenda kupima bidhaa hizo jijini Dar es salaam.
“Maabara hizi zikikamilika zitasaidia kufanya vipimo na udhibiti wa bidhaa katika mipaka mingi ya kanda ya ziwa ikiwemo Silali,Lusumo na Mtukula ili kuweka usalama wa bidhaa zinazoingia na kutoka nje ya nchi kwa usalama wa wananchi.
Sambamba na hilo Waziri Ummy alipata nafasi ya kutembelea kukagua ujenzi wa jengo la wodi ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou toure na kuhakikisha ujenzi unakamilisha ili kuokoa vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na uzazi.
“Kama watu wa mwanza wanaridhishwa na huduma zinazotolewa katika hospitali hii basi ni lazima huduma za afya ziboreshwe ikiwemo afya ya mama na mtoto hivyo ninaleta mashine ya CT Scan kwa ajili ya kuboresha matibabu hapa” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy aliwataka watendaji wa Hospitali  kutoa taarifa za utendaji kwa Waziri wa Afya na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo pamoja na kusimamiwa na Wakuu wa Mikoa yao ili kuimarisha huduma za afya nchini.

Jumatatu, 9 Julai 2018

WILAYA 58 ZAFANIKIWA KUDHIBITI UGONJWA WA TRAKOMA

- Hakuna maoni
Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi akifungua Mkutano wa mafunzo wa nchi 21 ambazo zina maambukizi ya Ugonjwa wa Trakoma (Vikope) uliofanyika katika jiji la Arusha.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt. Timothy Wonanji  akiongea na Wadau  kutoka nchi mbali mbali wa magonjwa ya Trakoma(Vikope) katika kikao kilichofanyika jijini Arusha huku lengo likiwa kuhimarisha mkakati wa namna ya kugundua ugonjwa wa Trakoma na jinsi yakuweka takwimu sahihi katika nchi hizo 21.

Mratibu wa Taifa wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele chini ya Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazeee na watoto  Dkt . Upendo Mwingila akionga kwa kifupi juu ya hali ya ugonjwa wa Trakoma nchini mbele ya Wadau wa ugonjwa wa Trakoma kutoka nchi 21.

Picha ya Wadau zaidi ya 100 kutoka nchi 21 ambao walihudhuria kikao chenye lengo la kuhimarisha mkakati wa namna ya kugundua ugonjwa wa Trakoma na jinsi yakuweka takwimu sahihi kilichofanyika jijini Arusha

 Kundi namba 1 la Wataalamu likiongozwa na madaktari (Graders) wakijadili kuhusu ugonjwa wa Trakoma katika nchi zao.

Kundi namba 2 ni Wataalamu wa masuala ya Takwimu wakijadil namna ya uingizaji wa takwimu kwa usahihi.
Picha ya Pamoja ya Wadau  kutoka nchi 21 wa ugonjwa ya Trakoma(Vikope) walioshiriki katika kikao kilichofanyika jijini Arusha huku lengo likiwa kuhimarisha mkakati wa namna ya kugundua ugonjwa wa Trakoma na jinsi yakuweka takwimu sahihi katika nchi hizo 21.

WILAYA 58 ZAFANIKIWA KUDHIBITI UGONJWA WA TRAKOMA

Na WAMJW - ARUSHA

Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi amethibitisha kuwa halmashauri 58 nchini zimefanikiwa kutibu ugonjwa wa trakoma kutokana na jitihada mbali mbali zilizofanywa na Serikali kwa ushirikiano na Wadau.

Alisema hayo wakati akifungua Mkutano wa Uzinduzi wa Mafunzo kwa wawakilishi wa nchi 21 ambazo zinamaambukizi ya ugonjwa wa Trakoma/ vikope huku lengo likiwa ni kuwajengea wataalamu hao uwezo ili waweze kupambana dhidi ya ugonjwa huu. 
"Mwanzoni tulikuwa na Wilaya takribani 75 ambazo zilikuwa na ugonjwa huu,  jitihada zimeweza kufanyika  tangu 2014 hadi leo Hii  Karibu Wilaya 58 zimeweza kushinda dhidi ya ugonjwa huu, tumebakiza Wilaya 13 na kama Serikali tutaendelea kutoa dawa na Elimu kwa umma ili waweze kujikinga  dhidi ugonjwa huu ", Alisema Dkt. Subi

