Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akitoa mfano kupitia kadi ya Kliniki, namna gani Mfumo utafanyakazi kwa kutumia kishikwambi, wakati akipokea majokofu ya
kutunzia chanjo na vishikwambi (tablets) kwaajili ya kukusanyia taarifa
katika vituo vya Afya hapa nchini, tukio limefanyika katika Ofisi ndogo
za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy
Mwalimu akipokea vishikwambi (tablets) kwaajili ya kukusanyia taarifa
katika vituo vya Afya hapa nchini, kutoka kwa Mkuu wa Masuala ya Afya
UNICEF Kyaw Aung, (Wakwanza kushoto) tukio limefanyika katika Ofisi
ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam. Pembeni kwa Waziri Ummy ni
Meneja wa Mpango wa chanjo Taifa Dafrosa Lyimo.
TAMKO LA WAZIRI WA AFYA MAENDELEO YA
JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO MHE. UMMY A. MWALIMU (MB), WAKATI WA UPOKEAJI WA MAJOKOFU YA KUTUNZIA CHANJO NA
VISHIKWAMBI KWA AJILI YA KUKUSANYA TAARIFA ZA CHANJO KATIKA VITUO VYA KUTOLEA
HUDUMA ZA AFYA HAPA NCHINI TAREHE 22.02.2019, D’ SALAAM.
Ndugu
Wanahabari,
Naomba nichukue fursa hii kumshukuru
mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kutuwezesha kukutana hii leo katika hafla
muhimu.
Ndugu
Wanahabari,
Kama mnavyofahamu, Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, ilikusudia kuwa
kila kijiji kiwe na zahanati na kila kata iwe na kituo cha afya kwa nia ya
kuzileta na kusogeza huduma za afya karibu zaidi na wananchi. Kati ya huduma
hizo muhimu ni pamoja na upatikanaji wa chanjo mbalimbali kwa ajili ya kuzuia
magonjwa mbalimbali yakiwamo ugonjwa kupooza unaosababishwa na virusi ya Polio,
ugonjwa wa kifaduro na donda koo, surUu rubella, kansa ya mlango wa kizazi,
n.k. Chanjo hizi hutunzwa, kusafirishwa na kutolewa kwa walengwa zikipitia
mfumo wa mnyororo baridi toka zinakotengenezwa hadi kituo cha kutolea huduma.
Aidha, Wizara hutunza na kufuatilia takwimu mbalimbali za chanjo zinazoonyesha
maendeleo ya utoaji huduma kwa kutumia mtandao wa komputa kote nchini.
Ndugu
Wanahabari,
Napenda kuutarifu umma wa Tanzania kuwa, Serikali
kwa kushirikiana na shirika la Gavi, imefanikiwa kununua jumla ya majokofu 1,385 yenye thamani ya shilingi bilioni 13,991,270,300 (serikali
imechangia 20% na Gavi 80%) kwa ajili ya kuimarisha mnyororo baridi wa utunzaji
wa chanjo katika vituo vya kutolea huduma za afya hapa nchini. Majokofu 1,190 yanatumia nishati ya jua na kila
jokofu lina thamani ya shilingi milioni 10,879,000
(USD 4,730) na majokofu 195
yanatumia umeme, na kila jokofu lina thamani ya shilingi milioni 5,361,000 (USD 2,331). Vilevile
Serikali na shirika la Gavi imenunua jumla ya vishikwambi (tablets) 1,249
vyenye gharama ya shilingi bilioni 1,598,720,000 kwa ajili ya kukusanya na
kuhifadhi taarifa za chanjo kwa njia ya mtandao, na kila kishikwambi kina
thamani ya shilingi milioni 1,280,000.
