Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) akiteta jambo na Binti Mfalme Zahra Aga Khan (kushoto) mara baada ya kufungua awamu ya pili ya hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wakati wa hafla ya awamu ya pili ya upanuzi wa Hospitali ya aga Khan, Jijini Dar Es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya awamu ya pili ya upanuzi wa Hospitali ya aga Khan, Jijini Dar Es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wazari Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Jackline Vicent aliyejifungua mtoto Lois Ladislaus katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam alipotembelea wodi ya wazazi kabla ya kufungua awamu ya pili ya upanuzi wa haospitali hiyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimfariji mtoto Ilham Ally wakati alipotembelea wodi ya watoto kabla ya kufungua awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Machi 9, 2019. Mtoto Ilham amelazwa hospitalini hapo kwa matibabu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa amembeba mtoto, Claribel Mwakatumbula (1) wakati alipotembelea wodi ya watoto kabla ya kufungua awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Machi 9, 2019. Mtoto Claribel amelazwa hospitalini hapo kwa matibabu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akisimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) wakati alipotembela Hospitali ya Aga Khan.
Na WAMJW – Dar Es Salaam.
Serikail imetoa wito kwa Taasisi
binafsi zinatozoa huduma za afya nchini ikiwemo Mtandao wa Maendeleo wa Aga
Khan (AKDN) kuangalia upya gharama za tiba wanazotoza kwa wananchi ili wananchi
wengi waweze kunufaika na huduma bora za matibabu.
Hayo yamesemwa leo na Waziri
Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya upanuzi wa
Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar Es Salaam.
“Wito wangu ni kuwa watoa huduma
wote nchini waangalie upya gharama zinazotokwa katika huduma mbalimbali hususan
za matibabu” Amesema Waziri Mkuu na kuendelea kusema kuwa gharama zikiwa kubwa
hazitawanufaisha wananchi hasa wale wenye kipato cha chini.
Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali
inatambua gharama kubwa za uwekezaji na uendeshaji wa shughuli za afya nchini unafanywa
na sekta binafsi katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya nchini.
“Mojawapo ya malengo ya
Serikai ni kutoa misamaha ya kodi kwa baadhi ya taasisi zisizokuwa za
kiserikali ikiwemo Aga Khani ili kuwezesha huduma zinazotolewa kuwa nafuu” Amesema
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa.
Hata hivyo Waziri Mkuu amesema
kuwa Serikali imekuwa ikiwahamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya (NHIF) ili kuhakikisha wananchi wote wanapata uhakika wa matibabu.
"Nitoe wito kwa taasisi zote
zisizo za kiserikali kuunga mkono jitihada za Serikali na kuhakikisha wananchi wote wananufaika na
huduma zetu kupitia mfumo huu bila kubaguliwa” amesema Waziri Mkuu, Mhe. Kassim
Majaliwa
Aidha Waziri Mkuu ameutaka
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kukamilisha majadiliano na Hospitali ya
Aga Khan ili kuhakikisha huduma za NHIF zinapatikana hospitalini hapo.
Kwa upande wake Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameupongeza
uongozi wa AKDN kwa kukamilisha ujenzi wa jengo hilo ambalo litatumika kutolea
huduma bora za za afya kwa wananchi.
Waziri Ummy amesema kuwa Jiji
la Dar Es Salaam bado lina uhitaji wa huduma bora za afya hasa kwa huduma za
malazi ya wagonjwa na kwa upanuzi wa hospitali hiyo sasa wanaongeza idadi ya
vitanda katika hospitali zilizopo Jijini Dar Es Salaam.
Aidha Waziri Ummy ameupongeza
uongozi wa Hospitali ya Aga Khani
kupitia mtandao wake kwa kutoa mafunzo kwa taasisi za afya na elimu hivyo kuongeza
ufanisi katika utoaji wa huduma kupitia mafunzo wanayopata wataalam.
Naye Balozi wa Ufaransa nchini, Balozi Frederic
Claiver amesema awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali hiyo utasaidia kuboresha
utoaji wa huduma za afy nchini.
Balozi Clavier amesema Ufaransa itaendelea
kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha inatimiza mkakati wake wa kukuza
uchumi kutoka wa chini kwenda wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025.
Mwisho
0 on: "WAZIRI MKUU AITAKA AGA KHAN KUPITIA UPYA GHARAMA ZA MATIBABU WANAZOTOZA KWA WANANCHI."