Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 5 Agosti 2019

WATOA HUDUMA ZA AFYA KIGOMA KUPIMWA UTAYARI KUKABILIANA NA EBOLA

Consolata Felix kutoka Wizara ya Afya (aliyesimama kushoto) akifuatilia zoezi la vitendo la utayari wa kukabiliana ugonjwa wa ebola kwa watoa huduma za afya katika jamii.
Washiriki wa zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa ebola Mkoa wa Kigoma wakiwa kwenye mazoezi ya mezani kujadili mikakati ya kudhibiti ugonjwa huo usiingie nchini mapema leo Mjini Kigoma.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Bw  Daniel Machunda akisema jambo kwa washiriki wa kikao kazi katika zoezi la upimaji wa utayari wa kukabiliana na ugonjwa ebola (hawapo pichani) mapema leo Mjini Kigoma.

Picha ya pamoja ya mgenu rasmi Bw . Daniel Machunda (aliyeketi kati kati) wadau wa maendeleo na washiriki wa zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa ebola nchini katika Mkoa wa Kigoma


Na Englibert Kayombo, Kigoma.

SEREKALI ya Tanzania kupitia uratibu wa wa ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  zitafanya zoezi la kupima utayari kwa watoa huduma za afya katika kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika Mkoa wa Kigoma.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Maafa  Ofisi ya Waziri Mkuu Bwana Bashiru Taratibu wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha wadau kutoka ndani nan je ya nchi kujadili mikakati iliyopo kudhibiti ugonjwa huo usiingie nchini.

Amesema kuwa zoezi hilo litazingatia dhana ya afya moja ambayo hujumuisha sekta ya afya ya mifugo,binadamu,mifugo,wanyamapori na mazingira katika kujiandaa,kufuatilia na kukabili magonjwa ambayo huambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda binaadamu.

"Zoezi hili litapima uelewa wa jamii kuhusu namna ambavyo wanapaswa kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa ebola, hivyo wakati wa zoezi watoa huduma za afya na sekta zingine watakuwa wakifanya zoezi hilo kwa vitendo"alisema

Bw. Taratibu amesema kuwa zoezi hilo litafanyika kuanzia tarehe 5 hadi 9 Agosti katika vituo vya kutolea huduma za afya na maeneo ya mipaka ya Mkoa wa Kigoma. Aliendelea kwa kusema kuwa katika zoezi hilo watoa huduma wa afya watakuwa wakifanya zoezi hilo kwa vitendo namna ya kumuhudumia mgonjwa wa ebola atakapogundulika.

Mgeni rasmi katika kikao hicho Daniel Machunda Kaimu katibu Tawala Msaidizi rasilimali watu kwaniaba ya katibu wa Mkoa wa Kigoma Rashid Mchata alisema Mkoa wa Kigoma una njia nyingi zisizo za halali za mipakani(panya road)ambazo zinachangia hatari ya ugonjwa wa Ebola kuingia nchini.

Aliwataka wananchi kuchukua tahadhari hasa wale wanaovuka mipaka kwenda nchi za jirani."Ikumbukwe kuwa zoezi linahusu upimaji wa utayari kwa Mkoa wa Kigoma na hakuna mgonjwa yeyote wa ebola aliyeripotiwa hadi sasa nchini"alisema Machunda

Mganga mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt Paul Chawote alisema kuwa nchi ya jirani ya DRC(Congo)imeendelea kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola tangu kulipotiwa mlipuko wa ugonjwa huo mnamo mwezi Agosti mwaka 2018.

Dkt Chawote amesema kuwa idadi ya vifo vilikuwa 1823 ikiwa ni sawa na asilimia 67 ya idadi watu walioathiriwa na ugonjwa huo huku nchi ya Uganda ambayo inapakana na DRC na Tanzania imekuwa na wagonjwa 3 wa Ebola kwa mujibu wa taarifa maambukizi hayo yametoka DRC.

"Kwenye mipaka yetu ya DRC na Burundi kuna mwingiliano mkubwa wa watu unaochangiwa na shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi hivyo vinachangia hatari zaidi ya ugonjwa wa Ebol kuingia nchini"alisema Dkt Chawote

Remidius Kakulu Afida Afya mwandamizi toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amesema mpaka sasa mipaka iliyorasmi yote imedhibitiwa na tayati Serikali imefunga vipima joto vya kisasa katika mipaka yote iliyo rasmi.

"Kuna ile mipaka ambayo siyo rasmi ambayo ipo kwenye vijiji na maeneo mengine tunawaomba Viongozi wa Vijiji pamoja na wananchi kutoa taarifa pale mgeni anapoingia au kumpeleka kituo cha afya ili aweze kupimwa"alisema

Mwisho

0 on: "WATOA HUDUMA ZA AFYA KIGOMA KUPIMWA UTAYARI KUKABILIANA NA EBOLA"