Ndugu
Wanahabari,
Majokofu na vishikwambi tunavyopokea leo
ni awamu ya kwanza, ambapo mapema mwezi Mei tutapokea jumla ya vishikwambi 2100
venye thamani ya shilingi bilioni 2,688,000,000 na mwishoni mwa mwaka huu,
tutapokea awamu nyingine ya majokofu (kati ya 800-1000) yenye thamani ya shilingi bilioni 11,533,357,820 (USD
5,014,503) na kufikia asilimia zaidi 80 ya mahitaji ya majokofu na
vishikwambi katika vituo vyote hapa nchini.
Ndugu
Wanahabari,
Majokofu haya ya kutunzia chanjo
yatasambazwa na kufungwa katika vituo vipya na vituo vyenye majokofu yenye
teknolojia iliyopitwa na wakati. Ifahamike kuwa, majokofu haya yanayotumia
teknolojia ya kisasa ambapo, nishati ya jua inatumika kutoa ubaridi na
hayahitaji kutumia betri, hivyo kuziondolea gharama halmasahuri za ununuzi wa
gesi kila mwezi au manunuzi ya betri, kama yalivyo majokofu mengine yanayotumia
nishati ya jua.
Ndugu
Wanahabari,
Halmashauri zote za Tanzania Bara pamoja
na Wilaya za Zanzibar zitapokea majokofu haya kwa awamu kuu mbili. Awamu ya
kwanza itahusisha mikoa 15 ambayo ni Dodoma, Geita, Kagera, Kigoma, Lindi,
Tanga, Mara, Mbeya, Mtwara, Mwanza, Shinyanga, Songwe, Unguja, Pwani na
Singida. Na awamu ya pili itahusisha mikoa iliyobaki.
Ndugu
Wanahabari,
Kama nilivyoeleza awali, Wizara ya Afya
kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tamisemi, kupitia Mpango wa Taifa wa Chanjo
imeanza kukusanya taarifa za chanjo kwa kutumia mifumo ya kielektroniki, ambapo
katika ngazi ya kituo kishikwambi kitatumika kukusanya taarifa za chanjo
kupitia mfumo wa kielektroniki wa leja ya Watoto (Tanzania electronic immunization Registry - TimR).
Ndugu
Wanahabari,
Taarifa
zilizokusanywa zitatumwa wilayani katika mfumo ujulikanao kama “Vaccine Information Management System
(VIMS)” na kutumwa katika Mfumo Mkuu wa Kielektroniki wa Wizara (District
Health Information System DHIS-2.
Ndugu
Wanahabari,
Mfumo wa VIMS tayari umeanza kutumika
katika mikoa na wilaya zote nchini na mfumo wa TimR kwa sasa unatumika mikoa ya
Arusha, Tanga, Kilimanjaro na Dodoma. Wizara inakusudia kusambaza mfumo wa TimR
katika mikoa ya Mwanza, Morogoro, Mtwara, Geita, Njombe na Dar es Salaam kabla
ya kufika mwezi Aprili mwaka huu.
Ndugu
Wanahabari,
Vile vile, ili kuhakikisha ufanisi na
ufuatiliaji wa utendaji kazi wa majokofu ya kuhifadhia chanjo, Wizara ya Afya
kwa kushikiana na wadau wa shirika la JSI na Nexleaf kwa ufadhili wa Gavi,
inatarajia kufunga vifaa vya kupima na kufuatilia halijoto katika vituo
takribani 5,000 kati ya vituo zaidi ya 7,000 kote nchini.
Ndugu
Wanahabari,
Vifaa
hivi vinamuwezesha Afisa Chanjo kujua utendaji kazi wa jokofu ikiwa ni pamoja
na kujua halijoto ya jokofu katika vituo vya huduma za afya bila ya kulazimika
kufika katika kituo husika. Vifaa hivi vinatuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS)
pindi halijoto inapopanda au kushuka.
Ndugu
Wanahabari,
Tanzania itakuwa ni miongoni mwa nchi
chache duniani zenye mfumo huu wa kisasa wa kufuatilia utendaji kazi wa
majokofu ya chanjo na kuhakikisha watoto wanapatiwa chanjo zenye ubora wa hali
ya juu wakati wote.
