Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumanne, 24 Desemba 2019

HOSPITALI YA KANDA YA KUSINI KUANZA KAZI MWAKANI

- Hakuna maoni





Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa hospitali ya rufaa ya kanda ya kusini kukamilisha ujenzi wa hospitali hiyo ili ianze kutoa huduma ifikapo juni 2020.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati alipotembelea na  kukagua maendeleo ya ujenzi wa hosputali hiyo ambayo na shirika la Taifa la nyumba (NHC)

“Nimeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa hospitali  hii,ninakutaka  ufanye kazi usiku na mchana ili ikiwezekana Hospitali ianze kutoa huduma ifikapo Juni,2020".Alisisitiza Waziri Ummy

Katika Ziara yake Waziri huyo pia alitembelea zahanati ya Ufukoni iliyopo Manispaa ya Mtwara na kukagua utoaji wa huduma ambapo katika kliniki ya watoto alikutana na changamoto ya uhaba wa chanjo hususan chanjo ya Surua na kuelekeza mkoa ufanye mawasiliano ya haraka na Mpango wa taifa wa  Chanjo ili kupatiwa chanjo hizo.

Aidha, Waziri Ummy aliwataka wananchi waliokuwa wamefika kupata huduma kwenye zahanati hiyo  wajiunge na Bima za Afya ili waondokane na tatizo la kukosa fedha za matibabu pindi wanapohitaji matibabu

Hata hivyo katika ziara yake kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa ya mtwara Ligula,Waziri Ummy ameridhishwa na hali ya upatikanaji wa dawa muhimu na hivyo kuwata viongozi wa hospitali hiyo.kuhakikisha wanatoa.vipaumbele katika masuala yanayojitokeza ikiwemo kuhakikisha wanatafuta ufumbuzi mapema kwa kufuata taratibu na miongozo ya kazi zao ili kuweza kuwahudumia wananchi kwa wakati.

Jumapili, 22 Desemba 2019

WANANCHI SASA KUJIPIMA VIRUSI VYA UKIMWI - WAZIRI UMMY

Nembo ya UKIMWI





Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akieleza jambo wakati akiwa katika ziara ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya na ujenzi wa miundombinu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi

WANANCHI SASA KUJIPIMA VIRUSI VYA UKIMWI - WAZIRI UMMY

Na Rayson Mwaisemba, WAMJW- Katavi.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo amesema kuwa bunge la Tanzania limerasimisha sheria ya Wananchi kuweza kujipima wenyewe maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU).

Waziri Ummy amesema hayo leo Disemba 20 katika ziara ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya na ujenzi wa miundombinu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, ikiwa ni jitihada za Serikali za kuboresha huduma za Afya nchini.

"Napenda kuwapa Habari njema kuwa Bunge la Mwezi wa 11 limepitisha Sheria, kwahiyo sasa ni rasmi Tanzania mtu kujipima maambukizi ya VVU mwenyewe, kwahiyo hivi vitendanishi (vifaa) vitakuwa vinauzwa kwenye maduka, pia kugawa bure baadhi ya maeneo kwa sababu wakati mwingine watu wanaona unyanyapaa kwenda kupima wenyewe," Amesema Waziri Ummy.

Ameendelea kusema kuwa, Serikali imeweka angalizo kuwa, kujipima mwenyewe sio majibu ya mwisho, hivyo kuwataka wananchi kuwa, baada ya kujipima wanatakiwa kwenda katika vituo vya kutolea huduma za Afya kwa ajili ya kuthibitisha na ushauri zaidi wa jinsi ya kuishi.

Aidha, Waziri Ummy ameagiza kuendelea kutoa elimu ya Afya kwa wananchi, hususan watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi kutumia dawa kwa usahihi kulingana na maelekezo ya Watoa huduma za Afya katika vituo vya kutolea huduma za Afya nchini.

"Tuendelee kuhakikisha watu wote waliobainika na ugonjwa wa Ukimwi, waendelee kutumia dawa kwa usahihi kama walivyoelekezwa na Wataalamu wetu katika vituo vya kutolea huduma za Afya nchini". amesema Waziri Ummy.

Mbali na hayo, amesema kuwa kuna changamoto ya maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 mpaka 24, huku akiweka wazi kuwa kitaifa hali ya maambukizi mapya kwa vijana hao ni asilimia 40%, huku vijana wa kike ikiwa ni asilimia 80 na wakiume ikiwa ni asilimia 20.

Kwa upande mwingine Waziri Ummy amewatia moyo wanaoishi na maambukizi ya VVU kwa kuwakumbusha kuwa, kuhudhuria katika vituo vya Afya na kufuata maelekezo kama walivyopewa na Watoa huduma, pia kuishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi sio mwisho wa maisha.

