Na WAMJWW
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu
aagiza Hospitali na Vituo vya Afya vyote vya Serikali nchini kuanzia
leo October 28 kutoa huduma ya uchunguzi wa Saratani kila siku wakati wa
kliniki ya mama na mtoto, sambamba na huduma hizi, kila mwezi vyatakiwa
kuwa na siku moja kwaajili ya kuchunguza na kufanya matibabu ya ugonjwa
wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti.
Ameyasema
hayo wakati alipofungua matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa
Saratani ya matiti, yalifunguliwa katika viwanja vya hospitali ya
Ocean Road mapema leo jijini Dar es salaam.
Aidha
Mh. Ummy ameipongeza kazi nzuri inayofanywa na Uongozi wa Hospitali ya
Ocean Road katika kutimiza majukumu yake ikiwemo kuongeza vitanda 40
mpaka vitanda 100 kwa gharama zao kwaajili ya wagonjwa wa saratani
pindi wanapopata huduma za matibabu ya Chemotherapy.
“Katika
kuwaunga mkono Serikali ya awamu ya tano ya Mh. Magufuli imewapatia
Bilioni 5 kwajili yakukamilisha mashine za kisasa za matibabu ya
Saratani kwa kutumia mionzi.” Alisema Mh. Ummy Mwalimu
Aidha
Mh. Ummy Mwalimu ametoa maelekezo kwa Uongozi wa Hospitali ya Ocean
Road kuwa wanatakiwa kwenda kwenye shule za Msingi na Sekondari ili
kuwajengea watoto uelewa kuhusu ugonjwa wa Saratani, lakini ni vipi
wataweza kujikinga na magonjwa yasiyo yakuambulizwa ikiwemo ugonjwa wa
Saratani.
Pia Mh. Ummy alitoa rai kwa wananchi wote
hususani wanawake kujitokeza kupima ugonjwa huo kwani unatibika endapo
itagunduliwa mapema,
Nae Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt
Grace Maghembe ambae pia alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam ,
ameipongeza Serikali ya awamu ya tano chini ya Raisi Dkt. John Pombe
Magufuli kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na
Watoto kwa kazi kubwa wanayoifanya ikiwemo kuongeza kwa bajeti ya Dawa ,
vifaa tiba vya uchunguzi na matibabu.
Kwa upande
mwingine Dkt. Grace Maghembe kwa niaba ya bodi ameahidi kuendelea
kufanya kazi kwa uaminifu na bidii kubwa katika kuhakikisha kwamba
wanakabiliana na ugonjwa huu wa Saratani kwa wananchi hasa wale wa hali
ya chini na kuahidi kuendelea kuboresha huduma hii.
“Niwaombe
wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam kwenda kupima Saratani kwani ni bure,
usisubiri mpaka kuugua, ukichelewa grarama zinaongezeka lakini pia
uwezekano wa kupona unakuwa ni mdogo”. Alisema Dkt Grace Maghembe
Aidha
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Ocean Road Dkt. Julius Mwaiselage
amemhakikishia Mh. Ummy Mwalimu kwamba upatikanaji wa dawa katika
Hospitali hiyo ni 80% na dawa za wagonjwa wengi zinapatikana kwa 100%,
ukilinganisha na 2015/2016 upatikanaji wa dawa ilikuwa 4% tu, jambo
ambalo lilikuwa ni changamoto kubwa na kufanya malalamiko ya dawa kuwa
makubwa sana katika hospitali hiyo, hivyo kuishukuru Serikali ya
Magufuli kwa niaba ya Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu.
Mwisho
Dkt. Julius Mwaiselage amemhakikishia Mh. Waziri kwamba Hospitali ya
Ocean Road ipo katika hatua ya Mwisho ya kuweka mashine mpya mbili
(Linear accerelators), hivyo zitasaidia kupunguza muda wa kusubiri kwa
wagonjwa kusubiri huduma , lakini kubwa kupunguza wagonjwa wanaokwenda
kutibiwa nje ya nchi.
0 on: "MH. UMMY AAGIZA HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA VYOTE VYA SERIKALI KUTOA HUDUMA YA UCHUNGUZI WA SARATANI."