Dkt Subi aliendelea kusema kuwa sifa mojawapo ya kudhibiti ugonjwa huu ni kupitia mafunzo yanayomjengea uwezo mtaalamu kuweza kujua namna ya kujua ugonjwa, na kuweza kudhibiti dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huu  

Kwa upande mwingine Dkt. Subi ametoa wito kwa wananchi wote hususani waliokatika hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa huu wa trakoma kuwa Safi wakati wote kwa kunawa uso, kujenga vyoo na kusafisha mazingira yanayotuzunguka mara kwa mara. 
"ugonjwa huu unatokana na uchafu, kama huogi, kama hunawi uso, unaweza sababisha macho yako yakahathirika, ni vizuri kutumia Fursa ya maji vizuri kwa kufanya usafi vizuri mda wote" alisema Dkt. Subi 

Pia Dkt Subi aliwahasa wananchi kutumia dawa Kwani ni  salama na nzuri ndiomaana zimeponya watu katika halmashauri 58 kufanikiwa kupambana dhidi ya ugonjwa huu wa trakoma. 

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt Thimothy Wonanji alisema kuwa bado Wilaya tatu jijini Arusha zinaendelea kusumbuliwa na tatizo hili lá trakoma, Wilaya hizo ni Longido,  ngorongoro pamoja na Monduli na kusema kuwa tatizo kubwa limeonekana kuwa ni changamoto ya upatikaaji wa maji katika maeneo hayo.

Aliendelea kusema kuwa Serikali katika ngazi ya Mkoa kuna uratibu wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ambao kwa kushirikiana na wadau wamekuwa na mradi wa kwenda kijijini na kupita nyumba kwa nyumba kuwapima wakazi wa maeneo hayo na kuwaanzishia dawa (zitromas) kwa wanaogundulika kuwa na ugonjwa huu. 

Nae Mratibu wa Taifa wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt Upendo Mwingila alisema kuwa idadi ya wagonjwa wamepungua kutoka 160 Mpaka mwaka huu wagonjwa elfu 25,000 hii inatoka na juhudi za Wizara ya Áfya kupitia mpango wa taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele na Wadau mbali mbali katika kupambana dhidi ya ugonjwa huu wa trakoma jambo lililosaidia kufanikisha kufanya upasuaji wa vikope takribani 12,000 kwa mwaka.

Jumamosi, 7 Julai 2018

DMO SIHA ASEMA KUWA UTOAJI WA DAWA ZA MINYOO MASHULENI YAFIKIA 97% KATIKA WILAYA YA SIHA.

- Hakuna maoni
Mtabibu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika Mpango wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Bw.  Wilfred Mandala akiwaelekeza Wawakilishi kutoka Taasisi ya Bill and Melinda Gate na The End Fund namna ya  kusafisha mguu wa Bw. Juma ambae ni mwasilika  wa ugonjwa wa Matende

Afisa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika Mpango wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Hope Rusibamayila akishirikiana na wanafunzi kutoka Shule ya Msingi ya Kilari iliyo katika Wilaya ya Siha katika Mkoa wa Kilimanjaro kutoa maelekezo kwa wawakilishi kutoka Taasisi ya Bill and Melinda Gate na The End Fund namna ya Kibuyu Chirizi kikifanya kazi ya kuosha mikono kwa sabuni baada yakutoka Chooni.

Wawakilishi kutoka Taasisi ya Bill and Melinda Gate na The End Fund wakiendelea na ziara yao yakukagua baadhi ya miundombinu waliyoisaidia katika Shule ya Msingi ya Kilari iliyo katika Wilaya ya Siha katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Wawakilishi kutoka Taasisi ya Bill and Melinda Gate na The End Fund wakigawa kalamu za kuandikia kwa wanafunzi wanafunzi kutoka Shule ya Msingi ya Kilari iliyo katika Wilaya ya Siha katika Mkoa wa Kilimanjaro 

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Siha Dkt. Endrew Method akiongea na Wanafunzi pamoja na Wageni kutoka Taasisi ya Bill and Melinda Gate na The End Fund wakati walipotembelea katika Shule ya Msingi ya Kilari iliyopo katika Wilaya ya Siha katika Mkoa wa Kilimanjaro

 Afisa Elimu Wilaya ya Siha Rose Sandi akifanya utambulisho kwa Wanafunzi pamoja na Wageni waliofika katika Shule ya Msingi ya Kilari iliyo katika Wilaya ya Siha katika Mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni kutembelea na kujionea maendeleo ya mchango waliotoa katika shule hiyo.

