Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile (wakati kati) akishuhudia
makabidhiano ya mabenchi yakukalia, wakwanza kulia ni Meneja wa NMB
kanda ya Dar es salaam Bw. Badru Idd akimpa mkono Mwakilishi wa
Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. John Rwegasha katika
tukio la makabidhiano ya mabenchi yakukalia 52 lililofanyika katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile akiteta jambo na Meneja wa
NMB kanda ya Dar es salaam Bw. Badru Idd katika tukio la makabidhiano ya
mabenchi yakukalia 52 yenye thamani ya Mikioni 10, lililofanyika katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile akikagua mabenchi hayo
baada ya makabidhiano leo, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini
Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile akimuaga Meneja wa NMB
kanda ya Dar es salaam Bw. Badru Idd baada ya tukio la makabidhiano ya
mabenchi yakukalia 52 yenye thamani ya shilingi Milion 10, lililofanyika
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.
Jengo la mahala pakupimzikia la Kitengo cha Dharura, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
HOSPITALI MPYA 67 ZA WILAYA KUJENGWA NCHINI
Na WAMJW - Dar es salaam.
SERIKALI
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee ma Watoto
inatarajia kujenga Hospitali za Wilaya 67, ikiwa ni mkakati na jitihada
za Serikali kuboresha Huduma za Afya na kupunguza adha kwa wananchi
kupata huduma za afya.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile leo wakati akipokea viti kwaajili
yakupumzikia hospitalini, kutoka benki ya NMB katika Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
Dkt.
Ndugulile amesema kuwa kwa sasa zipo Hospitali za Wilaya 80, hivyo
Serikali imeamua kuongeza hospitali za Wilaya takribani 67 ikiwa ni
mkakati wa kuboresha huduma za Afya hususani huduma za mama na mtoto.
"Mwaka
huu tunajenga Hospitali za Rufaa, Mikoa ambayo haina, tunajenga
Hospitali za Wilaya 67, na tunahospitali kama 80 za Wilaya," alisema
Dkt. Ndugulile.
Dkt.
Ndugulile aliendelea kusema kuwa Serikali imeboresha vituo vya Afya
takribani 200 ili kusaidia kutoa huduma za upasuaji, hivyo kusaidia
kupunguza msongamano wa wagonjwa kupata huduma katika Hospitali za
Wilaya na za Rufaa za Mkoa.
Sambamba
na hayo Dkt. Ndugulile ameishukuru Benki ya NMB kwa kutenga Asilimia 1
ya mapato yanayotoka kwenye faida kuelekeza kwenye Jamii ya Watanzania
hususani katika huduma za Afya.
"Niwashukuru
sana NMB bank, kwa kutenga mapato yenu na faida yenu kuielekeza kwenye
jamii, na nimefurahi zaidi, kusikia kwamba mmewekeza zaidi katika huduma
za Jamii, Sisi kama Serikali tunawapongeza" alisema Dkt Ndugulile
Dkt.
Ndugulile aliendelea kusema kuwa vitawasaidia sana wagonjwa ambao
wanatoka sehemu mbali mbali ya nchi kupata maeneo mazuri yakuweza kukaa
wakati wagonjwa wao wakipata huduma za Afya, hivyo niwaombe sana
msiishie hapo kwani bado kuna maeneo mengi yanahitaji msaada.
Nae
Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam Bw. Badru Idd amesema kuwa benki
ya NMB huwa inalipa fadhira kwa Jamii baada ya kupata faida, kwa kuleta
maendeleo, ikiwemo kujenga miundombinu, na kuboresha huduma za Jamii ili
watanzania waweze kunufaika na kutoka Benki yao ya NMB.
"Kwa
mujibu wa taratibu za Benki ya NMB huwa tunatoa Asilimia 1% kwenye pato
ambalo tumepata kwa mwaka huo, mathalani mwaka Jana tumeingiza milioni
94, hivyo tunatoa Asilimia 1% ya Milioni 94 na kuirudisha kwa Jamii"
alisema Bw. Badru Idd.
Bw.
Badru Idd aliendelea kusema kuwa hiyo Asilimia 1% ipo kwenye mafungu
makubwa 3, kundi la kwanza NMB inapenda sana kutoa huduma kwenye sekta
ya Afya, kundi la pili ni Sekta ya Elimu na kundi la tatu ni huduma
kwenye majanga yanayotokea.
Mwisho.
0 on: " HOSPITALI MPYA 67 ZA WILAYA KUJENGWA NCHINI"