"Niendelee kuwatia moyo kuwa na maambukizi ya Ukimwi sio mwisho wa Dunia, sio sentensi ya kifo, sikuhizi watu Wanaishi vizuri, kwahiyo nawahimiza kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya, kupima na kuanza kutumia dawa". Amesema Waziri Ummy.

Nae Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi, ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bi Lilian Matinga amesema kuwa, hali ya upatikanaji wa dawa ipo vizuri Mkoani hapo, huku akidai kuwa kwa mwaka 2017/2018 bajeti ya dawa na vitendanishi ilikuwa Bilioni 2.9 na kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Mkoa umetengewa jumla ya shilingi Bilioni 3.97 ikiwa ni ongezeko la shilingi Milioni 460.07.

Aliendelea kusema kuwa, kwa sasa hali ya upatikanaji wa dawa muhimu ni zaidi ya asilimia 90% katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya nchini. alisisitiza.

Mwisho.

Ijumaa, 20 Desemba 2019

MUUGUZI ANAYETUHUMIWA KUBAKA MJAMZITO ASIMAMISHWA KAZI.

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, akielekeza jambo mbele ya Wananchi waliojitokeza katika viwanja vya shule ya msingi Majalila Wilaya ya Mpanda, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma katika Mkoa wa Katavi.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda (Tanganyika) Bi Lilian Matinga akiwasalimu Wananchi, katika viwanja vya shule ya msingi Majalila Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi.

Wananchi waliojitokeza katika viwanja vya shule ya msingi Majalila Wilaya ya Mpanda (Tanganyika) kumsikiliza Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Mkoa wa Katavi.


MUUGUZI ANAYETUHUMIWA KUBAKA MJAMZITO ASIMAMISHWA KAZI.

Na Rayson Mwaisemba WAMJW- Katavi

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo ameliagiza Baraza la Uuguzi na Ukunga kumsimamisha kazi muuguzi anayetuhumiwa kumbaka mama mjamzito katika kituo cha Afya Mamba kilichopo Kijiji cha Mamba Mkoani Katavi ili kupisha uchunguzi.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati akiongea na Wananchi katika viwanja vya shule ya msingi Majalila Wilaya ya Mpanda, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na uboreshaji wa miundombinu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi.

"Naliagiza baraza la wauguzi na ukunga kusimamisha leseni ya muuguzi huyu wakati uchunguzi unafanyika  ".Amesema Waziri Ummy

Aidha,amewataka watumishi  wote wa afya nchini kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, weledi na viapo vya kazi zao

“Na yeyote atakayefanya kazi kinyume na maadili,weledi na kiapo chake tutamchukulia hatua za nidhamu ikowemo kuwafutia leseni zao na kuwapeleka katika vyombo vya dola"Amesisitiza Waziri Ummy.

#TunaboreshaAfya

HOSPITALI YA KANDA YA RUFAA MBEYA (MZRH) YAANZISHA KIWANDA CHA UZALISHAJI MAJI TIBA (DRIP)

- Hakuna maoni
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji akiongea na Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake (hawapo pichani) wakati walipotembelea Hospitali hiyo ili kuona mafanikio katika kipindi cha miaka minne ya Rais Magufuli madarakani.

Baadhi ya chupa za maji ya tiba zinazotengenezwa na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.

Mtaalamu akionesha jinsi maji ya tiba yanavyotengenezwa

Mashine ya kutengeneza maji ya tiba



Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya imetaja mafanikio iliyopata katika kipindi cha miaka minne ya Rais Dkt. John  Pombe Magufuli akiwa madarakani ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa kiwanda chenye uwezo wa kuzalisha maji tiba lita 3,840  kwa mwezi.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dkt. Godlove Mbwanji alipokuwa akizungumza na Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Wizara ya Afya na Taasisi zake walioambatana na waandishi mbalimbali wa habari katika kutekeleza kampeni ya “Tumeboresha Sekta Ya Afya” katika mikoa ya nyanda za juu kusini.

Dkt. Mbwanji amesema Hospitali hiyo imetekeleza kwa vitendo sera ya Viwanda ya Awamu ya Tano pamoja maagizo ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kuanzisha kiwanda cha uzalishaji wa maji tiba “Drip”.

Amesema kiwanda hicho kilianzishwa Februari 2019 kwa gharama ya TSh. Milioni 120  kwa mapato ya ndani na kinazalisha dripu hizo zenye lita za ujazo 250 na 500 zimeanza kutumika kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wenye uhitaji.