 Afisa Mipango wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kutoka Wizara ya Afya  Bw. Oscar Kaitaba akitoa salam kutoka Wizara ya Afya mbele ya Wanafunzi pamoja na Wageni kutoka Taasisi ya Bill and Melinda Gate na The End Fund

Mwanafunzi Kutoka Shule ya Msingi ya Kilari Vaileth Wilfred akimkabidhi ujumbe Afisa Elimu Wilaya ya Siha Rose Sandi baada ya kumaliza Shairi lao, kulia kwake ni  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Siha Dkt. Endrew Method na wa mwisho ni Afisa Mipango wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kutoka Wizara ya Afya Bw. Oscar Kaitaba.

Picha yapamoja ya Watumishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Wageni kutoka Taasisi ya Bill and Melinda Gate na The End Fund baada ya kumaliza shughuli ya kutembelea na kukagua miundombinu katika Shule ya Msingi Kilari wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro.

Picha ya Pamoja ya Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Kilari wakionesha kalamu zao juu kuonesha furaha zao baada ya kupokea kutoka katika Taasisi ya Bill and Melinda Gate na The End Fund


DMO SIHA ASEMA KUWA UTOAJI WA DAWA ZA MINYOO MASHULENI YAFIKIA 97% KATIKA WILAYA YA SIHA.

Na WAMJW - SIHA KILMANJARO

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Endrew Method amesema kuwa Wilaya ya Siha imepiga hatua kubwa katika kukabiliana na changamoto ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, huku akidai kuwa  97% ya watoto tayari wameshapata dawa hizo za minyoo.
Ameyasema hayo alipowapokea wageni kutoka Bill and Melinda Gate na THE END FUND waliokuja kuangalia utekelezaji wa miradi waliyoifadhili na kufuatilia namna ya wanufaika wanavyofaidika na miradi hiyo katika Wilaya ya Siha.
“Ukiangalia utoaji wa Dawa za minyoo mashuleni kwa Wilaya tulifikia 97% jambo ambalo linasaidia watoto kutopata changamoto za ugonjwa wa minyoo, hata hivyo kwa wagonjwa wa  n je tu matatizo ya minyoo yanafikia hadi nafasi ya tatu hivyo kuna umuhimu mkubwa wa wa kuufanya uwe mkakati endelevu” Alisema Dkt. Method
Dkt. Method aliendelea kusema kuwa Taasisi ya Bill and Melinda Gate na THE END FUND wamekuja kuangalia ni jinsi gani miradi hiyo imekuwa ikitekelezwa na namna ambavyo matumizi ya fedha wanazotoa yamekuwa yakiwanufaisha wahusika.
 “Wamekuja kuangalia, ni jinsi gani yale mambo waliyokuwa wakititusaidia tunatekeleza, na miongoni mwa mambo hayo ni  unyweshaji wa watoto dawa za minyoo kwaajili ya kukabiliana na minyoo mashuleni, usafi wa vyoo na ujenzi wa vyoo bora katika mashule yetu ambayo tumefanya kwa zaidi ya miaka Sita, pia wamekuja kuangalia namna ya kukabiliana na ugonjwa wa trakoma”. Alisema Dkt. Method 
Aidha, Dkt. Method amewashukuru wafadhili hao kutoka Taasisi ya Bill and Melinda Gate na THE END FUND kwa msaada mkubwa ambao wamekuwa wakitoa katika kuisaidia Serikali ya Tanzania na jamii kwa ujumla kwaajili ya kupambana na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
Kwa upande wake Afisa Mipango kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kutoka Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto Oscar Kaitaba akieleza namna Taasisi ya THE  FUND na Bill and Melinda Gate ilivyosaidia Wizara amesema kuwa ;-
“THE END FUND imekuwa ikishirikiana na Wizara ya Afya katika kudhibiti ugonjwa wa Vikope (Trakoma) na ugonjwa wa Matende na Mabusha kwa kuwafanyia upasuaji katika Mikoa ya Tanga, Pwani na sehem chache Mkoa wa Dar es salaam”,Alisema Oscar Kaitaba
Oscar Kaitaba aliendelea kuwa Kwa ugonjwa wa Trakoma wamesaidia kufanya upasuaji wa Kope katika Mikoa ya Kilimanjaro katika Wilaya ya SIHA na Arusha katika maeneo ya watu waliohathirika zaidi na ugonjwa huu.


