Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Ijumaa, 14 Septemba 2018

VIDONDA VIUGUZWE KWA USAFI KUEPUKA SEPSIS

 Katibu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akitoa ufafanuzi juu ya Ugonjwa wa Sepsis katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es salaam.
 
VIDONDA VIUGUZWE  KWA USAFI KUEPUKA SEPSIS

Na WAMJW- DAR ES SALAAM. 

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto imewataka watanzania kuuguza vidonda kwa usafi na uangalizi mkubwa  pale wanapopata majeraha ili kuepuka kupata Bakteria wa Sepsis. 

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya  Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati akitoa tamko kuhusu uwepo wa bakteria hao na jinsi ya kujikinga leo jinini Dar es salaam. 

"Watoa huduma za afya hususan wale wanaofunga vidonda wanatakiwa kujirinda na kuhudumia kwa kujistiri zaidi ili kuepuka kupata bakteria  hao kwani vidonda vinapokuwa wazi inakua rahisi kupata bakteria hao" alisema Dkt. Ulisubisya.

Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa wamama wanaojifungua na watoto wachanga wapo katika hatari zaidi kwani tafiti zinaonesha kuwa asilimia 8 ya vifo vya wajawazito na asilimia 32 ya vifo vya watoto wachanga huchangiwa na bakteria hao. 

Dkt. Ulisubisya amesema kuwa kutokana na  takwimu za Shirika la Afya Duniani WHO zinaonesha kuwa watu milioni 30  duniani kote wanapata bakteria  wa Sepsis na milioni 6 hupoteza maisha kutokana na bakteria hao kila mwaka. 

Kwa mujibu wa Dkt.  Ulisubisya amebainisha kuwa watu wenye ugonjwa wa Ukimwi, Kisukari,utapia mlo uliopitiliza,  wanaotumia dawa za saratani pamoja na wenye usugu wa dawa wapo kwenye mazingira hatarishi ya kupata bakteria hao. 

Aidha Dkt. Ulisubisya alisema kuwa dalili za mwenye bakteria hao ni homa kali kupindukia, mapigo ya moyo kwenda haraka sana au polepole sana pamoja na kuhema harakaharaka na madhara yake hayaachi maeneo yeyote ya mwili. 

Dkt. Ulisubisya amesema kuwa jinsi ya kujikinga na bakteria hao  ni kufanya usafi wa mwili ikiwemo  kuoga mara kwa mara na kunawa mikono kwa maji safi na salama 

Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa Wizara ya Afya  imetoa mafunzo ya Kukinga na Kudhibiti Maambukizo kwenye ngazi ya Kitaifa, Kanda, Mikoa, Halmashauri pamoja Vituo vya Afya na Zahanati. 

"Kama Wizara tutaendelea Kuimarisha huduma na Maabara ili kuweza kubaini aina ya Vijidudu vinavyohusika na Sepsis kwa mgonjwa husika pamoja na hali ya usugu wa viuavivyasumu ili Madaktari na Matabibu waweze kutoa tiba sahihi ili kutokomeza bakteria hao" alisema Dkt. Ulisubisya.  

Sepsis ni uwepo wa bakteria hatari kwenye mwili hivyo uwepo wa bakteria hawa mwilini husababisha uzalishaji wa kemikali hatari ambazo husababisha mtu kuumwa sana na wakati mwingine kufikia kupata mshituko ambao kitaalamu huitwa "septic shock". 

MWISHO.

0 on: "VIDONDA VIUGUZWE KWA USAFI KUEPUKA SEPSIS"