Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Ijumaa, 6 Aprili 2018

TANZANIA YAPATA TAKRIBANI WAGONJWA WAPYA WA SARATANI 50,000 KILA MWAKA.

Shekhe wa Mkoa wa Dar es salaam Alhaj Musa Salum akiishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kujali Afya za wananchi, akiwa katika kikao cha kuhamasisha chanjo ya mlango wa kizazi kwa mabinti kilichoandaliwa na Wizara ya Afya kupitia mpango wa chanjo.

Askofu Wa kanisa la mito ya baraka Bruno Mwakibolwa akichangia hoja mbele ya Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu na viongozi wengine wa dini (hawapo kwenye picha)  wakati wa kikao kuhamasisha chanjo ya mlango wa kizazi kwa mabinti kilichofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akitoa mapendekezo mbele ya viongozi wa dini waliokutana mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa kikao cha kuhamasisha chanjo ya mlango wa kizazi.

Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi akimkaribisha Mhe. Ummy Mwalimu ili azungumze na viongozi wa dini.

Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo Dkt. Dafrossa Lymo akiwasilisha taarifa kuhusu masuala ya chanjo nchini mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Viongozi wa Dini (hawapo kwenye picha).

Viongozi wa dini ya Kikristo wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mhe.Ummy Mwalimu wakati wa kikao na viongozi wa dini zote cha kuhamasisha chanjo ya mlango wa kizazi.

Viongozi wa dini ya kiislamu wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mhe.Ummy Mwalimu wakati wa kikao na viongozi wa dini zote cha kuhamasisha chanjo ya mlango wa kizazi.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Sub wakati wa kikao kuhamasisha chanjo ya mlango wa kizazi kwa mabinti kilichofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiwa na viongozi wa dini wakati wa kikao kuhamasisha chanjo ya mlango wa kizazi kwa mabinti kilichofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.


Na WAMJW-Dar es salaam.

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa kila mwaka Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa wapya wa Saratani 50,000 huku Saratani ya mlango wa kizazi ikiongoza ikifuatiwa na saratani ya matiti na saratani ya ngozi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) wakati wa mkutano na viongozi wa dini, uliofanyika mapema leo katika ukumbi wa Serena jijini Dar es salaam.

“Kila mwaka Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa wa Saratani wapya 50,000, katika kila wagonjwa 100 wanaokwenda katika Hospitali ya Ocean Road wagonjwa 32 wanasaratani ya mlango wa kizazi, inafuatia saratani ya matiti ambayo takribani wagonjwa 12 katika wagonjwa 100, saratani ya tatu ni saratani ya Ngozi” alisema Mhe. Ummy Mwalimu.

Aliendelea kusema kuwa Saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti zinachukua takribani asilimia 45 ya wagonjwa wa saratani nchini, huku Saratani ya tezi dume ikiwa na asilimia 2.

Kwa upande mwingine Mhe. Ummy Mwalimu amewaomba viongozi wakuu wa madhehebu ya dini kuwahimiza wananchi kuwapeleka wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 14 kupata chanjo ya kuwakinga na saratani ya mlango wa kizazi inayotarajiwa kuzinduliwa tarehe 10 Aprili,2018 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam

Waziri Ummy amesema kwamba kama viongozi wa dini ni vyema kufikisha ujumbe huu kwa waumini wao na kuwaunga mkono ili kuweza kuwafikia wasichana laki 6 nchi nzima ili kuweza kuwaokoa na vifo vipatavyo asilimia 50 vitokanavyo na saratani nchini"idadi hii ni kubwa sana,hivyo juhudi na ushirikiano zaidi vinahitajika katika kupunguza vifo hivi.

Hata hivyo aliwatoa hofu viongozi hao pamoja na wananchi kwa ujumla kwamba chanjo hii haizuii binti kutopata watoto katika maisha yake ya baadae bali ni kinga dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi".  Kinga ni bora kuliko tiba, hivyo ni vyema tukashirikiana kuweza kuwaokoa mabint wetu na vifo".

Chanjo mpya ya kuwakinga wasichana wenye umri wa miaka 14 dhidi ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi itaanza kutolewa mara baada ya uzinduzi wa kitaifa tarehe 10 Aprili, 2018 na itahusisha mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar pia itatolewa kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya Serikali, binafsi na huduma mkoba kwenye shule na sehemu mbalimbali. Chanjo hii itatolewa mara mbili ili kupata kinga kamili(chanjo ya pili itatolewa baada ya miezi sita)

Kwa upande mwingine Mhe. Ummy mwalimu alimshukuru Mhe. Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuongeza bajeti ya dawa za Saratani kutoka shilingi Milioni 700 hadi Bilion 7 jambo lililosaidia sana katika matibabu ya Saratani.

“Nashukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kupandisha bajeti ya dawa za saratani kutoka shilingi Milioni 700 hadi Billion 7, leo nasimama kifua mbele, angalau katika wagonjwa 10, wagonjwa 7 watakwambia tumepata dawa bila malipo yoyote” alisema Mhe. Ummy Mwalimu.


0 on: "TANZANIA YAPATA TAKRIBANI WAGONJWA WAPYA WA SARATANI 50,000 KILA MWAKA."