Ijumaa, 6 Julai 2018

UBALOZI WA JAPAN YAMUUNGA MKONO MHE. UMMY KUJENGA MADARASA MKOANI TANGA

- Hakuna maoni


PICHA ZINAZOONYESHA TUKIO LA UTIAJI SAINI MAKUBALIANO YA UJENZI WA MADARASA 6 KATIKA SHULE YA MSINGI MWAKIDILA MKOANI TANGA KATI YA UBALOZI WA JAPAN NA TAASISI YA MAENDELEO YA WANAWAKE  TANGA ( TAWODE).

NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

Serikali ya Japan kupitia ubalozi wa Japan nchini Tanzania imetoa kiasi cha shilingi miliioni 188 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 6 ya shule ya msingi Mwakidila kata ya Tangasisi iliyopo Jijini Tanga
Fedha hizo zimetolewa leo jijini hapa kupitia  Shirika la Maendeleo ya Wanawake wa Mkoa wa Tanga (TAWODE) chini ya Mwenyekiti wake Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu .
Ubalozi wa Japan nchini imetoa fedha hizo ikiwa  ni kuunga mkono  jitihada za Serikali za kuboresha  miundombinu ya elimu ya Msingi na Sekondari katika jiji la Tanga.
Akiongea wakati wa hafla ya kutia saini mkataba wa ujenzi wa madarasa hayo Balozi wa Japan Nchini Tanzania Mhe. Masaharu Yoshida  alisema Serikali ya japan imetoa fedha hizo  ili kusaidia maendeleo ya elimu kwa Jiji la Tanza ili kutatua  tatizo la mrundikano wa wanafunzi madarsani
Aidha, Balozi Yoshida  ameitaka TAWODE kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kikamilifu  na kukamilisha ujenzi huo wa madarasa kwa wakati.
Akiongea wakati wa kutiana saini mkataba huo Mwenyekiti wa TAWODE, Waziri Ummy Mwalimu ameushukuru Ubalozi wa Japan nchini kwa kukubali ombi la kufadhili ujenzi wa madarasa  ya shule hiyo ya Msingi  Mwakidila ambayo ina wanafunzi zaidi ya 1,400 kulinganisha na madarasa yaliyopo.
“Sisi kama sehemu ya wanajamii wa Jiji la Tanga tuliona tuna wajibu wa kuunga mkono Serikali kwa kutafuta vyanzo vingine vya fedha ili kuwezesha elimu ya Msingi na ile ya sekondari hususan changamoto ya madarasa itatuliwe hivyo fedha hizi ni za jamii ya Wana Tanga hivyo TAWODE tutahakikisha zinatumika ipasavyo”.Alisema Waziri Ummy.
Hata hivyo alisema hivi sasa kumekuwa na changamoto ya madarasa kwenye halmashauri mbalimbali nchini  kutokana na ongezeko la wanafunzi  kutokana na  Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt.John Magufuli ya kutoa elimu bure .
Kwa upande wake Meya wa Jiji la Tanga Mhe.Selebosi Mhina ameushukuru Ubalozi wa japan pamoja na kumpongeza Mhe.Ummy mwalimu kwa kuwa bega kwa bega katika kusukuma  mbele maendeleo ya wananchi wa Tanga katika sekta ya Elimu na Afya.

Jumatano, 4 Julai 2018

GLOBAL FUND YARIDHISHWA NA UTENDAJI WA WIZARA YA AFYA NCHINI.

- Hakuna maoni




Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa kikao na wawakilishi wa Mfuko wa Pamoja wa Dunia wa kushughulikia magonjwa ya TB,Maralia na Ukimwi(GLOBAL FUND)  hawapo pichani kilichofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Mfuko wa Pamoja wa Dunia wa kushughulikia magonjwa ya TB,Maralia na Ukimwi (GLOBAL FUND)  hapa nchini Dkt. Sai Kumar kulia akimueleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa kikao cha kujadili mambo mbalimbali ya afya kilichofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia  akizungumza na Naibu Waziri wake Dkt. Faustine Ndugulile kushoto wakati wa kikao na wawakilishi wa Mfuko wa Pamoja wa Dunia wa kushughulikia magonjwa ya TB,Maralia na Ukimwi (GLOBAL FUND)  hawapo pichani kilichofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akizungumza wakati wa kikao na wawakilishi wa Mfuko wa Pamoja wa Dunia wa kushughulikia magonjwa ya TB,Maralia na Ukimwi (GLOBAL FUND) kilichofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile.


