Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 28 Februari 2018

SERIKALI YATARAJIA KUWA NA WATOA HUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII ZAIDI YA ...




SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatarajia kuwa na watoa huduma wa Afya ngazi ya jamii (CHWz) Zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka 2020 katika vijiji Zaidi ya 15,000 nchini.
Hayo yamesemwa leo na  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu  katika Mkutano wa Wadau wa Afya, mashirika yasiyo Yakiserikali, na Serikali katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.
“Tunataka itakapofika mwaka 2020, tuwe na angalau Wahudumu wa Afya zaidi ya 30,000 katika vijiji Zaidi ya 15,000 tulivyonavyo Tanzania, Eneo hili tumeliona ni eneo muhimu kwasababu tutapata matokeo ya haraka, ni bora kutumia Bilioni 40 kwa ajili ya kinga ya magonjwa kwa Watanzania .” Alisema Mhe. Ummy Mwalimu.
Mhe. Ummy alisema kuwa lengo la Mkutano huo ni kujadiliana na Wadau wa Maendeleo na Mashirika yasiyo Yakiserikali juu ya kuimarisha huduma ya Afya ya msingi hasa katika kuwakinga wananchi dhidi ya maradhi kupitia mikakati ambayo inakubalika kimataifa ya kuwa na watoa huduma katika ngazi ya jamii.

SERIKALI YATARAJIA KUWA NA WATOA HUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII ZAIDI YA 30,000

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akielezea jambo mbele ya Wadau wa Afya, mashirika yasiyo Yakiserikali, na Serikali katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.

Afisa kutoka kitengo cha Elimu ya Afya kwa umma Wizara wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Amalbega Kasangala akiwasilisha taarifa mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu(hayupo kwenye picha).

Wadau wa Afya, mashirika yasiyo Yakiserikali, Watumishi wa Serikali na Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa kutoka kwa mgeni rasmi Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu(hayupo kwenye picha), katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.



Na WAMJW. Dar es salaam.
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatarajia kuwa na watoa huduma wa Afya ngazi ya jamii (CHWz) Zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka 2020 katika vijiji Zaidi ya 15,000 nchini.
Hayo yamesemwa leo na  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu  katika Mkutano wa Wadau wa Afya, mashirika yasiyo Yakiserikali, na Serikali katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.
“Tunataka itakapofika mwaka 2020, tuwe na angalau Wahudumu wa Afya zaidi ya 30,000 katika vijiji Zaidi ya 15,000 tulivyonavyo Tanzania, Eneo hili tumeliona ni eneo muhimu kwasababu tutapata matokeo ya haraka, ni bora kutumia Bilioni 40 kwa ajili ya kinga ya magonjwa kwa Watanzania .” Alisema Mhe. Ummy Mwalimu.
Mhe. Ummy alisema kuwa lengo la Mkutano huo ni kujadiliana na Wadau wa Maendeleo na Mashirika yasiyo Yakiserikali juu ya kuimarisha huduma ya Afya ya msingi hasa katika kuwakinga wananchi dhidi ya maradhi kupitia mikakati ambayo inakubalika kimataifa ya kuwa na watoa huduma katika ngazi ya jamii.
“Kisera tumesema kuwa tunataka kuwa na watu wawili ambao watakuwa wanafanya kazi kama watoa huduma za Afya na kazi yao kubwa haitakuwa kutibu bali itakuwa ni kusisitiza masuala ya lishe, masuala ya uzazi wa mpango, kuhimiza watu kujua hali zao hasa katika maambukizi ya VVU na kuwaelekeza waende maeneo gani ili kupata huduma za Afya” alisema Mhe. Ummy
Kwa upande mwingine Mhe. Ummy Mwalimu aliwashukuru wadau wa maendeleo na Mashirika yasiyo Yakiserikali kwa kuwa tayari kushirikiana na Serikali katika kufanikisha kuwa na watoa huduma za Afya ngazi ya jamii kwa idadi yakuridhisha ifikapo 2020.
Hata hivyo Waziri Ummy alisema kuwa rasilimali watu katika Sekta ya Afya nchini ni Asilimia 51, huku kukiwa na upungufu wa watoa huduma za Afya kwa Asilimia 49, ambao ni pamoja na Madaktari, Wauguzi, Wataalamu wa Maabara, huku mikoa ambayo inaupungufu Zaidi ni Katavi, Rukwa, Tabora, Kigoma na Kagera.
Naye, Afisa kutoka kitengo cha Elimu ya Afya kwa umma Wizara wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Amalbega Kasangala alisema Serikali kuwa Serikali imejipanga katika kukinga ugonjwa kuliko kutibu jambo ambalo litasaidia katika kupunguza gharama kwa wananchi.