“Hali hii imesaidia kuondokana na adha ya kununua au kuagiza dripu nje ya nchi na kiwanda kina uwezo wa kutengeneza maji tiba lita 3840  kwa mwezi huku uhitaji wa hospitali ni lita 5232 na hivyo kukidhi kwa asilimia 73 ya uhitaji wa maji tiba kwa ajili ya hospitali”. Amesema Dkt. Mbwanji.

Mkurugenzi huyo amesema wamefanikiwa kupunguza gharama za manunuzi ya maji tiba nje nchi, wana uhakika na upatikanaji wake, wametoa mafunzo ya utaalam wa utengenezaji wa maji tiba na kuongeza ajira kwa wataalamu wa kutengeneza bidhaa hiyo.

Aidha Dkt. Mbwanji amesema wanatarajia kuanza kutengeneza dawa ya macho na masikio kwenye kiwanda hicho mwaka 2020.

Hospitali hiyo inahudumia mikoa saba ya Nyanda za juu kusini  ambayo ni Iringa, Njombe, Ruvuma, Katavi Rukwa, Songwe na Mbeya na  imeendelea kuboresha huduma zake mbalimbali ili kutoa huduma bora za afya kwa wananchi.

Mafanikio mengine yaliyotajwa ni pamoja na kuwa na ongezeko la upatikanaji wa dawa kutoka asilimia 70 hadi 95,  ongezeko la madaktari bingwa kutoka 36 hadi 53, huduma za kibingwa za masikio, koo, pua.

Pia amesema kuanzishwa kwa chuo cha Udaktari cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tawi la Mbeya kumetoa fursa kwa madaktari kuanza kufanya tafiti mbalimbali, kuanzishwa kwa huduma ya mkalimani wa lugha ya alama, uwezo wa kulaza wagonjwa kutoka vitanda 477 hadi 553 baada ya kukamilika jengo la watoto.

Dkt. Mbwanji amesema Serikali ilitoa TSh. Bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Radiolojia ambalo baada ya kukamilika limefanikisha utoaji wa huduma za mionzi na kuanzisha huduma mpya za  CT Scan, mashine za kidigitali za X ray, Fluoroscopy, Mammography na Ultrasound.

MWISHO

SERIKALI YADHAMIRIA KUBORESHA HUDUMA ZA RUFAA

- Hakuna maoni
Waziri Ummy, akieleza jambo wakati akiwa katika ziara ya kukagua hali ya utoaji  huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Honoratha Rutatinisibwa akitoa taarifa ya hali ya Afya katika Mkoa wa Tabora wakati wa ziara ya Waziri Ummy katika Mkoa huo.

Waziri wa Afya,Maendeleo  ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.@umwalimu akiongea na baadhi ya wanawake waliofika kupata huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.@umwalimu akikagua uboreshaji miundombinu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, pindi alipofanya ziara katika Mkoa huo.
Wananchi wa Tabora wakisikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwasilisha Salam kutoka kwa Mhe. Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt.@MagufuliJP kwa wananchi hao.

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.@umwalimu baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na miundombinu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora.



SERIKALI YADHAMIRIA KUBORESHA HUDUMA ZA RUFAA

Na Rayson Mwaisemba WAMJW- TABORA

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imedhamiria kuboresha huduma za Rufaa katika Hospitali za Rufaa za mikoa kwa kuhakikisha inaboresha kwa kujenga miundombinu ya majengo ya dharura na ajali.

Hayo yamesemwa, na Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora.

" Sisi kama Serikali, tumedhamiria kuboresha huduma za Rufaa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa, kwa kuhakikisha tunaweka miundombinu, hususan jengo la dharura na ajali ". alisema Waziri Ummy Mwalimu.

Hata hivyo, Waziri Ummy alisema Serikali imedhamiria kuboresha huduma za Afya kwa wananchi, kwa kutenga takribani Bilioni 8.8 kwa ajili ya ujenzi wa zaidi ya Vituo vya Afya 13, huku akieleza kuwa Hospitali za Wilaya za Sikonge na Uyui nazo zinaendelea kujengwa hali itakayosaidia kupunguza mzigo kwa Hospitali ya Mkoa.

"Sisi kama Serikali tumedhamiria kuboresha huduma za Afya, kuanzia miundombinu, Serikali tunajenga vituo vya Afya zaidi ya 13, ambayo takribani Bilioni 8.8 zimeshaingizwa na vingine nimeanza kutoa huduma lakini tunajenga Hospitali mbili za Wilaya ambazo ni Sikonge pamoja na Uyui" alisema

Licha ya kupunguza kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria nchini, Waziri Ummy ameagiza kupitia Maafisa Afya kutoa elimu kwa wananchi ili kutokomeza mazalia ya mbu waenezao Malaria, huku akisisitiza kuwa ni lazima Halmashauri kununua viuadudu vya kuangamiza viluilui katika mazalia ya mbu.

