Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo
tarehe 23 Oktoba, 2017 amekabidhi mashine 100 za tiba mgando (cryotherapy) na mashine 9 za upasuaji mdogo (LEEP) ambazo
zitatumika kwa ajili ya matibabu ya awali ya saratani kwa wanawake
watakaofanyiwa uchunguzi na kukutwa na mabadiliko ya awali ya saratani ya
mlango wa kizazi
Makabidhiano
hayo yamefanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara hiyo zilizopo Jijini Dar es
Salaam ambapo Mhe. Waziri Ummy amesema katika kuhakikisha tunaongeza
upatikanaji wa huduma za uchunguzi na matibabu ya awali ya Saratani ya Mlango
wa Kizazi, Wizara ya Afya imekuja na mkakati wa kuboresha huduma hizi kwa kununua mashine na vifaa hivyo ambavyo vimegharimu
kiasi cha shilingi bilioni moja na vitasambazwa katika mikoa 10 ikijumlisha
halmashauri 31 ambazo tumebaini zina vituo vichache vya kutolea huduma hizi ukilinganisha na Mikoa mingine.
0 on: "PICHA ZA BAADHI YA MATUKIO YAKUKABIDHI MASHINE ZA KUCHUNGUZA SARATANI."