Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
HALI YA HUDUMA ZA AFYA NCHINI KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2018
4.MAPAMBANO DHIDI YA VVU/UKIMWI, MALARIA NA KIFUA KIKUU
#Mapambano Dhidi ya VVU/UKIMWI
Katika
kuhakikisha kuwa Tanzania ina kuwa salaama kutokana na maambukizi mapya
ya VVU, kuwapunguzia makali ya virusi vya UKIMWI na kuzuia waathirika
wasishambuliwe na magonjwa nyemelezi, Sekta ya Afya ikishirikana na
Wadau inatekeleza mpango wa Kimatatifa wa 90-90-90.
#
Mpango huo unazitaka nchi kuwatambua wenye VVU kwa asilimia 90 ifikapo
mwaka 2020 miongoni mwa watanzania wote wanaoishi na VVU wanaokadiriwa
kuwa 1,500,000 nchi nzima, hatua ya pili ni kuhakikisha kuwa asilimia 90
ya wanaogundulika kuwa na VVU wanaanza dawa za ARV na kati ya wanaoanza
dawa za ART asilimia 90 wanaimarisha kinga zao za mwili ili kuzuia
wasishambuliwe na magonjwa nyemelezi.
#Hadi
kufikia mwisho wa Mwezi Septemba 2018, Wizara kupitia Mpango wa Taifa
wa Kudhibiti UKIMWI iliweza kuwaandikisha katika tiba ya kufubaza virusi
vya UKIMWI, jumla ya wagonjwa 1,087,382 kati ya hao watoto walikuwa ni
58,908.
#Idadi hii ya
wagonjwa walio katika tiba ni asilimia 72 ya watu 1,500,000
wanaokadiriwa kuishi na VVU nchini kote ikilinganishwa na asilimia 70
mwaka 2017.
#Lengo la 90
ya pili ni kuhakikisha asilimia 90 ya waliokutwa na VVU wanaanzishiwa
dawa za ART, lengo hili limefikiwa ambapo Watanzania 1,068,282 sawa na
asilimia 98.2 wanatumia dawa za ART.
#
Na lengo la 90 ya tatu ni kuhakikisha asilimia 90 ya wanaoanzishiwa
dawa za ARV kinga zao za mwili zinaimarika (Viral road suppression),
ambapo lengo hili limefikiwa kwa asilimia 87.
# Mapambano dhidi ya Malaria nchini
mwaka 2018 idadi ya 5,769,837 waligundulika kuwa na ugonjwa wa malaria ikilinganishwa na watu 5,595,916 mwaka 2017.
#
Matumizi ya kipimo cha haraka cha malaria (mRDT) yaliiongezeka kutoka
asilimia 79 mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 86 mwaka 2018
#Mapambano dhidi ya Kifua Kikuu Nchini
Wizara
kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya afya iliendelea na mapambano
dhidi ya ugonjwa wa kifua kikuu ambapo katika mwaka 2018 jumla 47,967
waligundulika kuwa na vijidudu vya Kifua kikuu ikilinganishwa na
wagonjwa 44,714 waliogunduliwa mwaka 2017.
#Huduma kwa Wagonjwa wa TB wanaogundulika kuwa na HIV 2017 na Mwaka 2018
Katika
kuimarisha tiba dhidi ya Kifua Kikuu na VVU, wagonjwa wote
wanaogundulika kuwa na kifua kikuu, hupimwa kama wanamaambukizi ya VVU.
*Hii
inawawezesha wagonjwa kutibiwa TB na VVU. Katika kipindi cha mwaka 2018
asilimia 99 ya wagonjwa waliogundulika kuwa na maambukizi ya Kifua
Kikuu walipimwa VVU ambapo asilimia 31 kati yao walikutwa na VVU
ikilinganishwa na mwaka 2017 ambapo asilimia 97 ya wagonjwa wa TB
waliopima VVU kati yao asilimia 34 waligundulika kuwa na VVU.
#Kwa wale waliogundulika kuwa na VVU asilimia 93 walianzishiwa dawa za ARV.
#Kiwango
cha maambukizi ya VVU kwa wagonjwa walio na TB kiko juu sana hivyo
Sekta ya Afya inahakikisha kuwa wagonjwa wote wanaogundulika kuwa na
VVU/UKIMWI wanaanzishiwa dawa za ART.
#Kitaifa zaidi ya asilimia 93 ya wagonjwa wote wa TB wliogundulika kuwa na VVU walianzishiwa dawa za ART
Imetolewa na;
Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
25/01/2019
0 on: "4.MAPAMBANO DHIDI YA VVU/UKIMWI, MALARIA NA KIFUA KIKUU"