Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 11 Desemba 2019

SAMPULI 5106 ZIMEFANYIWA UCHUNGUZI NA MAABARA YA MKEMIA KANDA YA KATI
Picha mbalimbali zikionesha Meneja wa mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kanda ya kati Bw. Musa Kuzumila akizungumza na Maafisa Mahusiano na Mawasilino wa Wizara ya Afya na Taasisi zake wakati walipotembelea mamlaka hiyo kujionea mafanikio yaliyofanywa katika kuboresha sekta ya afya nchini chini ya kipindi cha miaka minne ya Rais Magufuli akiwa madarakani.

Dodoma

Jumla ya sampuli 5106 zimefanyiwa uchunguzi katika maabara zikiwemo za masuala ya kijamii na kijinai katika mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali kanda ya kati.

Hayo yamesemwa na Meneja wa mamlaka hiyo kanda ya kati Musa Kuzumila wakati wa ziara ya maofisa habari wa wizara ya afya na taasisi zake wakati wa kutembelea mamlaka hiyo kujionea mafanikio yaliyofanywa katika kuboresha sekta ya afya nchini.

Kazumila amesema kwamba tangu kuanzishwa kwa kanda hiyo miaka miwili na nusu sasa ,kanda yake imefanikiwa kupima sampuli hizo ambazo zimefanyiwa uchunguzi katika maabara na kuzitolea ushahidi mahakamani

"Mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu inasimamia sheria na kudhibiti kemikali hivyo tumeweza kufanyia uchunguzi sampuli na hivyo kupunguzia wateja  umbali na hivyo kusaidia wananchi kupata haki na kutoa ushahidi kwa wakati".Amesema Kazumila.

Kwa upande wa vinasaba Kazumila amesema kati ya sampuli walizopokea jumla ya sampuli 36 zilizowasilishwa asilimia 90 zilikua zinaangalia uhalali wa baba wa mtoto.

Hata hivyo amesema kwamba mamlaka hiyo imeweza kukagua maeneo yanayojihusisha na kemikali zipatazo 360 pamoj na kutoa vibali 139 za kuingiza na kusafirisha kemikali nchini kwa kanda ya kati.

Kwa upande wa wajasiriamali wadogo wadogo mamlaka hiyo imewapatia mafunzo wajasiriamali 315 namna ya matumizi salama ya kemikali pamoja na kutoa elimu kwa wachenjuaji wa dhahabu wanaotumia kemikali aina ya sodium cyanide.

Mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali kanda ya kati inahudumia mikoa ya morogoro,iringa,dodoma,singida na tabora na ilianzishwa mwaka 2017.


-Mwisho-

0 on: "SAMPULI 5106 ZIMEFANYIWA UCHUNGUZI NA MAABARA YA MKEMIA KANDA YA KATI"