Mbali na hayo, Waziri Ummy aliipongeza timu ya Afya ya Mkoa kwa jitihada inazozichukua katika kuimarisha usafi wa mazingira hususan katika ujenzi na matumizi ya vyoo bora jambo litalosaidia kupunguza magonjwa ya kuhara, magonjwa ya tumbo na Kipindupindu.

"Ujenzi na matumizi ya vyoo Bora ndani ya mwaka mmoja mmetoka Asilimia 53.7 mpaka asilimia 59, lakini pia tumepunguza kaya ambazo hazina vyoo kabisa kutoka asilimia 7 mpaka asilimia 2" alisema.

Kwa upande mwingine, ameagiza asilimia 2 ya watu wasiokuwa na vyoo kutafutwa ili kuhakikisha wanajenga vyoo na kuvitumia kwa usahihi, huku akisisitiza wasiofanya hivyo ndani ya muda wa makubaliano wachukuliwe hatua za kisheria, alisisitiza.

Pia, Waziri Ummy alisema kuwa katika Mkoa wa Tabora vifo vya akina mama wajawazito vimepungua kutoka wajawazito 99 mpaka wajawazito 60 kwa mwaka huku akisisitiza Watoa huduma kuendelea kujituma ili kuhakikisha usalama wa mama na mtoto.

Aliendelea kusema, Wanawake ambao wanajifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya katika Mkoa wa Tabora ni zaidi ya Asilimia 100%, huku kitaifa ikiwa ni asilimia 63, hivyo ametoa Wito kwa wanawake kuendelea kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya.

"Tumeona kwamba Wanawake ambao wanajifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya katika Mkoa wa Tabora ni zaidi ya 100%, wakati kitaifa tunazungumizia asilimia 63 kwahiyo hongereni sana kwa kupunguza vifo, kutoka wajawazito 99 mpaka 60" alisema.

Mwisho.

Jumatano, 18 Desemba 2019

NIMR MKOANI MBEYA YAFANIKIWA KUTAFITI KIPIMO CHA VVU KWA WATOTO WACHANGA

Mkurugenzi wa NIMR Mkoani Mbeya, Dkt. Nyanda Ntinginya akiongea na maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Wizara ya Afya na Taasisi zake ambao wametembelea nyanda za juu kusini katika kutekeleza kampeni ya “Tumeboresha Sekta ya Afya”.

Dkt. Nyanda akitoa maelezo kwa  Maafisa wa Wizara na Taasisi zake kuhusiana na moja za mashine za maabara zinazopatikana katika Maabara ya NIMR - Mbeya.

Mtaalam wa Maabara akiwa anatimiza majukumu yake katika Maabara ya NIMR mkoani Mbeya

Mtaalamu wa Maabara Abisai Kisinda akionesha mtungi wa Liquid Nitrogen Tank wa kuvuna Nitrogen kwa ajili ya kuhifadhia sampuli za utafiti ulioko kwenye maabara ya NIMR mkoani Mbeya.

Mtaalamu wa Maabara Bariki Mtafya akionesha mashine za Gene Xpert zinazotumika kupima sampuli za Kifua Kikuu zilizoko katika Maabara ya NIMR Mkoani Mbeya.


Baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Afya na Taasisi zake  wakiwa pamoja na Waandishi wa Habari walipotembelea Maabara ya NIMR Mkoani Mbeya.



Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu kanda ya nyanda za juu kusini (NIMR) imepiga hatua kubwa katika shughuli za utafiti inazofanya ikiwa ni pamoja na kuwa na vifaa vya kisasa vya maabara pamoja na watalaamu waliobobea.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa NIMR wa kanda hiyo Dkt. Nyanda Ntinginya wakati akiongea na maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Wizara ya Afya na Taasisi zake ambao wametembelea nyanda za juu kusini katika kutekeleza kampeni ya “Tumeboresha Sekta ya Afya” ili kuona mafanikio ya  sekta ya afya katika kipindi cha miaka mitano ya Rais John Magufuli akiwa madarakani.

Dkt. Nyanda amesema moja ya mafanikio makubwa ya NIMR ya kanda hiyo ni Utafiti wa vipimo vya awali vya Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa watoto wachanga waliozaliwa na akina mama wenye maambukizi.

Utafiti huo ujulikanao kwa jina la 'BABY' uliofanywa na Taasisi  hiyo unatumia kipimo cha “Early Infant Diagnosis (EID)” ambacho ufanyika kwa kutumia mashine za Gene Xpert.

