Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo wakati akitoa tamko la Siku ya Figo Duniani, lililotolewa leo katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo kwenye picha) wakati akitoa tamko la Siku ya Figo Duniani, lililotolewa leo katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma. Wakwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dkt. Grace Maghembe na wamwisho ni Mwenyekiti wa Chama cha Magonjwa ya Figo nchini Dkt. Kisanga
SERIKALI YAOKOA BILION 3.4 KWENYE MATIBABU YA UGONJWA WA
FIGO
Na WAMJW-DOM.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Serikali imefanukiwa kuokoa kiasi
cha Shilingi Bilion 4.2 ambacho kingetumika katika matibabu kwa Wagonjwa wa
Figo nje ya Nchi.
Dkt. Ndugulile ameyasema hayo leo Machi 14 wakati akiongea
na Waandishi wa Habari katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma ikiwa ni
Siku ya Figo Duniani ambayo inaongozwa na kauli mbiu ya Afya ya figo kwa kila
mmoja kila.
Dkt. Ndugulile
amesema kuwa Serikali imeokoa
kiasi cha shilingi bilioni 4.2 ambacho kingetumika katika matibabu ya wagonjwa
80 mpaka 100 ambao wangepelekwa nje ya nchi kwaajili ya matibabu.
“Wagonjwa waliokwishapandikizwa figo
hapa nchini ni 42, kama tungewapeleka
wagonjwa nje ya nchi ingegharimu serikali kiasi cha shilingi bilioni 4.2
kwa idadi hiyo ya wagonjwa. 80 mpaka
100, wakati huduma hii hapa nchini inagharimu kiasi cha shilingingi milioni 21
kwa kila mgonjwa.” Alisema Dkt. Ndugulile
Aidha, Dkt, Ndugulile amesema kuwa miongoni
mwa sababu zinazochangia magonjwa ya figo ni pamoja na uzito wa kupindukia
(obesity), matumizi makubwa ya sigara, unywaji wa pombe, uvutaji wa
sigara,kutokufanya mazoezi na kunywa madawa kiholela hasa dawa za kupunguza
maumivu.
Aliendelea kusema kuwa, magonjwa ya
kisukari na shinikizo la damu ni magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha matatizo
ya figo, magonjwa haya yakitambuliwa mapema yanaweza kudhibitiwa kwa matibabu
na kuepusha madhara kwenye figo.
Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile
amesema kuwa Kufikia Desemba mwaka 2018, jumla ya vituo 28 vyenye jumla ya
wagonjwa 1050 vilikuwa vikitoa huduma ya usafishaji damu katika mikoa ya Dar es
Salaam, Mwanza, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro na Dodoma.
0 on: "SERIKALI YAOKOA BILION 4.2 KWENYE MATIBABU YA UGONJWA WA FIGO"