Jumanne, 27 Februari 2018

TANZANIA KUONDOA TATIZO LA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI KWA WANAWAKE



SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imedhamiria kupambana na Saratani ya mlango wa kizazi nchini kwa kuwapa kinga wasichana kuanzia umri wa miaka 9 mpaka 14 ili kuondoa tatizo hilo nchini.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) mapema leo wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.

“Katika kukabiliana na ugonjwa wa Saratani, kuimarisha afya ya wanawake Tanzania pamoja na kupunguza vifo vitokanavyo na Saratani , Wizara ya Afya itaanza kutoa chanjo ya kuwakinga wasichana dhidi ya Saratani ya mlango wa kizazi mwaka huu”. Alisema Mhe. Ummy Mwalimu.

TANZANIA KUONDOA TATIZO LA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI KWA WANAWAKE

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo mbele ya Wadau wa Afya na waandishi wa habari wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.


Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi akimkaribisha mgeni rasmi Mh. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha) wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi.


Meneja mpango wa Taifa wa Chanjo Wizara ya Afya Dkt. Dafrossa Lyimo akiwasilisha taarifa mbele ya Mgeni rasmi (hayupo kwenye picha) wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi.


Mwakilishi wa WHO Dkt. Ritha Njau akiwasilisha salamu za WHO wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Bakari Kambi.

Wadau wa Afya na Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa kutoka kwa Mgeni rasmi (hayupo kwenye picha) wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB)  wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.


Na WAMJW - Dar es salaam.

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imedhamiria kupambana na Saratani ya mlango wa kizazi nchini kwa kuwapa kinga wasichana kuanzia umri wa miaka 9 mpaka 14 ili kuondoa tatizo hilo nchini.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) mapema leo wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.

“Katika kukabiliana na ugonjwa wa Saratani, kuimarisha afya ya wanawake Tanzania pamoja na kupunguza vifo vitokanavyo na Saratani , Wizara ya Afya itaanza kutoa chanjo ya kuwakinga wasichana dhidi ya Saratani ya mlango wa kizazi mwaka huu”. Alisema Mhe. Ummy Mwalimu.

Hata hivyo alisema hivi sasa hakuna takwimu za kitaifa ila kwa  takwimu toka vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na  taasisi ya Saratani ya Ocean Road,"kwa mwaka 2016/2017 saratani ya shingo ya kizazi ni  Asilimia 32.8 huku ikifuatiwa na saratani ya matiti kwa asilimia 12.9"

Alisema kati ya wagonjwa 100, wagonjwa 46 ni wa Saratani ya mlango wa kizazi na Saratani ya Matiti na vifo vitokanavyo na saratani kwa akina mama ni asilimia 50 ambapo chanzo ni saratani ya shingo ya kizazi na matiti.

Aidha,Waziri Ummy alisema Serikali imepanga kuanza kuwapatia chanjo hiyo wasichana wenye umri wa miaka 14 kama umri wa chini na jumla ya wasichana 616,734 watapatiwa chanjo hiyo.
Aidha,Waziri Ummy ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwapeleka mabinti wao kwenye chanjo hivyo kwani ni salama na itatolewa kwenye vituo vyote vya afya vya Serikali vipatavyo 7,000,mashuleni pamoja na huduma za afya za vikoba bila malipo.
Naye Meneja wa Mpango wa Taifa wa Chanjo Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Dafrossa Lyimo  amewatoa hofu wananchi na kusisitiza juu ya umuhimu wa kinga kuliko tiba na kusema kuwa chanjo hiyo ni salama na imethibitishwa na shirika la Afya Duniani (WHO)na itatolewa na wahudumu wa afya waliopata mafunzo.

Jumatatu, 26 Februari 2018

TANZANIAI YAPOKEA TUZO YA KUPAMBANA NA UGONJWA WA MALARIA KUTOKA SHIRIKA ...