Ndugu
Wanahabari,
Kwa namna ya pekee, napenda kuchukua fursa
hii kuwapongeza watoa huduma za chanjo hapa nchini, Waganga Wakuu wa Mikoa na
Wilaya, pamoja na Waratibu wa Chanjo wa Mikoa na wilaya zote kwa kuwezesha nchi
yetu ya Tanzania kufikisha viwango vya juu vya utoaji wa huduma za chanjo.
Ndugu
Wanahabari,
Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa
mwaka 2017 nchi yetu ilifikisha kiwango cha uchanjaji cha asilimia 98 na
kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya tatu duniani kwa viwango vya juu vya utoaji wa
huduma za chanjo. Mafanikio ya huduma za chanjo hapa nchini, pamoja na afua
zingine, imeiwezesha nchi kufikia malengo ya milenia (MDG 4) kwa kupunguza vifo
vya Watoto chini ya miaka mitano kwa theluthi 2/3.
Ndugu
Wanahabari,
Napenda kuchukua fursa hii kuwasisitiza
Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri pamoja na Waratibu wa Chanjo katika ngazi
za mikoa na halmashauri, kuhakikisha kuwa watoa huduma wote wa chanjo
wanafundishwa jinsi ya kufanya matengenezo madogomadogo ya majokofu (planned
preventive maintenance) ili kuhakikisha kuwa vifaa hivi vinadumu kwa muda mrefu
kama ilivyokusudiwa. Ni matarajio ya Wizara na Serikali kuwa, vifaa hivi
vitaongeza upatikanaji wa huduma za chanjo karibu na wananchi na hivyo
kupunguza idadi ya Watoto ambao hawajafikiwa na huduma za chanjo.
Ndugu
Wanahabari,
Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru
wadau wote wa chanjo kwa kuendelea kutoa ufadhili na kuhakikisha kuwa kila
mtoto anafikiwa kwa huduma za chanjo.
Ndugu
Wanahabari,
Mwisho kabisa, napenda kuwahimiza wazazi
na walezi wote hapa nchini kuwapeleka watoto wao katika vituo vya kutolea
huduma za afya ili wakapate chanjo mbalimbali zinazotolewa kukinga magonjwa
anuai. Halikadhalika, ninawahimiza mabinti wote waliotimiza umri wa miaka 14
wajitokeze ili kupata chanjo ya kuwakinga dhidi ya maambukizi ya saratani ya
mlango wa kizazi kwani chanjo hii inatolewa bila malipo yoyote katika vituo vya
serikali na binafsi. Dozi ya kwanza ya chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa
kizazi inatolewa wakati wowote binti anapofikisha umri wa miaka 14 na dozi ya
pili inatolewa miezi sita (6) baada ya dozi ya kwanza.
