Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Ijumaa, 30 Novemba 2018

DKT. MPOKI -"MADAKTARI TIMIZENI WAJIBU WENU"

- Hakuna maoni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Utawala wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Beatrice Erasto wakati alipotembelea Taasisi hiyo kujionea hali ya utoaji wa huduma leo jijini Dar Es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Udhibiti wa Ubora wa Huduma kutoka Wizara ya Afya Dkt. Mohamed Mohamed.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (katikati) akiongea na Mgonjwa wa Saratani (Jina halijafahamika) aliyelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road iliyoko Jijini Dar Es Salaam wakati alipofanya ziara kujionea hali ya utoaji wa huduma katika Taasisi hiyo. Kushoto ni Kaimu Meneja wa huduma za tiba Dkt. Sadik Siu na kulia ni Mkurugenzi wa Udhibiti wa Ubora wa Huduma kutoka Wizara ya Afya Dkt. Mohamed Mohamed.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na wananchi waliofika kupata huduma za uchunguzi na matibabu katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road wakati alipotembelea Taasisi hiyo leo kujionea hali ya utoaji huduma.


Na.WAMJW, Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya amewataka Madaktari wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road   kutimiza wajibu wao katika kuwahudumia wagonjwa  wanaofika hospitalini hapo kila siku  na kumuagiza Mkurugenzi wa Huduma za  Uhakiki na Ubora kutoka Wizarani kwake kufuatilia.

Dkt.Mpoki ametoa agizo hilo alipotembelea taasisi hiyo ili kujionea hali ya utoaji huduma pamoja na kusikiliza wagonjwa wanaofika kupata huduma kwenye taasisi hiyo kutokana na kulalamikiwa kwa baadhi madaktari na wauguzi “Taasisi hii ni ya faraja lazima mtengeneza mazingira mazuri yakuwahudumia wagonjwa,kwani ndugu wanafuatilia hali za wagonjwa wao hivyo jamii inapolalamika tusiseme moja kwa moja ni waongo bali tushughulikie malalamiko yao ,kama huna jibu muelekeze kwa mtu ambaye anaweza kumpa jibu ili aweze kupata faraja”.Alisisitiza Dkt.Mpoki.

Aidha, aliwataka watumishi wa taasisi hiyo kuvaa vitambulisho ambavyo vinaweka wazi utambulisho wao ili ndugu na wagonjwa waweze kuwatambua na kutaja ni nani ambaye hajatimiza wajibu wake ipasavyo.

“watakaoshindwa kwenda nasi tutawapeleka kwingine,hatutaki maumivu yawe sehemu ya uzoefu wa wagonjwa wanaolazwa Ocean Road,nyinyi kazi yenu ni kuwahudumia wagonjwa”.

Hata hivyo aliwataka madaktari wabobezi (Mabingwa) kutimiza wajibu wao na sio kuwaachia jukumu la kuwahudumia wagonjwa madaktari waliopo mafunzo kwa vitendo”kuanzia sasa tukigundua mgonjwa ameachiwa daktari wa mafunzo kwa vitendo tutawaondoa wasifanye mazoezi hapa lazima tuishi kwa kutii na kufuata miiko ya taaluma zetu”alisema dkt.Mpoki

Aliagiza kufanyika mikutano ya ndani mara kwa mara ya kufuatilia utendaji kazi wa taasisi  na kujibu malalamiko yanayotolewa kwenye mitandao ya kijamii pamoja na masanduku ya maoni ili kupata mrejesho kutoka kwa wananchi ili kuboresha huduma zinazotolewa kwenye taasisi.

Kuhusu adha ya umbali wa kufuata huduma kwenye taasisi hiyo Dkt. Mpoki aliwathibitishia wagonjwa na ndugu waliopo hospitalini hapo kuwa Serikali kupitia wizara ya afya iko mbioni kupeleka huduma za saratani kanda ya kusini mara tu itakapokamilika hospitali ya Rufaa ya kanda,pia huduma kama hizo zipo mbioni kupelekwa kwenye hospitali ya rufaa ya Tabora pamoja na hospitali maalum ya Benjamin Mkapa iliyopo jijini Dodoma kwani ni wajibu wao kuhakikisha huduma hizo karibu na wananchi.

-Mwisho-

ASILIMIA 85 YA WANAWAKE MKOANI MARA WANAJIFUNGUA KATIKA VITUO VYA AFYA.

- Hakuna maoni

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisikiliza maoni ya mmoja kati ya wagonjwa waliofika kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,...

Alhamisi, 29 Novemba 2018

TAASISI YA MIFUPA (MOI) YATAKIWA KUWASILIANA NA WATEJA KWA NJIA YA SIMU

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiangalia mashine ya mionzi ya CT SCAN katika Taasisi ya mifupa (MOI) wakati alipoitembea ili kujionea hali ya utoaji wa...

WAZIRI UMMY AAGIZA HOSPITALI ZOTE ZA RUFAA ZA MIKOA KUTOA MATIBABU YA KINYWA NA MENO.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee hma Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya Madaktari wa Afya ya kinywa na meno (hawapo kwenye picha) wakati akifungua mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa...

Jumatano, 28 Novemba 2018

DKT. NDUGULILE AIPONGEZA TAASISI YA NIMR KWA KUFANYA TAFITI ZENYE TIJA KWA TAIFA.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia sampuli za mbu katika maabara ya Taasisi ya Nimr Muheza, Tanga Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na...

Jumatatu, 26 Novemba 2018

WADAU WA SEKTA YA AFYA KUENDELEA KUBORESHA UTOAJI WA HUDUMA NCHINI

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na wadau mbalimbali wa maendeleo na wakurugenzi wa wizara (Hawapo Pichani) wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ya afya...

VITUO VYA DAMU SALAMA VYATAKIWA KUBORESHA HUDUMA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa ameketi kwenye kiti maamul kinachotumika wakati wa kutoa damu alipitembelea kituo cha damu salama kanda ya kaskazini. Naibu Waziri wa Afya,...

HOSPITALI YA KIBONG’OTO KUWA KITUO CHA TAFITI, TIBA NA MAFUNZO YA MAGONJWA AMBUKIZI

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akipata maelekezo namna wanavyopima wagonjwa wa kifua kikuu toka kwa Mganga Mfawidhi Hospitali Maalum ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto Dkt. Riziki Kisonga...

Ijumaa, 23 Novemba 2018

MATUKIO KATIKA PICHA, ZIARA YA DKT. NDUGULILE MKOANI KILIMANJARO.

- Hakuna maoni

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile jana Novemba 22, 2018 ameanza ziara yake ya kikazi kwa Mkoa wa Kilimanjaro. Akiwa mkoani kilimanjaro jana alifika katika Ofisi ya...

Page 1 of 102123»