Kwa mujibu wa Dkt. Nyanda amesema awali, upimaji wa kawaida ulikuwa unafanywa kwa watoto wachanga wenye wiki 4 hadi 6 na majibu yake yalikuwa yakichukua wiki mbili.

Dkt. Nyanda amesema utafiti huo uliofanyika Julai 2015 hadi Novemba 2016 kituo cha NIMR Mbeya kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Munich cha nchini Ujerumani ulilenga kutathimini vipimo vya awali vya VVU kwa watoto wachanga ambao wazazi wao wameathirika.

"Huu utafiti ulilenga kufanya tathmini ya vipimo vya awali vya VVU katika kituo cha kutolea huduma na vipimo vilifanywa na wauguzi tofauti na upimaji wa sasa ambao huhitaji wataalamu wa maabara na hivyo kuhitaji usafirishaji wa sampuli za damu kwenda maabara ya kanda au ya mkoa”. Amesema Dkt. Nyanda.

Matokeo ya utafiti yameonesha vipimo hivyo vilifanya vizuri kwa asilimia 100 na vinatoa majibu ndani ya masaa mawili tu na hivyo mgonjwa kupewa majibu yake siku hiyo hiyo ukilinganisha na upimaji wa kawaida ambapo huchukua wiki mbili au zaidi kupata majibu.

“Upimaji wa VVU wa awali kwa watoto wachanga umejumuishwa katika muongozo wa sasa wa utoaji wa huduma za VVU nchini,”alisema.

Hata hivyo, matokeo ya utafiti huo uliofanywa nchini Tanzania, Afrika ya kusini na Msumbiji yamepelekwa Shirika la Afya Duniani(WHO) kutoa miongozo ya upimaji wa VVU kwa watoto hao katika muongozo wa utoaji wa huduma za VVU wa mwaka 2016.

Maabara ya Taasisi ya Taifa ya utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ya Mkoani Mbeya imepata ithibati ya ubora wa kimataifa Maabara za utafiti ya nchini Marekani "College of American Pathologists" (CAP) kutokana na ubora wake wa kufanya tafiti ambapo ithibati hiyo imetolewa kwa nchi mbili tu katika ukanda wa Afrika Mashariki ikiwa ni Tanzania na Uganda.

WARATIBU WA MTUHA WATAKIWA KUIMARISHA UPATIKANAJI WA TAKWIMU SAHIHI

Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Saitore Laizer akiongea na waratibu wa  mfumo wa taarifa,na ufuatiliaji wa huduma za afya kutoka mikoa na halmashauri nchini.

Kaimu mkurugenzi msaidizi ufuatiliaji na tathimini kutoka wizara ya afya Tumainiel Macha  akiongea kwenye kikao kazi hicho.

Mwenyekiti wa waratibu hao Dkt. Ally Msoke akitoa neno la shukrani wakati wa ifunguzi wa mkutano huo.

 Waratibu hao wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani)  wakati wa ufunguzi wa kikao kazi hicho.kinachofanyika chuo cha mipango Dodoma.

Picha ya pamoja ya watumishi kutoka wizara ya afya na OR-TAMISEMI na mgeni rasmi.


WARATIBU WA MTUHA WATAKIWA KUIMARISHA UPATIKANAJI WA TAKWIMU SAHIHI

Na. Catherine Sungura, Dodoma

Waratibu wa Mfumo wa Taarifa za Utoaji wa Huduma za Afya (MTUHA) nchi wametakiwa kuimarisha upatikanaji wa takwimu sahihi za sekta ya afya  katika maeneo yao ya kazi.

Rai hiyo imetolewa leo na Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali ambaye pia ni mkurugenzi wa mafunzo na rasiliamali watu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Saitore Laizer wakati akifungua  kikao kazi cha waratibu MTUHA wa mikoa na halmashauri Tanzania kinachofanyika jijina hapa.

Dkt. Saitore amesema kuwa Wizara imeboresha mfumo wa takwimu kulingana na mahitaji  ya sasa na zinaingizwa na kuchanganuliwa kwa kutumia program maalum ya kompyuta katika ngazi ya wilaya ijulikanayo  kama ‘District health information software-DHIS 2’, hivyo ana imani  watasimamia na kuratibu kwa umakini.

“Matarajio ya wizara ni kuwa takwimu  zinazopatikana kutoka katika program hii zitakuwa sahihi  na mtatengeneza  orodha ya kielekroniki ya vituo vya kutolea huduma  za afya  ili kusaidia  katika mipango na kutoa maamuzi katika Sekta ya Afya”.