ASANTENI
KWA KUNISIKILIZA
MGAWANYO WA MAJOKOFU
S/N
|
MKOA
|
WILAYA
|
IDADI YA MAJOKOFU
|
1
|
DODOMA
|
BAHI
|
9
|
KONDOA DC
|
21
|
KONGWA DC
|
20
|
MPWAPWA DC
|
28
|
JUMLA
|
78
|
2
|
GEITA
|
BUKOMBE DC
|
6
|
CHATO DC
|
14
|
GEITA DC
|
17
|
GEITA TC
|
7
|
MBOGWE DC
|
12
|
NYANG’WALE DC
|
8
|
JUMLA
|
64
|
3
|
KAGERA
|
BIHARAMURO
|
6
|
BUKOBA DC
|
25
|
KARAGWE DC
|
23
|
KYERWA DC
|
22
|
MISENYI DC
|
21
|
MULEBA DC
|
24
|
NGARA DC
|
20
|
BUKOBA MC
|
7
|
JUMLA
|
148
|
4
|
KIGOMA
|
BUHIGWE DC
|
6
|
KAKONKO DC
|
4
|
KASULU TC
|
5
|
KIBONDO DC
|
3
|
KIGOMA DC
|
14
|
KIGOMA MC
|
1
|
UVINZA DC
|
10
|
JUMLA
|
43
|
5
|
LINDI
|
KILWA DC
|
23
|
LINDI DC
|
25
|
LINDI MC
|
5
|
NACHINGWEA DC
|
20
|
LIWALE DC
|
21
|
RUANGWA DC
|
11
|
JUMLA
|
105
|
6
|
MARA
|
BUNDA DC
|
10
|
BUTIAMA DC
|
18
|
MUSOMA DC
|
25
|
MUSOMA MC
|
11
|
SERENGETI DC
|
28
|
TARIME DC
|
25
|
RORYA
|
28
|
JUMLA
|
145
|
7
|
MBEYA
|
BUSOKELO DC
|
10
|
CHUNYA DC
|
21
|
KYELA DC
|
18
|
MBARALI DC
|
18
|
MBEYA CITY
|
3
|
MBEYA DC
|
20
|
RUNGWE DC
|
21
|
JUMLA
|
111
|
8
|
MTWARA
|
MASASI DC
|
29
|
MASASI TC
|
7
|
MTWARA MC
|
6
|
MTWARA DC
|
10
|
NANYAMBA
|
11
|
NANYUMBU DC
|
15
|
NEWALA DC
|
14
|
NEWALA TC
|
9
|
TANDAHIMBA DC
|
6
|
JUMLA
|
107
|
9
|
MWANZA
|
BUCHOSA DC
|
17
|
ILEMELA DC
|
15
|
KWIMBA DC
|
27
|
MAGU DC
|
11
|
MISUNGWI DC
|
26
|
SENGEREMA DC
|
16
|
UKEREWE DC
|
18
|
NYAMAGANA DC
|
16
|
JUMLA
|
146
|
10
|
PEMBA
|
CHAKE CHAKE
|
8
|
MICHEWENI
|
10
|
MKOANI
|
11
|
WETE
|
8
|
JUMLA
|
37
|
11
|
SHINYANGA
|
KISHAPU DC
|
25
|
MSALALA DC
|
16
|
SHINYANGA DC
|
17
|
SHINYANGA MC
|
10
|
USHETU DC
|
17
|
KAHAMA TC
|
7
|
JUMLA
|
92
|
12
|
SONGWE
|
ILEJE DC
|
26
|
MBOZI DC
|
28
|
MOMBA DC
|
23
|
SONGWE DC
|
15
|
TUNDUMA TC
|
4
|
JUMLA
|
96
|
|
|
|
|
13
|
UNGUJA
|
KASKAZINI A
|
5
|
KASKAZINI B
|
8
|
KATI
|
14
|
KUSINI
|
5
|
MAGHARIBI
|
14
|
MJINI
|
12
|
JUMLA
|
58
|
14
|
PWANI
|
BAGAMOYO DC
|
8
|
CHALINZE DC
|
22
|
JUMLA
|
30
|
15
|
SINGIDA
|
ITIGI DC
|
5
|
|
|
|
|
16
|
TANGA
|
BUMBULI
|
9
|
HANDENI DC
|
19
|
KILINDI DC
|
14
|
KOROGWE DC
|
16
|
KOROGWE TC
|
2
|
LUSHOTO DC
|
8
|
MKINGA DC
|
14
|
MUHEZA DC
|
24
|
PANGANI DC
|
14
|
JUMLA
|
120
|
|
|
|
|
|
|
JUMLA KUU
|
1385
|
MGAWANYO WA
VISHIKWAMBI
S/No
|
MKOA
|
IDADI YA VISHIKWAMBI
|
1
|
DAR ES SALAAM
|
300
|
2
|
MWANZA
|
350
|
3
|
MTWARA
|
100
|
4
|
NJOMBE
|
236
|
5
|
GEITA
|
143
|
6
|
MOROGORO
|
120
|
|
JUMLA
|
1249
|