Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumamosi, 16 Machi 2019

WAGONJWA WATANO WAPANDIKIZWA FIGO BENJAMIN MKAPA

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa na Daktari Bingwa wa magonjwa ya Figo kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Charles Shija

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (Wakwanza kushoto) akiwa katika kikao na Madaktari bingwa kutoka shirika la Tokushukai kutoka nchi ya Japan baada yakufanikisha upandikizaji wa figo kwa kushirikiana na Madaktari kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Kikao cha Madaktari bingwa kutoka shirika la Tokushukai kutoka nchi ya Japan na kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa, kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile baada yakufanikisha upandikizaji wa figo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akiwa na Madaktari bingwa kutoka shirika la Tokushukai kutoka nchi ya Japan na Wataalamu kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma baada yakujionea upandikizaji wa figo wenye mafanikio.

Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma


WAGONJWA WATANO WAPANDIKIZWA FIGO BENJAMIN MKAPA

Na WAMJW - DOM

Hospitali ya  Benjamin Mkapa imefanikiwa kupandikiza Figo jumla ya Wagonjwa saba tangu ilipoanza kufanya huduma hiyo kwa kushirikiana na Madaktari kutoka shirika la afya la Tokushukai lilopo nchi ya Japan.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto   wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za kibingwa za magonjwa ya Figo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Dkt.  Ndugulile amesema kuwa Idadi ya wagonjwa waliokwishapandikizwa figo hapa nchini ni 43, ambapo 38 wamepatiwa huduma hiyo kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili na wagonjwa watano(5) hospitali ya Benjamin Mkapa

"Hivi navyoongea tayari mgonjwa mmoja amekwishapandikizwa figo na ameshatoka salama, yupo anaendelea kuangaliwa, lakini wana mpango wa kuwafanyia wengine wawili tutapokuwa tumekamilisha hili tutakuwa na wagonjwa saba ambao wamefanyiwa hospitali hii" alisema Dkt. Ndugulile.

Dkt. Ndugulile aliendelea kusema kuwa, Serikali imelenga kuhakikisha kwamba inawajengea uwezo Wataalamu wa ndani kufanya upasuaji  wa kibingwa ili waweze kuwahudumia Watanzania bila msaada kutoka Wataalamu wa nje.

"lengo na kusudio ni kuhakikisha kwamba tunajenga uwezo wa ndani wa kuweza kufanya upasuaji huu" Alisema Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeokoa zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 4.2 ambacho kingetumika katika matibabu ya wagonjwa 80 mpaka 100 ambao wangepelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

“Wagonjwa waliokwishapandikizwa figo hapa nchini ni 42, kama tungewapeleka  wagonjwa nje ya nchi ingegharimu serikali kiasi cha shilingi bilioni 4.2 kwa idadi hiyo ya wagonjwa.  80 mpaka 100, wakati huduma hii hapa nchini inagharimu kiasi cha shilingi milioni 21 kwa kila mgonjwa.” alisema Dkt. Ndugulile

Aidha, Dkt. Ndugulile amewashukuru Wataalamu kutoka shirika la Tokushukai kutoka nchi ya Japan kwa kujitoa na kuja kuwajengea uwezo Wataalamu wa ndani hali iliyosaidia kupunguza kiasi kikubwa cha fedha ambacho hutumika kwa ajili ya matibabu kwa wagonjwa wanaoenda kutibiwa nje.

"Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania nimepita kuwashukuru na kuwapongeza,  kwa sababu badala ya kutusaidia sisi samaki, wenzetu wa Japan wameamua kutupatia sisi mishipi na kutufundisha jinsi ya kujua naamini ujuzi huu utatusaidia sana " alisema Dkt. Ndugulile.

Mwisho.

0 on: "WAGONJWA WATANO WAPANDIKIZWA FIGO BENJAMIN MKAPA"