Vile vile Dkt. Saitore aliwataka waratibu hao kuweka mipango kabambe ili kuhakikisha mrejesho wa zoezi la uhakiki  wa ubora wa takwimu za afya  uliofanywa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali pamoja  na kutoa mafunzo ya mrejesho katika meza maalum zitakazoandaliwa ili kutoa msaada wa watumishi ambao wanahitaji kujifunza,kupata ufafanuzi au kuuliza na kupata majibu ya masuala ya MTUHA yanayowasumbua  katika maeneo ya kazi .

Hata hivyo aliwataka waratibu hao kuhakikisha  halmashauri zinatenga fedha kwa ajili ya  MTUHA katika mpango kabambe wa  halmashauri(CCHP) na timu za  za afya za mikoa na halmashauri na Wadau wa Maendeleo wanashiriki kikamilifu katika kuimarisha  upatikanaji wa takwimu sahihi za Sekta ya Afya.

Mfumo wa taarifa za utoaji wa huduma za afya nchini umesaidia kuwezesha sekta ya afya kupata takwimu sahihi na kwa wakati zinazowezesha kufanya maamuzi sahihi katika kupanga na kutekeleza malengo yake ili hatimaye kufikisha huduma bora kwa wananchi kutoka asilimia 43 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 85 mwaka 2019.

Jumanne, 17 Desemba 2019

KAYA ZENYE VYOO BORA ZIMEONGEZEKA KUFIKIA ASILIMIA 62.4 NCHINI

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, akisisitiza jambo katika kilele cha wiki ya usafi wa mazingira  kitaifa na mkutano wa maafisa afya wa mikoa,halmashauri  na wadau uliofanyika jijini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Musa Sima akitoa maelekezo kwa maafisa Afya katika kilele cha wiki ya usafi wa mazingira  kitaifa na mkutano wa maafisa afya wa mikoa,halmashauri  na wadau uliofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akiwasalimia Maafisa Afya, katika kilele cha wiki ya usafi wa mazingira  kitaifa na mkutano wa maafisa afya wa mikoa,halmashauri  na wadau uliofanyika jijini Dodoma.

Dkt. Ntuli Kapologwe akitoa salamu za Waziri wa OR TAMISEMI katika kilele cha wiki ya usafi wa mazingira  kitaifa na mkutano wa maafisa afya wa mikoa,halmashauri  na wadau uliofanyika jijini Dodoma.

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi akieleza jambo katika kilele cha wiki ya usafi wa mazingira  kitaifa na mkutano wa maafisa afya wa mikoa,halmashauri  na wadau uliofanyika jijini Dodoma.

Baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara ya Afya waliohudhuria katika kilele cha wiki ya usafi wa mazingira  kitaifa na mkutano wa maafisa afya wa mikoa,halmashauri  na wadau uliofanyika jijini Dodoma. 

Baadhi ya Maafisa Afya kutoka Mikoa,halmashauri  wakifuatilia kwa makini maagizo kutoka kwa mgeni rasmi, Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu (Hayupo kwenye picha).

Washindi wa Makala Televisheni ya Usafi wa Mazingira wanaotoka ITVwakipokea tuzo na zawadi kutokana na kuibuka namba moja.

Waandishi waliofanikiwa kushinda tuzo mbali mbali na zawadi kwa kuandaa makala na vipindi (Radio na Televisheni) kuhusu usafi wa mazingira wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa kutoka Wizara ya Afya na Wadau wa Mazingira.



KAYA ZENYE VYOO BORA ZIMEONGEZEKA KUFIKIA ASILIMIA 62.4 NCHINI

Na. Catherine Sungura,Dodoma

Kaya zenye vyoo bora nchini zimeongezeka hadi kufikia asilimia 62.4 mwaka 2019 kutoka asilimia 34 mwaka 2015 kupitia kampeni ya usichukulie poa, nyumba ni choo iliyoendeshwa kipindi cha miaka miwili na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katika kilele cha wiki ya usafi wa mazingira  kitaifa na mkutano wa maafisa afya wa mikoa,halmashauri  na wadau uliofanyika jijini hapa .

“Katika kipindi cha miaka miwili ya kampeni hii  kaya zenye vyoo bora zimeongezeka ,vile vile  kaya zisizokuwa na vyoo kabisa imepungua kutoka asilimia 7.5 hadi asilimia 1.9 katika kipindi hiki”Amesema Waziri Ummy.

Aidha, amesema  kwa upande wa wa vijiji ambavyo kaya zake zote zina vyoo imeongezeka kutoka 743 hadi 4,311 na kwa upande wa taasisi wameweza kuboresha  huduma ya maji na usafi wa mazingira katika vituo vya tiba  1,267 kati ya lengo  la vituo 1,000.

