Na.WAMJW.Dodoma
Taasisi ya Chakula na lishe nchini imetakiwa
kujikita katika kutoa elimu kwa umma ili wananchi waweze kujua faida ya kula
chakula bora na kuepukana na utapiamlo na udumavu
Hayo yamesemwa na Mwenyeketi wa kamati ya
Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii
Mhe. Peter Serukamba wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utendaji wa
shughuli za taasisi hiyo mjini Dodoma leo.
Mhe.Serukamba alisema bila elimu kwa umma
wananchi watakuwa wanatumia fedha nyingi kwa ajili ya matibabu kwa kuwa hali ya
udumavu ni mkubwa ,”watu wakiwa na chakula na lishe bora unakuwa na uhakika
hutougua hovyo na kupoteza fedha nyingi kwa ajili ya matibabu,lakini wakijua
wale mlo gani ambao ni sahihi hii itasaidia kutokomeza kabisa tatizo hili”
Aidha, alisema Tanzania haina tatizo la
chakula ila hawafahamu ni mlo gani sahihi wanapaswa kula hivyo kwa kutoa zaidi
elimu itakua ni kinga na itasaidia wananchi wasiugue
“Taasisi hii iboreshwe na mkishirikiana na
Tamisemi,wakulima na wasafirishaji wa mazao kupitia maofisa maendeleo ya jamii
mtawafikia wananchi wengi na hakutokuwa na vizazi vyenye udumavu na matatizo ya
akili.
Awali akiwasilisha taarifa ya utendaji wa
taasisi hiyo Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
dkt.Faustine Ndugulile alisema zaidi ya asilimia 35 ya vifo vya watoto wenye
umri wa chini ya miaka mitano nchini vinachangiwa na matatizo ya lishe duni na katika kipindi cha mwaka 199 hadi 2015/2016
vifo vya watoto vimepungua kutoka 147
hadi 67 kwa kila vizazi hai 1000.
“Serikali inafanya jitihada kubwa katika kumjenga mtoto ili akue vizuri kimwili
na kiakili kuanzia siku elfu moja za mwanzo za mtoto ambazo ni muhimu kwa
makuzi ya mtoto”.
Hata hivyo dkt.Ndugulile alisema hali ya
lishe nchini inaendelea kuimarika kutokana na kupungua kwa viwango vya
utapiamlo nchini kati ya mwaka 1992 na 2015.
Alisema udumavu (urefu wa umri) umepungua
kutoka asilimia 49.7 hadi 34.4 na mikoa inayoongoza ni Rukwa (56%) na Ruvuma
(44%) ,kwa upande wa ukondefu (uzito kwa urefu) kutoka asilimia 7.8 hadi 4.5 na
mikoa inayoongoza ni Zanzibar-Kusini Pemba na Kaskazini Pemba(9%),Manyara
(6.4%),Geita (6.2%),Kigoma (6%) na Morogoro (6.0%)
Kwa upande wa uzito pungufu alisema (uzito
kwa umri) kutoka asilimia 25.1 hadi 13.7 na mikoa inayoongoza ni Rukwa
(23%),Arusha (20%) pamoja na Kigoma (20%).
Vilevile,mwanamke mmoja kati ya kila
wanawake 10 walio katika umri wa kuzaa ana uzito pungufu (underweight) wakati
asilimia 18 wana uzito mkubwa (over weight) na asilimia 10 wana kiribatumbo(obesity).Mikoa
inayoongoza kwa kiribatumbo ni Zanzibar mjini Magharibi kwa 22%,Unguja Kusini
19%,Dar es Salaam 21%,Kilimanjaro 19% na Tanga 17%.
Naibu Waziri huyo aliahidi kuwa watajipanga
katika kutoa elimu ya afya kwa umma na kuwafikia wananchi wengi zaidi “bado
Watanzania hawajui kula lishe iliyokamilika na matumizi bora ya chakula.
0 on: "LISHE BORA KWA WATANZANIA BADO NI TATIZO, ASEMA MH. PETER SERUKAMBA"