Na WAMJW-DSM
 
Mfuko wa pamoja wa  Dunia wa kupambana na magonjwa ya UKIMWI,Malaria na Kifua Kikuu (GLOBAL FUND) umeridhishwa kwa kiasi kikubwa na Jinsi Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya katika kupambana na magonjwa hayo.

Pamoja na hayo Wawakilishi wa Mfuko huo hapa Nchini wamesema kuwa kutokana na mwenendo mzuri wa Tanzania katika kutumia vizuri Mfuko huo sasa wanaweza kuanzisha kitu kingine kizuri kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya na kupeleka mapendekezo na kukubaliwa.

Malengo ya kikao hiko  kati ya Global Fund na Wizara ya Afya ilikuwa ni kujadili ,kupanga na kuboresha Sekta ya Afya nchini.

Jumanne, 3 Julai 2018

KIWANDA CHA DAWA KIKUBWA KUJENGWA NCHINI.

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya Wadau wa Masuala ya Uwekezaji na masuala ya Afya wakati akiwa katika Kikao cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka nchini China.

Picha ya Wadau wa Masuala ya Uwekezaji na Masuala ya Afya, ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage katika Kikao cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka nchini China.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akijadili jambo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage katika Kikao cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka nchini China.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimuaga Rais wa Kampuni ya Fosun Pharma inayotarajia kufungua kiwanda cha uzalishaji wa Dawa hapa nchini hivi karibuni baada ya majadiliano yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Kituo cha uwekezaji yaliyomuhusisha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage.

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage baada ya kikao cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka nchini China.

NA WAMJW-DAR ES SALAAM

KIWANDA kikubwa cha kutengeneza dawa kinatarajiwa kujengwa nchini ili kupunguza adha na gharama zinazoikumba nchi wakati wa  kuagiza dawa nje ya Tanzania. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa kujadili uwekezaji wa kiwanda cha dawa hapa nchini leo jijini Dar es salaam. 

"Leo tumekutana kujadili jinsi ya kuwekeza na kiwanda cha kutengeneza dawa cha FOSUN PHARMA kutoka nchini ili kupunguza changamoto za kuagiza dawa nje ya nchi na kutokomeza tatizo la upatikanaji wa dawa nchini", alisema Waziri  Ummy . 

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa kutokana na kujengwa kwa kiwanda hiko kitapunguza asilimia kubwa ya fedha inayokwenda nje kwa ajili ya manunuzi ya dawa kwani mpaka sasa asilimia 94 ya fedha zinakwenda kununua dawa nje na asilimia 6 ndiyo inannua dawa nchini. 

Waziri Ummy amesema kuwa kutokana na uwekezaji huo kutapelekea kupunguza muda wa kuagiza dawa kwani muda mwingine kunachukua miezi 9 mpaka miezi 11 kupata dawa kutoka nje ya nchi hivyo kuifanya Serikali kuagiza mzigo mkubwa zaidi ili kukimbizana na mahitaji ya Watanzania. 

"Tunatumia mda mrefu sana kupata dawa tangu tunapoagiza na wakati mwingine tunaweza kupata dawa zisizo na ubora kutokana na dawa hizo zinakaguliwa na mdhibiti wa nje hivyo zinaweza zikaruhusiwa tu na zikija kukaguliwa na mdhibiti wa ndani unaweza kukuta hazina ubora" alisema Waziri Ummy. 

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa kampuni hiyo inayotengeza sindano za kutibu Maralia kali ya ATESUNAT itaweza kutengeneza sindano nyingi zaidi na kuweza kuwahudumia nchi jirani ikiwemo Kenya, Uganda na Burundi. 

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema kuwa hakuna kikwazo kwa Kampuni hiyo kuanzisha ujenzi wa kiwanda cha dawa hapa nchini kwani kitasaidia upatikanaji wa dawa kwa urahisi na kukua kwa uchumi kupitia viwanda. 

"Tumejadili na kuwakubalia bila ya kuweka kikwazo kwani tumeridhishwa na ubora wao katika utengenezaji wa dawa na mafuta nchini kwao hivyo tunawakaribisha kuja kufanya uwekezaji huo" alisema Waziri Mwijage. 