SERIKALI ya Jamhuri wa Muungano Tanzania imepata tuzo kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kutambua mchango mkubwa uliofanywa katika jitihada ya kudhibiti Ugonjwa wa Malaria nchini.
Akikabidhiwa Tuzo hiyo wakati wa mkutano wa siku mbili ulioanza leo wa kujadili mafanikio na changamoto katika kudhibiti Malaria,Mganga Mkuu wa Serikali  Profesa Muhammad Bakari Kambi alisema tuzo hiyo imetolewa kwa Serikali na Watanzania kwa ujumla na Shirika hilo  kanda ya Tanzania

TANZANIA YAPOKEA TUZO YA KUPAMBANA NA UGONJWA WA MALARIA KUTOKA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO)

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammed Bakari Kambi akipokea cheti cha kutambua mchango mkubwa uliofanywa na Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Malaria kutoka mwakilishi wa WHO Dkt. Ritha Njau tukio lililofanyika mapema leo Serena jijini Dar es salaam.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammed Bakari Kambi akiongea na wadau wa Afya na waandishi wa habari katika kikao cha kupokea cheti cha kutambua mchango mkubwa uliofanywa na Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Malaria.

Meneja wa Mpango wa Kupambana na Kudhibiti Malaria nchini Dkt. Ally Mohamed akiwasilisha taarifa mbele ya wadau na waandishi wa Habari katika kikao cha kupokea cheti cha kutambua mchango mkubwa uliofanywa na Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Malaria kutoka mwakilishi wa WHO Dkt. Ritha Njau tukio lililofanyika mapema leo Serena jijini Dar es salaam.

Mwakilishi wa WHO Dkt. Ritha Njau akijiandaa kumkabidhi cheti Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammed Bakari Kambi

Wadau wa Afya wakifuatilia kwa umakini taarifa ilokuwa ikiwasilishwa na Meneja wa Mpango wa Kupambana na Kudhibiti Malaria nchini Dkt.  Ally Mohamed (hayupo kwenye picha)wakati wa kikao cha kupokea cheti cha kutambua mchango mkubwa uliofanywa na Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Malaria.


Na WAMJW-Dar es salaam.
SERIKALI ya Jamhuri wa Muungano Tanzania imepata tuzo kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kutambua mchango mkubwa uliofanywa katika jitihada ya kudhibiti Ugonjwa wa Malaria nchini.
Akikabidhiwa Tuzo hiyo wakati wa mkutano wa siku mbili ulioanza leo wa kujadili mafanikio na changamoto katika kudhibiti Malaria,Mganga Mkuu wa Serikali  Profesa Muhammad Bakari Kambi alisema tuzo hiyo imetolewa kwa Serikali na Watanzania kwa ujumla na Shirika hilo  kanda ya Tanzania
Prof.Kambi alisema tuzo hiyo imetolewa kwa kuanisha mchango mkubwa uliofanywa na  Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuweka Mikakati,Rasilimali fedha na kufanya kazi kwa ukaribu na wahisani mbalimbali katika kupambana na Malaria
Prof. Kambi aliendelea kusema kuwa ushiriki wa Tanzania katika tafiti mbalimbali ambazo zimechangia katika udhibiti wa Malaria ikiwemo utafiti wa kutumia vyandarua vyene viuatirifu vya kuzuia mbu pamoja na  tafiti za awali za chanjo za kudhibiti Malaria.
“Mafanikio mengine ni  upungufu wa Ugonjwa wa Malaria kutoka wagonjwa milioni 18 kwa mwaka 2008 hadi wagonjwa milioni 5.5 kwa mwaka 2017.Pia Malaria imekua chanzo kikubwa cha vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano hivyo kumekua na upungufu kutoka vifo 112 kati ya watoto 1,000 mwaka 2005 hadi vifo  79 kati ya watoto 1,000 mwaka 2016”.Alisema
Aidha, kipengele kingine katika vita dhidi ya udhibiti wa ugonjwa wa Malaria ni kwamba, Tanzania ndio nchi pekee Barani Afrika kuwa na kiwanda kinachotengeneza vyandarua vyenye dawa ya kudhibiti mbu aenezaye Malaria.
Naye,Kaimu Mwakilishi Mkazi wa WHO, Dkt. Ritha Njau amesema tuzo hiyo imetolewa kwa Tanzania baada ya kufanikiwa kupunguza maambukizi ya Malaria kwa kipindi cha miaka 10, hivyo WHO imeona ni vema kutoa tuzo hiyo ikiwa ni katika kutambua mafanikio hayo.
Wakati huo huo,Meneja Mpango wa Kudhibiti Malaria Nchini Dkt. Ally Mohammed alisema hali ya maambukizi ya Malaria nchini hivi sasa imepungua na kufika asilimia 7.3 ambapo lengo ni kutokomeza malaria nchini.
Dkt. Ally Mohammed Alitaja mikoa ya Kigoma, Geita na Kagera hali ya malaria bado ipo juu, hivyo mkutano huo utaweza kujibu maswali kwanini mikoa hiyo maambukizi ya malaria bado juu na kitu gani kifanyike ili kuweza kutokomeza ugonjwa huo.

