Naibu Waziri wa Afya,maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
dkt.Faustine Ndugulile akiongea kwenye mkutano huo wa wataalamu wa
magonjwa ya figo nchini.Mkutano huo wa siku mbili unafanyika kwenye
Hotel ya Morena Mjini Dodoma na kuhudhuriwa na wataalamu mbalimbali
kutoka Hospitali nchini,Wadau wa Maendeleo pamoja na wataalamu wengine
kutoka nchi za Kenya,Sudan,India pamoja na Norway.
Makamu
wa Rais wa Chama cha wataalamu wa magonjwa ya Figo Tanzania (NESOT),
Dkt.Paschal Ruggajjo akiongea dhima kubwa ya mkutano huo ni teknolojia
ya upandikizaji wa viungo nchini ili kuweza kuhudumia wagonjwa takribani
milioni 23.
Baadhi ya Wataalamu wa magonjwa ya figo waliohudhuria mkutano
huo.Mkutano huo ni wa siku mbili ambapo watajadili dhana mbalimbali ya
ugonjwa wa figo ikiwemo kutoa elimu kwa umma ili kuweza kukabiliana na
magonjwa ya figo pamoja na upandikizaji.Tanzania imekua ikipeleka
wastani wa wagonjwa thelathini na tano(35) kwa mwaka nje ya nchi kwa
ajili ya kupandikiza figo na gharama ya kupandikiza nje ya nchi ikiwemo
India ni shilingi milioni 75 hadi 77 kwa mtu mmoja ikiwemo
kupandikiza,nauli pamoja na malazi
Makamu
wa Rais wa Chama hicho akimpa zawadi mmoja wa wataalamu wa figo ambaye
amefanya tafiti na kuwasilisha mada ya katika mkutano huo Profesa
Ainory Gesase ambaye ni mkufunzi wa Chuo cha Sayansi ya Tiba.
Picha ya pamoja ya Mgeni Rasmi wa mkutano huo Dkt.Ndugulile akiwa na
wataalamu wa figo nchini pamoja na wadau wengine wa ndani ya nchi na nje
ya nchi.
Naibu Waziri akisalimiana na washiriki wa Mkutano huo mara baada ya
ufunguzi.Dkt.Ndugulile alisema Serikali mgonjwa mmoja anahitaji wastani
wa shilingi za kitanzania 37,620,504 kwa mwaka kwa ajili ya kulipia
gharama za kusafisha damu nchini.
Mashine za kusafisha figo (Dialysis Machine) ambazo zimefungwa kwenye
hospitali nchini.Serikali imefunga mashine katika hospitali nchini
ikiwemo UDOM (10),Hospitali ya Muhimbili (42), Hospitali ya Rufaa
Mbeya(5), Hospitali ya Rufaa Bugando (10), KCMC(10),Hospitali ya Misheni
Serian(10),Hospitali ya NSK Arusha(5),TMK(10),Regency(15),
Hurbert
Kairuki(5), Aga Khan(10) na Access(10).Mashine hizo zina uwezo wa
kuhudumia wagonjwa 783 kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) na
391 kwa huduma ya malipo ya papo kwa papo(Picha zote na Wizara ya Afya).
0 on: "DKT. FAUSTINE NDUGULILE AFUNGUA MKUTANO WA NNE WA CHAMA CHA WATAALAMU WA FIGO."