Naibu Waziri Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine
Ndugulile akiwasilisha taarifa ya utendaji wa shughuli za Taasisi ya
Chakula na Lishe Tanzania(TFNC) mbele ya Kamati ya Bunge ya Huduma na
Maendeleo ya Jamiii inayoongozwa na Mwenyekiti wake Peter Serukamba(wa
kwanza kulia) leo mjini Dodoma,ambapo imeonekana tatizo la ulaji wa
chakula bora kwa Watanzania bado ni tatizo kubwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt.Vicent Assey akijibu maswali ya wajumbe wa kamati hiyo ambapo ilionekana licha ya uzalishaji chumvi kwa wingi bado kaya
zinazotumia chumvi yenye madini joto bado ipo chini kwa asilimia 30
kwenye Mikoa ya Simiyu,Mtwara na Lindi.wakati kiwango cha mahitaji ya
mwili ni asilimia 61 kwa takwimu za mwaka 2015/2016 hivyo kiwango hicho
kimepanda kutoka asilimia 47 cha mwaka 2010.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma na
Maendeleo ya Jamiii wakifuatilia kwa umakini uwasilishaji wa taarifa kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Faustine Ndugulile(Hayupo kwenye picha) leo jijini Dodoma.
0 on: " "