“Haya si mafanikio  ya kubeza na kimsingi ninapenda kuwashukuru wadau  kwa kushirikiana  na serikali kufanikisha kapeni hii,lengo letu ni kufuta kabisa  kaya zisizokuwa  na vyoo  na kuongeza kaya zenye vyoo boras hadi asilimia 75 ifikapo Juni,2021”.

Kwa upande wa maeneo ya kutupia taka ngumu,Waziri huyo amesema kuwa  Serikali ya awamu ya tano ina nia ya dhati ya kuboresha maeneo ya kutupia taka  hususan madampo yaliyopo kwenye miji ili yawe ya kisasa.

Hata hivyo amesema kuwa uchakuzi wa mazingira utokanao na taka ngumu umeendele kuwa changamoto  katika maeneo ya mijini,hivyo serikali imejipanga kuongeza nguvu kwenye mamlaka za serikali za mitaa ili kuboresha miundombinu iliyopo katika mitaa hapa nchini.

“Serikali pia imeandaa mwongozo wa uwekezaji  katika taka ngumu ili kuhamasisha  uwekezaji na kuongeza jitihada  za kuboresha usimamizi wa taka hapa nchini”.

Tafiti zinaonesha kwamba nchi inapoteza takribani  asilimia moja ya pato ghafi la taifa(GDP) kutokana na hali duni ya usafi na utafiti uliofanywa na benki ya dunia mwaka 2012 ulionesha kwamba kila mwaka shilingi bilioni 450 zinapotea kutokana na madhara ya uchafu.

#TunaboreshaAfya

SAMPULI 2589 ZAFANYIWA UCHUNGUZI KATIKA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

- Hakuna maoni



Meneja wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kanda ya nyanda za juu kusini, Gaspar Gerald akizungumza na waandishi wa habari walioambatana na Maofisa habari wa Wizara na taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Afya katika kampeni ya 'Tunaboresha sekta ya afya".


Baadhi ya Wakemia wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kanda ya Nyanda za juu kusini wakionesha namna vifaa vya maabara vinavyofanya kazi na baadhi ya sampuli wanazopata kwa ajili ya kufanyia uchunguzi.

MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali(GCLA) kanda ya nyanda za juu kusini, imekusanya sampuli mbalimbali 2589 na kuzifanyia uchunguzi na kutoka ushahidi mahakamani katika kesi 68.

Aidha, kati ya sampuli hizo 221 zilikuwa za Vinasaba(DNA) ambazo zililenga masuala kibinadamu ya utambuzi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja wa kanda hiyo, Gaspar Gerald alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari walioambatana na Maofisa habari wa taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Afya katika kampeni ya 'Tunaboresha sekta ya afya' inayolenga kuangalia mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.

Meneja huyo  sampuli hizo 2580 ni za kimazingira,makosa ya jinai,  vinasaba na chakula na dawa ndio zinazopokelewa.

Aidha alisema  kanda hiyo kwa kipindi cha miaka minne wametoa ushahidi kwenye kesi 68 na kwamba sio kila sampuli zinazopimwa zinatolewa ushahidi bali ni zile zinazohitajika kutolewa ushahidi mahakamani.

"Huu ushahidi ni pale mahakama inapohitaji ushahidi ndo tunaenda kutoa na ushahidi tunaotoa ni kile tulichokiona kwenye sampuli iliyoletwa kama vile dawa za kulevya hivyo mkemia anatoa ripoti yake,"alisema

Akizungumzia kuhusu mafanikio mengine, Gerald alisema wamefanikiwa kujenga ofisi yao kwa gharama ya Sh.Milioni 300, kukagua na kudhibiti kemikali, kuongezeka wafanyakazi kutoka watatu hadi 18 na kufanikiwa kupima  sampuli 2580.

"Mwaka 2017 wafanyakazi waliongezeka kwa asilimia 80 na inatokana na juhudi za Rais Magufuli kuhakikisha anatekeleza sera ya serikali ya kufikisha huduma kwa wananchi, kanda hii kijiografia ina mikoa sita lakini kiutawala kwa mujibu wa mkemia wa serikali ni mikoa mitano Njombe, Songwe, Mbeya, Katavi na Rukwa,"alisema

Alisema huduma zinazotolewa ni pamoja na uchunguzi wa kimaabara, utekelezaji wa sheria za mamlaka ikiwemo ya kemikali za majumbani na viwandani, Vinasaba vya binadamu na sheria ya Mkemia Mkuu.

