Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akimjulia hali mtoto aliyefika na mama yake kupata matibabu katika Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya
utoaji Huduma za Afya kwa wananchi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akimjulia hali mtoto aliyefika kupata matibabu akiwa na Baba yake, katika Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya
utoaji Huduma za Afya kwa wananchi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akitoa maelekezo ndani ya chumba cha kuhifadhi Dawa katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi, wakati alipofanya ziara ya kukagua
hali ya utoaji Huduma za Afya kwa wananchi mkoani Lindi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akikagua
miundombinu katika chumba cha X- ray wakati alipofanya ziara ya
kukagua hali ya utoaji Huduma za Afya kwa wananchi katika Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Lindi.
WAGONJWA WA SARATANI WAONGEZEKA KUTOKA 2500 HADI 6500
Na.WAMJW-LINDI
SERIKALI
Kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imesema kuwa kutoka kipindi cha mwaka 2002 mpaka hivi sasa kumekuwa na
ongezeko kubwa la Wagonjwa wa Saratani kutoka wagonjwa 2500 hadi
wagonjwa 6500, kutokana na mitindo tofauti ya maisha na mabadiliko ya
sayansi na teknolojia.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiwa katika ziara ya kukagua hali ya
utoaji huduma za afya na uhamasishaji kwa wakulima kujiunga na mfuko wa
Bima ya afya (#UshirikaAfya) katika Mkoa wa Lindi.
"Kama
Serikali, Tumeshtushwa na ongezeko la Wagonjwa wa Saratani na magonjwa
mengine yasiyo ya kuambukiza, mwaka 2002 wagonjwa wa Saratani nchini
walikuwa kati 1500 mpaka 2000, lakini kwa takwimu za mwaka Jana,
wagonjwa wa Saratani wameongezeka kutoka 2500 hadi 6500" alisema Waziri
Ummy.
Waziri Ummy
aliendelea kusema kuwa Serikali imeona upo ulazima wa kuchukua hatua za
makusudi katika kupambana na Saratani ya Mlango wa kizazi na magonjwa
mengine yasiyo ya kuambukiza yakiwemo shinikizo la damu, magonjwa ya
moyo na ugonjwa wa Kisukari.
Pia,
Waziri Ummy alisema kuwa katika kila Wagonjwa 100 wa Saratani, Wagonjwa
34 ni wa Saratani ya mlango wa Kizazi, Wagonjwa 12 ni wa Saratani ya
Matiti, kibaya zaidi katika kila Wagonjwa 100 wa Saratani, Wagonjwa 80
wanafika wakiwa wamechelewa na wengine ugonjwa ukiwa katika hatua ya
tatu au ya nne, hivyo kupona kwao kunakuwa ni kugumu.
Awali
akisoma taarifa ya Mkoa, Katibu tawala Mkoa wa Lindi Bi. Rehema Madenge
alisema kuwa Mkoa umeweza kuanzisha utoaji wa chanjo ya kukinga
Saratani ya mlango wa kizazi (HPV) kwa Wasichana wa umri wa miaka 9
hadi 14 ambapo leo tutashudia ikizinduliwa na rasmi kimkoa na Waziri wa
Afya mhe. Ummy Mwalimu.
Hata
hivyo Bi. Madenge alisema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2017/2018
jumla ya mahudhurio 164,259 yalirekodiwa katika vituo vyote vya kutolea
huduma za Afya vya Serikali, binafsi na vile vya dini huku Hospitali ya
Mkoa Sokoine ikirekodi mahudhurio 39,324 na kulipwa shilingi
1,654,964,965 katika kipindi hicho.
"Mkoa
umeendelea kuhudumia wanufaika wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) kwa
ufanisi mkubwa na katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 jumla ya mahudhurio
164,259 yalirekodiwa katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya vya
Serikali, binafsi na vile vya dini" alisema Bi. Madenge
Aidha,
alisema kuwa ili kuweza kuwafikia wananchi wengi kupitia makundi mbali
mbali, mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umekuja na mpango uitwao
#Ushirika Afya ambapo wakulima wanaungana pamoja katika vyama vyao vya
mazao na kuweka mkakati wa kujiunga na Bima ya Afya kwa utaratibu wa
ushirika wao.
Mwisho.
0 on: "WAGONJWA WA SARATANI WAONGEZEKA KUTOKA 2500 HADI 6500"