Ijumaa, 23 Februari 2018

SERIKALI YAPANGA KUSITISHA UTOAJI HUDUMA YA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA K...

- Hakuna maoni














SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepanga kusitisha shughuli za utoaji wa huduma zinazofanywa na waganga wa tiba asili na tiba mbadala pindi muda wa kujisajili utakapokuwa umwekwisha.
Amebainisha hayo Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa tiba asili na tiba mbadala kutoka Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Poul Mhame mapema leo pindi alipoongea na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
“waganga wa Tiba asili na Tiba mbadala na vituo vyao watalazimika kusitisha utoaji huduma wanazotoa pindi muda wa usajili cha itafika mwisho” Alisema Dkt. Mhame

SERIKALI YAPANGA KUSITISHA UTOAJI HUDUMA YA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA KWA WAGANGA WASIOJISAJILI

- Hakuna maoni
Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa tiba asili na tiba mbadala kutoka Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Poul Mhame akiongea na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya leo jijini Dar es salaam.




Na WAMJW. Dar es salaam.
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepanga kusitisha shughuli za utoaji wa huduma zinazofanywa na waganga wa tiba asili na tiba mbadala pindi muda wa kujisajili utakapokuwa umwekwisha.
Amebainisha hayo Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa tiba asili na tiba mbadala kutoka Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Poul Mhame mapema leo pindi alipoongea na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
“Waganga wa Tiba asili na Tiba mbadala na vituo vyao watalazimika kusitisha utoaji huduma wanazotoa pindi muda wa usajili cha itafika mwisho” Alisema Dkt. Mhame
Dkt. Mhame aliendelea kusema kuwa Serikali ilianza usajili wa Waganga wa Tiba asili takribani miaka saba ilopita na mpaka sasa ni waganga 16,300 tu ndio waliofanikiwa kujisajili huku mchakato huo ukiendelea mpaka sasa.
Dkt. Mhame alielezea kusikitishwa sana na idadi ndogo ya Waganga wa tiba asilia kujisajili inayoendelea kwa maeneo ya mjini hususania katika Manispaa, Miji, na Halmashauri, ikilinganishwa na maeneo ya vijijini ambao wanaonekana kwenda kwa kasi sana,
“Ni Dhahiri kuwa taarifa hizi, hazijawafikia wengi hususani waliopo vijijini kutokana na vyombo vya habari vilivyopo kule, lakini wengi waliopo mijini hawana sababu zakusema hawajui” Alisema Dkt. Mhame.
Aidha, Dkt, Mhame amewashauri Wanganga wa Tiba asili kutumia fursa hii kwa muda uliobaki kwa kwenda ofisi za Waganga wa Halmashauri zao kujaza fomu na kuziwasilisha ili waweze kujisajili na kuondokana na usumbufu huo.
“Itakuwa si busara kwa mganga alipo Dar es salaam akakutwa hajajisajili kwa kipindi chote cha miaka saba, asilalamike kwamba hana taarifa” Alisema Dkt Mhame.
Kwa upande mwingine Dkt. Mhame aliwataka wanaojihusisha na uzalishaji wa Dawa kusajili dawa hizo huku akiwahasa wataalamu mbali mbali kama vile Madaktari, Wafamasia, Wakemia, Maafisa lishe kushirikiana kwa ukaribu katika kuboresha huduma za tiba Asili kwa kutumia taalama zao kwa kushirikiana na Waganga wa Tiba Asilia ili kuweza kupata soko linalostahili na lenye usalama na ufanisi wakutosha.

Jumatano, 21 Februari 2018

Usitumie Dawa bila ushauri wa mtoa huduma za Afya

Jumanne, 20 Februari 2018

CHUKUA TAADHARI DHIDI YA UGONJWA WA KIPINDUPINDU

Alhamisi, 15 Februari 2018

FAHAMU UGONJWA WA KIFAFA










Jumatano, 14 Februari 2018

SERIKALI YAENDELEA KUSOGEZA HUDUMA ZA AFYA KWA WANANCHI KWA KUONGEZA VITUO VYA AFYA NCHINI.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi katika ufunguzi wa jengo la mama na mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana, mapema leo jijini Dar es salaam, katikati ni Naibu waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimjulia hali moja ya mama aliyekuwa akiuguliwa na mtoto wake, akifanya hivyo baada ya kuzindua jengo la mama na mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana, kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Poul Makonda.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakisalimiana na Mbunge wa Ilala Mhe. Azan Zungu wakati wa Uzinduzi wa jengo la mama na mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana, wa pili ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Poul Makonda na wa mwisho ni Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa mama aliyekuwa akiuguliwa na mtoto wake, akifanya hivyo baada ya kuzindua jengo la mama na mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana, kulia kwake ni Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, kulia kwake ni Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Poul Makonda.