Alieleza ofisi hiyo imefanikiwa kusimamia kemikali na kudhibiti zinazoingia mipakani kwenye  mpaka wa Tunduma na Kasumulu na kutoa elimu kwa watu zaidi ya 150 wanaojihusisha na kemikali na watu 140 wanaotoka jeshi la polisi kwa ajili ya usimamizi wa sampuli za jinai.

Kadhalika, Gerald alisema udhibiti wa kemikali awali hakuwa mzuri lakini baada ya mamlaka hiyo kuanzishwa udhibiti umekuwa mkubwa na wasafirishaji wamepewa elimu ili kufuata taratibu za kulinda mazingira na afya za watu.

Kuhusu DNA, Meneja huyo alisema vinasaba vinapimwa kwa maana mbili ya utambuzi na masuala ya jamii au ya ndoa.

"Kwenye sheria ya DNA imeanisha mamlaka inayoomba kupimiwa DNA, ile mamlaka ndio zinazoleta maombi kwa mkemia kuomba kupimiwa DNA, hakuna uoga watu wanafuata taratibu, kwenye suala la utambuzi kwa mfano tukio la moto Morogoro pale mkemia aliingia kujua huyu ni nani,"alisema.

Alisema mpaka sasa sampuli 221 za DNA kwa kipindi cha miaka minne na mamlaka zingine zilizowasilisha maombi ya kupimiwa kwa Mkemia ndio zenye majibu ya vinasaba hivyo.

Mwisho.

Jumatatu, 16 Desemba 2019

MAOFISA AFYA WATAKIWA KUWAKINGA WANANCHI DHIDI YA MAGONJWA-DKT. SUBI

Mkurugenzi wa Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi akieleza jambo mbele ya Maafisa Afya wa Mikoa na Halmashauri, wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya usafi wa mazingira.

Afisa kutoka Idara ya Mazingira Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto Bw. Anyitike Mwakitalima akieleza mafanikio mbali mbali yaliyopatikana kutokana na afua mbali mbali za usafi wa mazingira zinazotekelezwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wadau.

Maafisa Afya kutoka Mikoa, Halmashauri na Wadau wakifuatilia kwa makini neno kutoka kwa Mkurugenzi wa Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi.


MAOFISA AFYA WATAKIWA KUWAKINGA WANANCHI DHIDI YA MAGONJWA-DKT. SUBI

Na Catherine Sungura, WAMJW - Dodoma

Maofisa afya wa mikoa na halmashauri wametakiwa kusimamia afya ya jamii kwenye maeneo yao ili wananchi wajikinge dhidi ya magonjwa yakuambukiza na yele yasiyoambukiza.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa kinga Dkt. Leonard Subi wakati akiongea na maofisa hao ambao wanakutana jijini hapa  kwa  kikao kazi cha siku tatu wakijadili utekelezaji wa maazimio yaliyotolewa kwenye mkutano mkuu wa kwanza mwaka jana  na  Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.

“Mkutano huu ni wa pili mwaka huu,ni mkutano muhimu kwa maofisa afya kwani ndio wasimamizi wa shughuli za afya katika ngazi za jamii kwa kuhakikisha wananchi wanajikinga na maradhi, kula chakula bora kuishi makazi bora,usafi wa mazingira pamoja na kuwa vyoo bora”.Amesema Dkt. Subi

Aidha, amesema katika mkutano huu mambo mbali mbali yatajadiliwa ikiwemo  afya mazingira,usafi na uchafuzi wa mazingira na kila kinachotumiwa na kumzunguka  mwananchi ,pia wataangalia mabadiliko ya tabia nchi na kupata taarifa kutoka ngazi za mikoa ni jinsi gani walivyotekeleza majukumu yao.

“Maafisa afya muendelee kuishauri wizara kwa kutumia takwimu kwani tunatarajia mkutano huu mtabadilishana uzoefu  kutoka sehemu zenu za kazi,kama wizara tumekua tukitengeneza sera na miongozo mbali mbali ya kudhibiti maradhi yote yanayoweza kuathiri afya za binadamu hivyo kazi ya wizara ni kukusanya taarifa,kuchakata na kuzitolea miongozo na maelekezo”. Aliongeza Dkt. Subi.

Hata hivyo amesema maofisa hao wana majukumu ya kusimamia na  kulinda afya mipakani ili kusiingie magonjwa ya milipuko kutoka nje hususan  nchi za jirani pamoja na utoaji wa chanjo ambapo Tanzania ipo vizuri.

Mkutano huo ambao utafunguliwa kesho na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu umebeba Kauli mbiu isemayo “Huduma bora za afya mazingira na usafi ni kichocheo muhimu cha uchumi endelevu.