Na WAMJW - MTAMA, LINDI.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewataka wakulima kujiwekea utaratibu wa kukata Bima ya Afya ili kurahisisha kupata matibabu pindi wanapopata maradhi.
Amesema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya na uhamasishaji kwa Wananchi pamoja na Wakulima kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya kwenye mkutano wa hadhara katika jimbo la Mtama Lindi vijijini.
Waziri Ummy, aliwqtaka wananchi wa mtama kujiunga na Bima ya Afya inayoitwa "UshirikaAfya " ambayo ni maalumu kwa wakulima inayopatikana kwa shilingi 76,800 kwa familia pia kuwakatia watoto chini ya miaka kumi na nane bima ya shilingi 50,400.
Aliendelea kusisitiza umuhimu wa kujiunga na Bima, kwa kuwaelezea Faida na ubora wa bima hiyo ya afya ambayo mtu anapaswa kujiunga kwa kiasi cha shilingi 76,800 na mtu huyo atapata huduma ya afya sehemu yoyote ndani ya Tanzania, katika Hospitali zote za Serikali na za Binafsi
"Hii inaitwa jipimie haina utofauti na vifurushi vya simu na ndiyo maana Mwanzo tulikuwa na CHF kwa shilingi 15,000, tukaja CHF iliyoboreshwa ya 30,000 na sasa tuna Ushirika Afya ya 76,800 ambayo mtu anatapata huduma kokote Tanzania na kwenye maduka ya dawa yote yaliyoungwanishwa na mfuko wa Bima ya Afya". alisema Waziri Ummy.
Aidha, Waziri Ummy aliwataka viongozi wa vyama vya msingi kuwa mabalozi wazuri kwa kuwahamasisha wakulima wao kujiunga na bima ya ushirika Afya ili kurahisisha kupata matibabu pindi wanapopata maradhi.
" Najua wananchi wetu watasema hiyo bima ni ghali nyie ndiyo muwe mabalozi wa kuwaelimisha juu ya faida ya bima hii kwa sababu mmepata bahati ya kupata elimu ya bima na ukitegemea wananchi wa huku wanategemea hela za msimu jitahidini kuwaelimisha kipindi hiki wanachopokea hela za korosho ili wajiunganishe na Bima ya Afya" alisema Waziri Ummy
Pia, Waziri Ummy alisema kuwa, mtu akijiunga na Bima hiyo ndani ya wiki atapata kadi yake na ndani ya siku 21 ataanza matumizi ya kadi hiyo sehemu yoyote atakayoenda iwe hospitali za Serikali, Hospitali za binafsi na maduka ya dawa yaliounganishwa na mfuko wa Bima ya Afya (NHIF).
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Lindi vijijini Dkt. Dismas Masulubu amesema kuwa Wilaya ya Lindi vijijini imepokea jumla ya watumishi 88, huku kati yao ni Watumishi 82 tu ndio walioripoti Na Watumishi 79 wakiwa wamekwishilaingizwa kwenye malipo ya mishahara, huku mchakato ukiendelea ili kukamilisha kwa Watumishi 3 waliobaki.
Dkt. Dismas Masulubu aliendelea kusema kuwa hali ya upatikanaji wa dawa katika Wilaya hiyo ni Asilimia 94.7% mpaka sasa, jambo lililosaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo katika Wilaya hiyo hasa vifo vya mama na mtoto.
Mbali na hayo Dkt. Dismas Masulubi alisema kuwa kwa Mwaka 2018/2019 Halmashauri ilitenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya viwili, miongoni mwa vituo hivyo ambavyo vilikuwa katika ukarabati ili viweze kufanya huduma za upasuaji wa dharura (CeMOCo) Kituo cha Afya cha Mtama ambacho kilitengewa zaidi ya Milioni 25, na kituo kingine kitajengwa Miole.
Mwisho.
0 on: "BIMA YA AFYA NDIO MPANGO MZIMA- UMMY MWALIMU."