Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumanne, 24 Oktoba 2017

BALOZI WA IRANI MH. MOUSA FARHANG ATETA NA WAZIRI WA AFYA MH. UMMY MWALIMU KATIKA OFISI NDOGO ZA WIZARA JIJINI DAR ES SALAAM.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu watatu kutoka kushoto akimsikiliza Balozi wa Irani nchini Tanzania Mh. Mousa Farhang mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam huku lengo la ugeni huo likiwa ni kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo hususani katika sekta ya Afya. Kulia mwa Barozi Mousa ni Dkt. Mahmoud.
Na WAMJWW
Balozi wa Irani nchini Tanzania Mh.Mousa Farhang mapema leo amemtembelea Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam, lengo likiwa ni kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili hususani katika nyanja za teknolojia na matibabu ya kibingwa.
Aidha Balozi Mousa amemtoa hofu Mh. Ummy na kumuahidi Irani itaendelea kushirikiana na Tanzania bega kwa bega katika kuhakikisha kwamba wanasukuma gurudumu la maendeleo hasa katika nyanja ya Afya kwa kuimarisha huduma za kibingwa.
Kwa upande mwingine Balozi Mousa ameishukuru Serikali yake ya Misri kwa kuisaidia Tanzania ikiwemo uchimbaji wa visima maeneo ya vijijini jambo lililosaidia kupunguza hadha ya maji kwa jamii hususani wanawake.
Hata hivyo Balozi Mousa Farhang ameahidi kuendeleza ushirikiano huo na Serikali ya Tanzania huku akiwataka wawekezaji kutoka Irani kuja kufanya uwekezaji mkubwa nchini hapa hususani katika viwanda vya dawa.
Nae Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu ameshukuru ugeni huo kutoka Irani ulio na tija kwa taifa la Tanzania huku akisisitiza na kuweka  mkazo wa ushirikiano huo katika uwekezaji wa chanjo, kutoa madawa,vifaa na vifaa tiba, ufadhili wa mafunzo ya muda mfupi kwa watoa huduma wa Tanzania na kujenga uwezo wa Ushirikiano katika maeneo ya utafiti wa tiba.

0 on: "BALOZI WA IRANI MH. MOUSA FARHANG ATETA NA WAZIRI WA AFYA MH. UMMY MWALIMU KATIKA OFISI NDOGO ZA WIZARA JIJINI DAR ES SALAAM."