Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 24 Februari 2020

VIFO VYA WANAWAKE WAJAWAZITO VYAPUNGUA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA TEMEKE



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiangalia kifaa cha uchunguzi kwenye idara ya meno    ambapo hivi sasa hospitali ya rufaa ya mkoa temeke wanatoa huduma za kibingwa za huduma ya meno.
Waziri Ummy Mwalimu akiwajulia hali wagonjwa waliofika hospitalini hapo

Waziri Ummy Mwalimu akiwajulia hali akina mama wajawazito waliolazwa kwenye wodi ya uzazi hospitalini hapo


Jengo la huduma za dharura lililofanyiwa ukarabati


Na. Catherine Sungura - Dar es Salaam 
 
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa temeke imejipanga kuokoa maisha ya wakina mama, wajawazito hususan katika kipindi cha kujifungua, kutimiza lengo hilo imeboresha miundombinu yake, vifaa tiba pamoja na kuimarisha huduma za afya kwenye ngazi za msingi.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, wakati wa ziara yake ya kikazi hospitalini hapo, ambako alikwenda kwa lengo la kusikiliza maoni na changamoto kutoka kwa wananchi na watumishi wa hospitali hiyo.

“Mwaka 2018 walikuwa na vifo 19 vya wajawazito na 2019 walikuwa na vifo 8 tu, lakini kwa takwimu za kuanzia Novemba 2019 hadi leo hakuna mwanamke mjamzito aliyekuja hospitalini hapa na kupoteza maisha, niwapongeze madaktari, wauguzi na watoa huduma wote wa hapa kwa hatua hii," amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa jitihada za makusudi, kuwekeza kwenye huduma za afya nchini sambamba na ujenzi wa vituo vya afya na ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa.

“Sasa hivi hapa temeke kuna huduma za kibingwa za meno ambapo zamani haikuwepo," amesema.

Waziri Ummy amesisitiza Wizara ina mpango pia wa kuhakikisha huduma zote za kibingwa zinazohitajika zinakuwepo kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa.

Hata hivyo amesema kuwa wanawake 15 kati ya wanawake 100 ndio ambao huhitaji kupelekwa kujifungulia kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa hususan wale wenye changamoto za ujauzito, kwa mfano mtoto amekaa vibaya au viashiria vya uzazi pingamizi.

Kwa upande  wa vipimo waziri huyo amesema kuwa Wizara yake imeongeza vipimo vya utra sound hivi sasa serikali imeboresha vituo vya afya na kwamba vipimo hivyo vinaanza kutolewa kuanzia ngazi za vituo vya afya vya umma na hospitali za wilaya nchini.

Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma kuanzia ngazi ya msingi na hospitali za rufaa za mikoa ni kwa wagonjwa watakaopata rufaa.

“Kwa yeyeote atakayefanya makusudi kukorofisha vipimo ili watu waende kupima kwenye vutuo binafsi tutawachukulia hatua kwani ni wahujumu uchumi, tunataka vipimo vyote vifanyike ndani ya hospitali ila pale mashine haipo tutaruhusu, lengo letu ni kujitosheleza kwa vipimo vyote kwenye vituo vya afya vya umma," amesisitiza Waziri Ummy.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Yudas Ndungile amesema kuwa kutokana na maboresho ya miundombinu, wataalam na vifaa tiba kwa mkoa huu wameweza kupunguza vifo vipatavyo arobaini kwa mwaka ukilinganisha na vifo186 mwaka 2018 hadi vifo 140 mwaka 2019 na matarajio yao ni kupunguza zaidi.

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke Dkt. Meshack Shimwela amesema kuwa  hospitali hiyo imeondoa msongamano wa wajawazito kwa kuwa hivi sasa wananchi wengi wanafuata mfumo wa rufaa.

"Hivyo wakina mama wajawazito wanaofika kwenye hospitali hii ni wale wenye changamoto ya uzazi kwa maana hiyo wengi wanajifungulia kwenye ngazi za chini ambapo huduma za afya nazo zimeboreshwa," amesema.

MWISHO

13 on: "VIFO VYA WANAWAKE WAJAWAZITO VYAPUNGUA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA TEMEKE"
  1. Characters, weapons, vehicles, robots, and even entire sceneries can be created using the game's extensive in-game tools. Feel like doing melon playground something crazy? Try it out. Is detonation your desired outcome? Even better.

    JibuFuta
  2. With its cartoon-style characters and smooth gameplay, Football Bros IO offers a fun, stress-free football experience that anyone can enjoy.

    JibuFuta
  3. Learn Each Track: There are different challenges in each level. You can learn challenging passages, ramps, and potential shortcuts by repeating Snow Rider 3D tracks. By predicting turns and jumps, skilled players can cut seconds off their best times.

    JibuFuta
  4. The Football bros gameplay loop is extremely tight:

    Start match (instant load)
    Control single player
    Attack / defend rapidly
    Use power-ups
    Score → repeat

    JibuFuta
  5. Football Bros is a fun and fast-paced game with smooth controls and exciting gameplay!

    JibuFuta
  6. For players who enjoy quick browser games and anime fighting games, BVNPlay offers a great archive of playable Bleach vs Naruto versions with complete controls and version guides.

    JibuFuta
  7. Habari nzuri sana kuhusu huduma za afya na maendeleo ya hospitalini. Kazi nzuri sana kwa wizara na watoa huduma wote. Tembelea Class of '09 Online kwa maelezo zaidi na burudani.

    JibuFuta
  8. Makala hii inatoa taarifa nzuri sana kuhusu huduma za afya na jamii. Pia kwa wanaopenda ubunifu wa kidijitali na michezo ya kujifunzia, tembelea スクラッチマイクラ ujionee.

    JibuFuta
  9. Taarifa nzuri sana kuhusu huduma za afya na maendeleo ya hospitalini. Kazi nzuri sana kwa wizara na watoa huduma wote. Tembelea Pixel Dungeon Online kwa maelezo zaidi kuhusu mchezo huu wa kuburudisha.

    JibuFuta
  10. Great informative article. For those who enjoy psychological horror visual novels with dialogue choices and multiple endings, check out Nate Hand Gesture online.

    JibuFuta
  11. Makala hii inasisitiza umuhimu wa kuokoa maisha ya akina mama. Mazoezi laini yanaweza kusaidia usawa na nguvu ya kila siku; nimeona mwongozo wa Taichi Walking kuhusu kutembea kwa utulivu.

    JibuFuta
  12. Makala hii inasisitiza umuhimu wa kujiandaa na kujifunza kabla ya hatua muhimu. Ninaona rasilimali kama G1 Practice pia inasaidia mazoezi ya usalama.

    JibuFuta
  13. Makala hii inakumbusha umuhimu wa kuboresha huduma za uzazi hospitalini. Kwa burudani ya kivinjari bila kupakua, tembelea Geometry Dash JP ujionee.

    JibuFuta