Na WAMJWW
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ahimiza weledi na kukemea vitendo vya baadhi ya Viongozi kuwachukulia hatua madaktari na badala
yake kuwataka wafuate utaratibu uliowekwa.
Mhe. Ummy aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa
Kongamano la 49 la Afya na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama Cha Madaktari.
Nae Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameliagiza Baraza la Mitihani kufanya uhakiki
haraka ili wataalamu wa Sekta za Afya wapangiwe vituo.
“Tangu tuingie madarakani
serikali imeweza kutoa vibali vya ajira mpya vipatavyo 3,410 kwa awamu
mbili, awamu ya kwanza vibali vya madaktari 258 na awamu ya pili vibali 3,150
kwa wataalamu wa kada ya afya na taratibu za ajira kwa wataalamu hawa 3150
zimekamilika na imebakia hatua ya uhakiki wa vyeti katika Baraza la Taifa la
Mitihani (NECTA)” alisema Mh. Samia Suluhu.
Makamu wa Rais aliwapongeza Chama cha Madaktari kwa
kuweza kuandaa Kongamano la 49 na kuweka historia ya kuandaa Makongamano tangu
mwaka 1965.
Kauli mbiu ya mwaka huu inayosema “ Malengo ya Maendeleo
Endelevu: Uweledi wa Kitaaluma na Utoaji Bora wa Huduma za Afya Nchini
Tanzania.” Mada hii ni muhimu sana katika kipindi hiki ambacho Serikali ya
Awamu ya Tano inatekeleza kwa vitendo wajibu wake wa kuhakikisha kuwa wananchi
wanapatiwa huduma za afya zenye viwango na zinazokidhi mahitaji.
0 on: "MH. UMMY AHIMIZA UTARATIBU UFUATWE ILI KUWACHUKULIA HATUA MADAKTARI."