Na WAMJW. DSM
SERIKALI yaendelea kuongeza vituo vya Afya nchini ikiwa ni moja ya jitihada za Serikali za kuboresha Huduma za afya nchini jambo litakalo saidia kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali za Wilaya na Mkoa kwa kuwa huduma zote zitakuwa zimeishia kwenye ngazi ya Kata.
Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa ufunguzi wa jengo la mama na mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana, mapema leo jijini Dar es salaam.
“Kumekuwa na ongezeko kubwa la vituo vya Afya nchini kutoka vituo vya Afya 6321 kwa mwaka 2010 hadi vituo vya Afya 7680 kwa mwaka 2016, na kazi ya nyongeza inaendelea, kwaiyo tunaamini  vituo hivi vitaweza kupunguza msongamano katika hospitali za Wilaya, pamoja na Hospitali za Mkoa”, alisema Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Mhe. Waziri Mkuu alisema kwamba Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametenga kiasi cha Zaidi ya Bilioni 100 ikiwa ni fedha za kuboresha Vituo vya Afya nchini ili kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi katika maeneo yote nchini.
“Tumeanza kuboresha Vituo vya Afya kwa kujenga Wodi yakinamama wanaojifungua, thieta, wodi za magonjwa yakawaida, maabara, tunaongeza na nyumba za watumishi, ili kila kituo cha Afya kiwe na miundombinu hiyo ili utoaji huduma uwe rahisi” alisema Mh. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Mhe. Waziri Mkuu aliendele kusema kwamba Serikali imetumia Zaidi ya Bilioni 161 katika kuendelea kuboresha Huduma za Mama na Mtoto kwa lengo la kuokoa Maisha ya mama na mtoto jambo ambalo ni moja kati ya changamoto kubwa nchini.
Aidha Mhe. Waziri Mkuu alisema kwamba Serikali imeendelea kuboresha Huduma za Afya kwa kutenga kiasi cha shilingi Bilioni 129 kwaajili ya vifaa vya kuwezesha kundesha shughuli za upasuaji katika kila kituo cha Afya ambacho kinaboreshwa.
Wakati akitoa taarifa ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Poul Makonda alisema kwamba wakina mama 126,164 walipata nafasi ya kujifungua katika vituo vya Afya, huku wakinamama 202 ambao ni sawa na Asilimia 0.5 walilazimika kujifungua kwa wakunga, na Asilimia 1.5 zaidi ya akinamama 1976 walijifungua njiani wakielekea kupata huduma, idadi inayoonekana kuwa kubwa sana katika Mkoa wa Dar Es salaam.
Idadi ya 2016 inaonesha Zaidi ya akina mama 85 walikuwa wanapoteza Maisha kati ya kina mama 100,000 waliokuwa wanajifungua lakini kwa sasa tangu maboresho yafanyike ni akina mama 57 kati ya akina mama 100,000 wanaojifungua ndio hupoteza Maisha, huku mikakati thabiti yakupunguza vifo hivyo ikiendelea kuwekwa.
Mhe. Makonda aliendelea kusema kwamba zaidi ya watoto ambao wanafanikiwa kuwa hai na kuwa salamakatika kujifungua ni Zaidi ya watoto 126,712, na watoto 131 huzaliwa wakiwa tayari wameshakufa, idadi hii ikilinganishwa .
Pia Mhe. Makonda alimshukuru AMSONS GROUP ambayo imetoa mchango mkubwa katika ujenzi wa Jengo hilo la Mama na Mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana huku akiwataka Wadau wengine kuiga mfano huo katika dhana ya kusukuma gurudumu la maendeleo katika jamii zetu.
Nae Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano tangu iingie madarakani imeongeza Bajeti ya Dawa kutoka Bilioni 30 mpaka sasa ni Bilioni 270 likiwa ni ongezeko la Zaidi ya mara 9, huku Wastani wa upatikanaji wa dawa ukiwa Zaidi ya asilimia 80.
“Serikali wakati inaingia madarakani Bajeti ya dawa ilikuwa ni Bilioni 30, mwaka unaofuata ikafikia Bilioni 200, na hivi tunavyoongea Bajeti ya Dawa ni Bilioni 270, likiwa ni ongezeko la mara 9, kama msaidizi wako nasimama kifua mbele na kusema ya kwamba hatuna uhaba wa Dawa muhimu”, alisema Dkt. Ndugulile.