Mwakilishi kutoka Hospitali
ya Benjamini Mkapa akibadilishana mkataba wa makubaliano na Mkurugenzi Mkazi wa
amref health afrika Tanzania Dkt. Florence Temu baada ya kusainiwa na pande
zote mbili wakati wa uzinduzi wa mradi wa amref health afrika wa kupambana na
ukimwi na kifua kikuu unaofadhiliwa na mfuko wa dunia.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisema
jambo mbele ya Wakurugenzi na Wawakilishi kutoka taasisi zisizo za Kiserikali
katika siku ya uzinduzi wa mradi wa amref health afrika wa kupambana na ukimwi
na kifua kikuu unaofadhiliwa na mfuko wa dunia (global fund).
Mkurugenzi Mkazi wa amref
health afrika Tanzania Dkt. Florence Temu akisoma hotuba mbele ya mgeni rasmi
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine
Ndugulile wakati wa uzinduzi wa mradi wa amref health afrika wa kupambana na
ukimwi na kifua kikuu unaofadhiliwa na mfuko wa dunia (global fund).
Mkurugenzi Mtendaji wa TAYOA Peter
Masika akitoa neno la shukrani mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile,
Wakurugenzi na Wawakilishi wa taasisi zisizo za Kiserikali wakati wa uzinduzi
wa mradi wa amref health afrika wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu.
Wakurugenzi na Wawakilishi wa taasisi zisizo
za Kiserikali wakifuatilia kwa makini tamko la Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa uzinduzi wa
mradi wa amref health afrika wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaofadhiliwa
na mfuko wa dunia (global fund).
Mkurugenzi Mtendaji wa TAYOA
Peter Masika akibadilishana mkataba wa makubaliano na Mkurugenzi Mkazi wa amref
health afrika Tanzania Dkt. Florence Temu baada ya kusainiwa na pande zote
mbili wakati wa uzinduzi wa mradi wa amref health afrika wa kupambana na ukimwi
na kifua kikuu unaofadhiliwa na mfuko wa dunia.
Picha ya pamoja ikiongozwa na
mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto
Dkt. Faustine Ndugulile na Mkurugenzi Mkazi wa amref health afrika Tanzania
Dkt. Florence Temu wakiwa na Wawakilishi wa taasisi zisizo za Kiserikali wakati
wa uzinduzi wa mradi wa amref health afrika wa kupambana na ukimwi na kifua
kikuu unaofadhiliwa na mfuko wa dunia.
Na WAMJW.DSM
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile amelitaka
Shirika la Afya lisilo Lakiserikali Amref kuweka mbinu na mikakati ya kibunifu
katika kuanikisha afua mbali mbali za kupambana na magonjwa ya VVU na Kifua
Kikuu.
Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mradi
wa amref health afrika wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaofadhiliwa na
mfuko wa dunia (global fund) mapema leo jijini Dar es salaam.
“Niwaombe watekelezaji wote
wa Afua, katika mambo ambayo tunataka kuyaona ni pamoja na ubunifu, ubunifu
wakufikia malengo lakini kitu kingine ni mikakati ya kufikia malengo” alisema
Dkt. Ndugulile
Dkt. Ndugulile aliendelea
kusema kuwa Serikali inatarajia kuona ifikapo 2020 malengo yote yanafanikiwa
huku akiwataka kuzingatia matumizi sahihi ya fedha kulingana na malengo
waliojiwekea.
“Tunatarajia, kwasababu ni
nyinyi mlioandika uhitaji wa fedha na mlijiamini kabisa kwamba mnaweza kutekeleza
hizo afua nendeni mkatekeleze, sisi Serikali tutaendelea kuwapa ushirikiano
muda wowote na wakati wowote” alisema Dkt. Ndugulile
Aidha, Dkt Ndugilile alisema
kuwa Serikali
kwa kushirikiana na wadau tumefanikiwa kutengeneza na kuweka miongozo
mbalimbali ili kuhakikisha ufanisi na utaratibu mzuri unafuatwa katika
kutekeleza mipango iliyoainishwa jambo litalosaidia kuepuka utendaji usio sahihi na kutekeleza kwa namna yake.
Mbali
na hayo alisema kuwa Serikali ya Tanzania inakusudia ifikapo mwaka
2022 asilimia 95% ya watu wote wanaoishi na Virusi vya UKIMWI kuwa kwenye dawa,
Vile vile, kuhakikisha ifikapo 2022 asilimia 90% watoto waliofikia vigezo na
wanaoishi na maambukizi wanabaki kwenye dawa na 95% ya watu wazima wanapatiwa
ART na kuendelea kubaki kwenye dawa.
Kwa
upande wa Kifua Kikuu Ndugulile alisema kuwa Kifua kikuu (TB) bado ni tatizo
nchini kwetu huku jumla ya watu 160,000 wanakadiriwa kuwa na ugonjwa huu nchini
Tanzania. Jumla ya Wagonjwa wapya wapatao 68,819 waliibuliwa mwaka 2017 ikilinganishwa na 62,182 mwaka
2015.
Nae
Mkurugenzi Mkazi kutoka Amref Dkt. Florence Temu alisema kuwa katika kufikia
adhma ya Serikali kufikia asilkmia 90 ya waishio na VVU kuwa wamepima na kujua
majibu yao, asilimia 90 ya wenye VVU kupatiwa tiba na asilimia 90 ya walio kwenye
tiba za VVU wafanikiwe kufubaza VVU (90 90 90) Amref health Afrika
ilihidhinishwa rasmi kuwa asasi itakayochukua jukumu la kusimamia na kuratibu
afua za kwenye jamii zihusuzo VVU na Kifua Kikuu kwa kupitia Asasi ya kijamii.
Dkt.
Temu aliendelea kusema kuwa mradi huu wa VVU na Kifua Kikuu wenye thamani ya
shilingi Billioni 55 na Million 256 na Laki 7 ($ 24,969,174) wenye dhamira ya
kufikia Watanzania 546,880 watafikiwa na huduma ya kupima VVU na kujua majibu,
huku wasichana wa umri balehe na wanawake 162,064 ili kuibua na kuwapatia rufaa
wenye maambukizi ya Kifua Kikuu wapatao 16,465 katika mikoa 15 ya Arusha,
Dodoma, Kilimanjaro, Manyara, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Pwani,
Shinyanga, Simiyu, Singida, Tanga na Ruvuma.