Naye Mkurugenzi wa Kituo Cha Uwekezaji Nchini Bw. Geofrey Mwambe amesema kuwa wameupokea uwekezaji huo na wanaufanyia kazi haraka iwezekanavyo ili kuipeleka Tanzania kuelekea uchumi wa Viwanda. 

"Kutokana na ahadi ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli la kuipeleka nchi kwenye uchumi wa viwanda na kutokomeza kabisa tatizo la uhaba wa dawa hatuna budi kushirikiana na wawekezaji hao kutimiza lengo hilo" alisema Bw. Mwambe. 

Kika hiko cha kujadili uwekezaji wa kiwanda hiko cha kutengeneza dawa kimeudhuriwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu,  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA, Bohari kuu ya Dawa MSD,  Kituo cha Uwekezaji nchini TIC na wadau mbalimbali.

Jumatatu, 2 Julai 2018

WIZARA YA AFYA YATANGAZA RASMI KUPOKEA HOSPITALI ZA RUFA ZA MIKOA.

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelekezo juu ya matangazo yaliyo kwenye mbao mapema leo wakati alipofanya ziara ya kukagua huduma za Afya zinazotolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimsikiliza moja kati ya wagonjwa waliofika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala wakati alipofanya ziara mapema leo katika Hospitali hiyo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimsikiliza kwa makini Bi Halima Said aliyefika kupata huduma za matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala pindi alipofanya ziara mapema leo katika Hospitali hiyo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na Bi. Angelina Erasto juu ya umuhimu wa kukata Bima ya Afya ya TOTO AFYA KADI itakayomsaidia kupunguza gharama za matibabu kwa mtoto wake,

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akishangaa idadi kubwa ya wakina mama iliyozidi kiasi katika wodi ya kupumzikia wakina mama baada ya kujifungua, akiwa katika ziara yake ya kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala kukagua ubora wa Huduma zitolewazo katika Hospitali hiyo.


NA WAMJJW-DAR ES SALAAM
WIZARA ya afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imetangaza rasmi kuanzia Juali 1 2018  imepokea Hospitali 28 za Rufaa za Mikoa ambazo zilikuwa chini ya usimamizi wa OR-TAMISEMI .

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala.

“Hospitali ambazo tumezipokea zina jumla ya vitanda 7,474 na jumla ya watumishi 8,671 ambao, kati yao Wauguzi ni 3,960, Madaktari 536, Madaktari Bingwa wa fani mbalimbali ni 182, na waliobakia ni watumishi wa kada zingine mbalimbali za Afya” alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema kuwa Hospitali ambazo Wizara imezipokea ni Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mount Meru (Arusha), Dodoma General (Dodoma), Kitete (Tabora), Shinyanga, Geita, Singida, Mpanda (Katavi), Mawenzi (Kilimanjaro), Bombo (Tanga), Morogoro, Ligula (Mtwara), Sokoine (Lindi), Maweni (Kigoma), Sekou Toure (Mwanza), Mwananyamala, Amana, Temeke (Dar es Salaam), Songwe, Kibena (Njombe), Iringa, Tumbi (Pwani), Sumbawanga (Rukwa), Bariadi (Simiyu), Musoma (Mara), Songea (Ruvuma), Mbeya, Babati (Manyara) na Bukoba (Kagera).

Waziri Ummy alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2018/19, Wizara imetenga shilingi Bilioni 30 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya kipaumbele katika Hospitali za Rufaa za Mikoa ambako tayari huduma zinatolewa ikiwemo Matibabu kwa wagonjwa wa dharura ,Huduma za upasuaji wa dharura hususan wakati wa ujauzito na uzazi pamoja na Huduma za tiba kwa wagonjwa mahututi zikiwemo za watoto wachanga .

Mbali na hayo Waziri  Ummy amesikitishwa na upungufu wa wodi pamoja na vitanda kwa ajili ya  wanawake wanaofika kujifungua katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala na kuahidi kulifanyia kazi mara moja iwezekanavo.

“Kama Mama,na nimeumia sana na lazima tulifanyie ufumbuzi mara moja kwahiyo namuagiza katibu mkuu alete mtaalamu wa majengo na tupandishe fedha za kujenga ghorofa mbili mara moja kwakweli halii hii haikubaliki” alisema Waziri Ummy.

Mnamo Novemba 25, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizindua Hospitali ya Taaluma na Tiba (MAMC) ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) aliagiza kuwa Hospitali za Rufaa za Mikoa zihamishiwe kwenye usimamizi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (WAMJW) kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI.