Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu (kushoto) akitoa dawa za Kifua Kikuu kwa Bw. Abbas Sudi
alipotembelea Hospitali ya Mbagala Jijini Dar Es Salaam kujionea hali ya
utoaji huduma za matibabu ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu na kutoa Tamko la
Serikali katikabkuadhimisha Siku ya Kifua Kikuu Duniani amnayo
huadhimishwa Tarehe 24 Machi kila Mwaka.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu (kushoto) akitoa dawa za Kifua Kikuu kwa Bi. Aisha Rashid
alipotembelea Hospitali ya Mbagala Jijini Dar Es Salaam kujionea hali ya
utoaji huduma za matibabu ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu na kutoa Tamko la
Serikali katikabkuadhimisha Siku ya Kifua Kikuu Duniani amnayo
huadhimishwa Tarehe 24 Machi kila Mwaka.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu (kushoto) akiangalia zawadi ya nguo aliyopewa na Taasisi ya
Mukukite inayojishughulisha kutoa huduma za matibabu ya ugonjwa wa kifua
kikuu.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
(wa kati kati) akipokea maelezo kutoka kwa mtaalam kuhusu uchugnguzi wa
ugonjwa wa Kifua Kikuu alipotembelea Hospitali ya Mbagala Jijini Dar Es
Salaam
Wananchi waliojitokeza kumsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (hayupo pichani) alipotembelea
Hospitali ya Mbagala Jijini Dar Es Salaam na kutoa Tamko la Siku ya
Kifua Kikuu Duniani.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akisema jambo na wananchi (hawapo pichani) alipotembea Hospitali
ya Mbagala Jijini Dar Es Salaam na kutoa tamko la Siku ya Kifua Kikuu
duniani.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaviva pindi alipofanya ziara na kujionea huduma za matibabu ya ugonjwa wa Kifua Kikuu katika Hospitali ya Mbagala Jijini Dar Es Salaam
Na WAMJW - DSM
SERIKALI imeendelea kuboresha huduma za matibabu ya kifua
Kikuu kwa kuongeza vituo vya kutolea huduma za matibabu sambamba na
kuongeza vifaa tiba, ikiwa ni jitihada za Serikali kutokomeza ugonjwa wa
Kifua Kikuu (TB) nchini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu leo wakati alipofanya ziara ya
kukagua hali ya utoaji huduma za kifua Kikuu na kutoa tamko kuhusiana
na ugonjwa huo katika Hospitali ya Mbagala Jijini Dar es salaam.
"Huduma za matibabu ya Kifua Kikuu (TB) sugu zimesogezwa
karibu kwa wananchi, ambapo kwa sasa tunazo hospitali 93 za kutibu Kifua
Kikuu sugu ikilinganishwa na mwaka 2015 ambapo, huduma za matibabu
zilikuwa zinapatikana katika Hospitali ya Kibong'oto pekee " amesema
Waziri Ummy.
Pia, Waziri Ummy amesema katika kila Watanzania 100,000
Watanzania 269 wanahisiwa kuwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu, huku watu 70
wanafariki kila siku kutokana ugonjwa wa Kifua Kikuu ambapo ni sawa na
watu watatu hufariki kila saa.
"watu 70 kila siku kutokana na ugonjwa wa Kifua Kikuu,
kwahiyo kila saa ni sawa na watu watatu wanafariki kutokana na ugonjwa
wa Kifua Kikuu ambao unatibika " alisema Waziri Ummy.
Waziri Ummy amesema takribani wagonjwa 154,000
wanaokadiriwa kuugua ugonjwa wa Kifua Kikuu wanapaswa kufikiwa na
kuingizwa katika mpango wa matibabu kila mwaka ili kuutokomeza ugonjwa
huu nchini.
Waziri Ummy ameendelea kusema kuwa Tanzania ni miongoni mwa
nchi 30 Duniani zenye kiwango kikubwa cha wagonjwa wa Kifua Kikuu,
inakadiriwa kuwa wapo wagonjwa takribani 154,000 ambao huugua ugonjwa wa
kifua Kikuu kila mwaka.
Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa Mgonjwa wa Kifua Kikuu
ambae hajaanza matibabu anaweza kuambkiza Kati ya watu kumi hadi watu 20
kwa mwaka, hivyo jitihada za makusudi zinatakiwa kuendelea kuchukuliwa
ili kutokomeza ugonjwa huu nchini.
"ifahamike kuwa mgonjwa wa kifua Kikuu ambae hajaanza
matibabu anaweza kuambukiza kati ya watu kumi hadi watu ishirini kwa
mwaka, hivyo tunalojukumu kubwa lakuhakikisha tunawafikia wote wanaougua
ili tuweze kuzuia maambukizi mapya ya Kifua Kikuu" amesemaWaziri Ummy
Mbali na hayo, Waziri Ummy amesema kuwa kitaifa
tunakadiliwa kuwa wapo wagonjwa wa Kifua Kikuu sugu takribani 200 na
kati yao, wagonjwa 167 sawa na 84% walianzishiwa matibabu, huku akitoa
wito kwa wagonjwa wengine kujitokeza kupata matibabu.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaviva
amemuomba Waziri Ummy kuona ulazima wa kuipanua Hospitali ya Mbagala,
ili kurahisisha utoaji huduma za Afya, kwani takribani wanawake 67 mpaka
70 hujifungua kwa siku.
"Wakina mama wanaojifungua hapa ni wengi sana, kwa Mfano
jana tu wakina mama 67 wamejifungua, siku nyingine wanafika 70 mpaka 80,
hivyo tunahitaji ipanuliwe hospitali hiyo " alisema Mhe. Felix Lyaviva
Nae Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mbagala Dkt. Dk Ally
Mussa amesema kuwa kutokana na maboresho makubwa ya hospitali kumekuwa
na ongezeko kubwa la wagonjwa hadi kufikia wagonjwa 1700 kwa siku,
kumekuwa na maboresho makubwa ya huduma za mama na mtoto, maboresho ya
huduma za uchunguzi wa magonjwa (maabara za kisasa)
"kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa baada ya maboresho
mengi katika huduma za Afya za hospitali, kumekuwa na ongezeko kubwa la
wagonjwa hadi kufikia wagonjwa 1700 kwa siku" alisema Dkt. Dk Ally Mussa
0 on: "SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA KIFUA KIKUU (TB)"