Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 7 Februari 2018

SERIKALI YAAZIMIA KUKUSANYA TAKWIMU ZA AFYA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akitoa taarifa mbele ya Wadau wa Sekta ya Afya wakati wa Kikao cha kusaini makubaliano ya Mfumo wa Ukusanyaji wa takwimu takwimu wa kielektroniki kilichofanyika mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.

Wadau wa Sekta ya Afya wakifuatilia kwa makini  taarifa ya mgeni rasmi (Hayupo kwenye picha) ambae ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa Kikao cha kusaini makubaliano ya Mfumo wa Ukusanyaji wa takwimu takwimu wa kielektroniki.

Mwinyekiti wa DPG HEALTH Mhe. Norzin Grigoleit-Dagyab akitutubia mbele ya Wadau wa Sekta ya Afya na Watumishi wa Serikali wa Idara kuu ya Afya wakati wa Kikao cha kusaini makubaliano ya Mfumo wa Ukusanyaji wa takwimu takwimu wa kielektroniki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya na wa mwisho kulia ni Mwakilishi kutoka WHO Dkt. Matthieu Kamwa.

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiwa na Wadau mbali mbali wa Sekta ya Afya katika Kikao cha kusaini makubaliano ya Mfumo wa Ukusanyaji wa takwimu wa kielektroniki kilichofanyika mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.

Picha ya Pamoja ya Viongozi wa Sekta ya Afya wakiwa wameshika mikataba iliyosainiwa ya makubaliano ya Mfumo wa Ukusanyaji wa takwimu wa kielektroniki ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.


Na WAMJW-DAR ES SALAAM.
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imeazimia kukusanya na kutumia takwimu kwa njia ya kielektroniki nchi nzima ili kuweza kumudu na kutoa huduma za afya kwa ubora zaidi nchini.
Hayo yamezungumzwa na Katibu Mkuu Wizara ya afya Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa kutia Sahihi ya makubaliano ya kuanzisha mfumo wa ukusanyaji takwimu za afya utakaotekelezwa na Wizara ya afya,Wadau wa Maendeleo,Asasi za Kiraia na Shirika la Afya Duniani (WHO) uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
“Takwimu ni muhimu sana amabazo zitazomuwezesha mtoa huduma kujua mgonjwa historia yake ya ugonjwa  na matibabu aliyopewa awali,kuwapa Uwezo utumishi kujua tunahitaji rasilimali watu kwa kiasi gani  katika kituo cha Afya” alisema Dkt. Ulisubsya.
Aidha, Dkt. Ulisubisya amesema kuwa kwa kuanzia zoezi hilo litaanza kwenye mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Manyara hatimaye kufikia nchi nzima mpaka kufika 2020 ili kuweza kuwa  na takwimu za afya.
Dkt. Ulisubisya amesema kuwa mfumo wa kujaza takwimu kwenye makaratasi umepitwa na wakati kwani kadri makaratasi ya takwimu yanapokuwa mengi na makosa ya utoaji huduma unaweza kutokea  kwani mpaka uanze kutafuta takwimu zilizopita inachukua muda mrefu tofauti na kuhifadhi takwimu kielektroniki.
Mbali na hayo Dkt. Ulisubisya amesema kuwa mpaka hivi sasa hali ya utoaji wa chanjo imefikia asilimia 97 na lengo letu ni kufikia asilimia 100 kupitia mfumo huu wa kukusanya takwimu kwa njia ya kielektroniki.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Matthieu Kamwa amesema kuwa wapo  tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya katika kutekeleza hilo ili kuweza kuboresha mifumo ya afya nchini.
“Unajua Takwimu ni utajiri hasa katika kutekeleza shughuli za kutoa huduma za afya kwa wananchi hivypo hatuna budi kuunga mkono juhudu za Serikali ya Tanzania katika kufanikisha hili jambo kwani litaturahisishia hata sisi katika kutoa miongozo ya afya” alisema Dkt. Kamwa.

0 on: "SERIKALI YAAZIMIA KUKUSANYA TAKWIMU ZA AFYA KIELEKTRONIKI NCHI NZIMA."