Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.
Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa Habari
(Hawapo kwenye picha) wakati akitoa tamko kuhusu kampeni ya kumeza dawa
kingatiba ya magonjwa ya minyoo ya Tumbo, Usubi, Trakoma na Matende na
Mabusha katika mikoa saba hapa nchini.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.
Faustine Ndugulile akitoa tamko kuhusu kampeni ya kumeza dawa kingatiba
ya magonjwa ya minyoo ya Tumbo, Usubi, Trakoma na Matende na Mabusha
katika mikoa saba hapa nchini, pembeni yake ni mratibu wa Magonjwa
yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Upendo Mungila
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.
Faustine Ndugulile akitoa tamko kuhusu kampeni ya kumeza dawa kingatiba
ya magonjwa ya minyoo ya Tumbo, Usubi, Trakoma na Matende na Mabusha
katika mikoa saba hapa nchini, pembeni yake ni mratibu wa Magonjwa
yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Upendo Mungila
TAMKO LA MHE. DKT. FAUSTINE NDUGULILE (MB.) NAIBU WAZIRI
WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU KAMPENI YA
KUMEZESHA DAWA KINGATIBA YA MAGONJWA YA MINYOO YA TUMBO, USUBI,
TRAKOMA, MATENDE NA MABUSHA KATIKA MIKOA SABA (7) HAPA NCHINI.
Ndugu Wananchi
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikishirikiana na
wadau itafanya kampeni ya kugawa dawa za Kingatiba ya magonjwa ya minyoo
ya tumbo, usubi, trakoma, matende na mabusha katika mikoa saba (7) hapa
nchini, ambayo ni Dar es Salaam katika Manispaa zote, Iringa wilaya ya
Mufindi DC, Mtwara wilaya ya Masasi, Pwani wilaya ya Kibaha na Mafia,
Rukwa wilaya ya Kalambo, Songwe wilaya ya Songwe na Tanga wilaya ya
Mkinga na Korogwe.
Lengo kuu la kufanya kampeni ni
kutibu na kuzuia maambukizi ya magonjwa ya minyoo ya tumbo, Usubi,
Trakoma, Matende na mabusha au Ngirimaji. Aidha, dawa hizi au kingatiba
hii, zitasaidia kupungua kwa ulemavu na adha za magonjwa haya. Kuna
faida kubwa kwa wananchi wakishiriki katika zoezi hili la umezaji kinga
tiba hii. Faida hizo ni:
Kukinga upungufu wa damu.
Kumuepusha mtu kupata upofu.
Kupunguza maambukizi kutoka mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Kuua vimelea vya Magonjwa haya.
Kukinga na kupunguza maumivu na madhara yanayosababishwa na Magonjwa haya.
Kupungua kwa Magonjwa ya ngozi.
Kuongeza virutubisho bora mwilini.
Kuboresha nguvukazi katika jamii.
Kuwezesha watoto kukua vizuri.
Kuongeza uelewa wa watoto wawapo shuleni.
Ugonjwa
wa Minyoo ya tumbo huathiri zaidi jamii maskini na husababishwa na mtu
kula mayai ya minyoo kutoka katika udongo au minyoo hii kupenya kwenye
ngozi. Aidha, Kuna minyoo ya aina tatu ambayo husababisha ugonjwa
huu,minyoo mviringo,minyoo mijeledi na minyoo ya safura. Pamoja na
kutoa dawa za kutibu ugonjwa huu lakini pia jambo la msingi ni vyema
wananchi mkaweka maeneo yanu katika hali ya usafi na kula vyakula
vilivyopikwa vizuri na kuiva.
Ugonjwa wa Usubi
husababishwa na minyoo inayoitwa Onchocerca volvulus, huenezwa na inzi
weusi wadogo wanaokaa kandokando ya mito yenye maji yaendayo kasi.
Athali za ugonjwa huu ni ngozi kuwasha, ngozi kuwa na mabakamabaka kama
ya chui, ngozi kuwa na muonekano wa kenge, pia uono hafifu na upofu.
Trakoma
au vikope ni ugonjwa sugu unaoshambulia macho na kusababisha kope
kupinda na kugusa kioo cha jicho ambapo husababisha makovu juu ya kioo
cha jicho na hupunguza uwezo wa kuona na kusababisha upofu usiotibika.
Ugonjwa huu husababishwa na bakteria aina ya Chlamydia trachomatis.
Juhudi
kubwa za kutokomeza ugonjwa wa Trakoma au Vikope zimefanyika na kuweza
kupunguza kiwango cha maambukizi. Kati ya Wilaya 71 zilizokuwa na
uambukizo, Wilaya 63 sawa na Asilimia Themanini na Tisa (89%) zimeweza
kufikia kiwango cha chini ya asilimia 5% ambayo inaruhusu kusimamisha
zoezi la kingatiba ya Trakoma katika ngazi ya Jamii. Katika mwaka huu
wa 2018 ni Wilaya 8 tu ndio zinaendelea na zoezi la Kingatiba ya
ugonjwa wa Trakoma kwa kutumia dawa aina ya Zithromax.
Ugonjwa
wa Matende na Mabusha husababishwa na minyoo midogo midogo ambayo
huenezwa na mbu wa aina zote kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Dalili
za ugonjwa huu ni homa kali ambayo huchukua siku 3 – na huambatana na
baridi kali, Kichefuchefu, kutapika, kuvimba kwa mitoki, kubabuka ngozi,
kuvimba kwa miguu, mikono, matiti au sehemu za siri kwa jinsia zote.
