Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumanne, 7 Agosti 2018

WIZARA YA AFYA YATENGA BILIONI 14 KWA AJILI YA HUDUMA UZAZI WA MPANGO

Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo katika Mkutano uliowakutanisha viongozi na watendaji wakuu wa Halmashauri na Wilaya kutoka Mkoa wa Tanga wenye lengo la kuendeleza juhudi za Serikali juu ya masuala Ya uzazi wa mpango,  chini ya JhPiego unaofadhiliwa na Melinda Gate.

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe ambae alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kisa Kasongwe akitoa neno umbele ya viongozi na watendaji wakuu wa Halmashauri na Wilaya baada ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Áfya Mhe Ummy Mwalimu.

Mganga mkuu wa Mkoa wa Tanga DKt. Asha Mahita akielezea hali ya huduma za uzazi wa mpango Mkoani Tanga katika Mkutano wa wenye lengo la kuendeleza juhudi za Serikali juu ya Uzazi wa mpango nchini.

 Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la JHPIEGO  Dkt. Dustan Bishanga

Viongozi wa Halmashauri na Wilaya kutoka Tanga leo waliohudhuria kikao chenye lengo la kuendeleza juhudi za Serikali juu ya uzazi wa mpango.

Picha ya pamoja ikiongonzwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akiwa na viongozi wa Halmashauri na Wilaya ya Tanga baada ya Mkutano wenye lengo la kuendeleza juhudi za Serikali juu ya masuala Ya uzazi wa mpango ulio chini ya JhPiego unaofadhiliwa na Melinda Gate.


WIZARA YA AFYA YATENGA BILIONI 14 KWA AJILI YA HUDUMA   UZAZI WA MPANGO

Na.WAMJW-Tanga
 
Viongozi na watendaji wakuu wa halmashauri ya Jiji la Tanga wametakiwa kuwa wabunifu katika kuhakikisha wanawafikia wanawake wengi wanaoishi mjini ili waweze kujiunga na huduma za uzazi wa mpango.
 
Wito huo umetolewa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akifungua mkutano uliowakutanisha Viongozi na watendaji wakuu wa Halmashauri ya Jiji,Wilaya ya Tanga Mjini pamoja na Wilaya ya korogwe wenye lengo la kuendeleza juhudi za uzazi wa mpango nchini.
 
Waziri Ummy alisema kwamba Serikali ya awamu ya tano imejipanga kutokomeza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga  hivyo imejipanga kuwafikia wananchi wengi ili kuweza kupunguza kwa asilimia 30 vifo vitokanavyo na uzazi.
 
“lazima muonyeshe utayari na umakini kama viongozi katika kuwekeza kwenye uzazi wa mpango, mkiwa wabunifu mtawawezesha kuwafikia akina mama wengi wa mjini, hata akina baba kwa kuwapa elimu ya kutosha na kufanya maamuzi ili wapange lini wanataka kuzaa,watoto wangapi na watofautiane kwa miaka mingapi”.Alisema Waziri Ummy.
 
Aidha, aliwataka viongozi kutumia fedha hizo kuziweka kwenye vitu endelevu ili mradi huo uongeze wanawake wengi kutumia njia za uzazi nchini.
 
“Msiweke mipango ya mardi huu kwenye semina bali mradi huu uwe njia ya kufungua miradi mingine kutoka kwa wadau wa maendeleo” alisema Waziri Ummy.
 
Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa Serikali kupitia Wizara ya afya kwa mwaka huu wa fedha 2018/2019 umetenga shilingi bilioni 14 kwa ajili ya afya ya uzazi wa mama na mtoto tofauti na miaka ya nyuma ambapo kabla Serikali ya awamu ya tano haijaingia madarakani wizara ilikua ikitenga shilingi bilioni 2 kwa ajili ya matumizi kitengo hicho.
 
Naye Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Bi.Kisa Kasongwe ambaye alimuakilisha Mkuu wa Mkoa wa Jiji la Tanga alisema halmashauri ya Jiji la Tanga ipo tayari kutoa ushirikiano na shirika hilo kwani mradi huo utaleta hali nzuri kwa akina mama pamoja na watoto wachanga.
 
Wakati huo huo Kaimu Mwakilishi Mkazi wa shirika la jhpiego Dkt.Dustan Bishanga alisema kuwa mradi huo unakuja kuongeza rasiliamali ambazo hazitoshi katika kusimamia  na kutekeleza katika uwekezaji wa uzazi wa mpango.
 
“Mradi huu utafanikiwa endapo viongozi  wa Jiji la Tanga  mtatekeleza  na kufanya mpango huu kufanikiwa hivyo mtapelekea tuwaletee mradi mwingine wa afya ya uzazi kwa vijana endapo mradi huu wa kwanza mtaufanikisha ipasavyo”.Alisema Dkt.Bishanga.
 
Mradi wa “Tupange pamoja” ulianzishwa mwaka 2016 na kutekelezwa na halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Arusha ambapo kwa jiji la Dar es Salaam walipatiwa shilingi milioni 250 kwa ajili ya kutekeleza uzazi wa mpango kwa halmashauri zote na hivi sasa unaanza kwa Jiji la Tanga.
 
Idadi ya akina mama wanaotumia uzazi wa mpango kwa Jiji la Tanga ni asilimia 31 ambapo kitaifa inatakiwa kufikia asilimia 45 hadi mwaka 2020 na vifo vya akina mama kwa halmashauri hii imepungua kutoka vifo 69 mwaka 2014 hadi vifo 45 kwa mwaka 2017.



0 on: "WIZARA YA AFYA YATENGA BILIONI 14 KWA AJILI YA HUDUMA UZAZI WA MPANGO"