Mafanikio
katika kutokomeza ugonjwa wa Matende na mabusha yameanza kuonekana,
kati ya Wilaya 120 ambazo zilikuwa na uambukizo, Wilaya 98 ambazo ni
sawa na asilimia sabini na Saba (77) zimeweza kupunguza maambukizi ya
ugonjwa huo na hivyo kufikia kiwango cha kusimamisha ugawaji wa
kingatiba kwa jamii katika Wilaya hizo.
Hii
ina maana kwamba kwa mwaka huu 2018 ni wilaya 28 tu ndizo zitakuwa na
zoezi la umezeji kingatiba kwa ajili ya kukinga na kutibu ugonjwa wa
Matende na mabusha katika ngazi ya jamii. Magonjwa haya yasipopatiwa
tiba haraka mtu anaweza kupata madhara kama:-
Maumivu ya muda mrefu na wakati mwingine ulemavu mkubwa.
Umaskini na kudumaza uchumi wa kaya na hatimaye Taifa.
Kudhoofisha ukuaji hasa kwa watoto wenye umri mdogo kimwili na kiakili.
Utapia mlo kwa watoto
Utumbo kujisokota
Hatimae kifo kama mgonjwa hakutibiwa.
Ndugu Wananchi
Pamoja
na kwamba ugawaji wa dawa utafanyika katika mikoa saba (7) hapa nchini,
napenda nijikite sana katika kuelezea umezaji wa dawa katika mkoa wa
Dar es Salaam kwa mwaka huu wa 2018. Hii siyo mara ya kwanza kwa mkoa
huu kufanya zoezi la umezaji wa dawa Kingatiba ya minyoo ya tumbo,
matende na mabusha. Zoezi hili kwa mkoa wa Dar es Salaam lilianza mwaka
2013 na limekuwa likitekezwa kila mwaka. Katika mwaka wa kwanza watu
wapatao 3,028,828 walijitokeza na kupatiwa kingatiba hii. Idadi hii
imekuwa ikiongezeka kila mwaka zoezi linapotekelezwa na kwa mwaka jana
2017, watu waliojitokeza kupatiwa kingatiba walikuwa 4,914,351 ambayo ni
sawa na asilimia 86 (86%) ya lengo lililotarajiwa.
Ingawa
kiwango cha umezaji wa dawa hizi kwa jamii kimeendelea kuwa juu, lakini
idadi ya watu wanaojitokeza kwenye zoezi hili bado haijaridhisha sana
kutuwezesha kutangaza kwamba tutatokomeza magonjwa haya katika mkoa wa
Dar es Salaam, bado maambukizi yapo juu ya kiwango cha asilimia mbili
(2%). Lengo la mwaka huu ni kugawa dawa watu wapatao 5,376,207 katika
Manispaa zote tano (5) za Mkoa wa Dar es Salaam.
Kama
wizara tumeweza kuwezesha rasilimali za dawa na fedha za utekekelezaji
wa kampeni hi muhimu. Aidha tumeweza kusaidiana na wenzetu wa TAMISEMI
kufanya uhamasishaji kwa ngazi mbalimbali kwa viongozi wa jamii, kata na
mitaa. Kampeni hii itawapa fursa wanajamii kupunguza uambukizo wa
magonjwa haya na hatimaye kuwa jamii kuwa huru na vimelea vya magonjwa
haya kwa vizazi vijavyo.
Kampeni hii kwa mwaka
huu, itahusisha wakazi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam na wageni waliopo
katika Jiji hili wenye umri wa kuanzia miaka mitano (5) na kuendelea.
Dawa zitakazotolewa ni aina Albendazole kidonge kimoja (kitatafunwa) na
Ivermectin (Mectizan) ambayo itatolewa kulingana kimo chake .
Ndugu Wananchi
Napenda
kuwataarifu kuwa kampeni hii itaendeshwa kuanzia tarehe 15 hadi 20
mwezi Disemba, 2018 kwa watu wenye umri uliotajwa hapo juu. Napenda
kusisitiza kuwa viongozi wa ngazi zote ikiwa ni pamoja na ngazi ya jamii
wanawajibika kutoa taarifa hii na kuhamasisha wananchi wote washiriki
kikamilifu katika kampeni. Aidha, katika kufanikisha zoezi hili
nawasishi wananchi na viongoziu wote kutumia njia mbalimbali za
mawasiliano kama vile vyombo vya habari, kuhamasisha wananchi makanisani
na misikitini kujitokeza kushiriki zoezi hili.
Aidha,
wanachi mtambue kuwa vituo vya kutolea huduma hizi vimesogezwa karibu
jamii ili kurahisisha upatikanaji wa huduma. Ambapo Jumla ya vituo mia
tisa kumi na tano (915) ambavyo ni pamoja na Zahanati, Vituo vya afya,
Hospitali, stendi za mabasi, masoko, ofisi za serikali za mitaa, ofisi
za taasisi mbalimbali pamoja na kambi za Majeshi yetu na Magereza
vitatoa huduma hiin a takribani wagawa dawa Elfu moja mia nane
thelathini (1,830) waliopatiwa mafunzo watahusika katika kutoa huduma
hiyo kwenye vituo Mwisho napenda kutoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Dar
es Salaam na wa mikoa mingine ambayo zoezi hili litafanyika kushiriki
kikamilifu katika umezaji dawa hizi. Zoezi hili ni muhimu kwani magonjwa
haya yanaathiri sana jamii yetu. Kwa viongozi wenzangu na wanahabari
tunaomba muendelee kuelimisha umma kuhusu magonjwa haya na umuhimu wa
umezaji wa kingatiba hii.
LINDA, OKOA MAISHA, ZUIA ULEMAVU JITOKEZE KUMEZA DAWA-KINGATIBA’
0 on: "SERIKALI YATOA RAI KWA WANANCHI KUJITOKEZA KUPATA DAWAKINGA YA MATENDE NA MABUSHA"