Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akiongozana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara ya kukagua Maendeleo ya ujenzi wa Wizara ya Afya iliyo katika mji mpya wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akipokea taarifa ya Maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Afya wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi huo, unaoendelea katika mji mpya wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma, pembeni yake ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akitoa maelekezo kwa mkandarasi (hayupo kwenye picha) wakati akikagua Maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Afya, unaoendelea katika mji mpya wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma, katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, wakwanza kushoto ni Mwakilishi kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.
Picha ya baadhi ya majengo ya Wizara ya Afya yanayoendelea kujengwa katika mji mpya wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma.
WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA KATIKA UJENZI WA MJI MPYA WA SERIKALI IHUMWA DODOMA.
Na WAMJW - DOM
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo amefanya ziara katika mji mpya wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ihumwa jijini Dodoma ili kujionea maendeleo ya shughuli za ujenzi ambazo zinatarajia kumalizika mwishoni mwa mwezi Januari 2019,
Katika ziara hiyo Mhe. Majaliwa amemwagiza Mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi, na kuongeza idadi ya wafanyakazi ili kuhakikisha anamaliza kazi yake ifikapo Januari 31, 2019 na kukabidhi kwa Wizara ya Afya ili waendelee na majukumu yao ya kuboresha Sekta ya Afya.
Aidha, amemwagiza Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu kusimamia kikamilifu ujenzi wa jengo hilo kila siku ili kuhakikisha ujenzi wa jengo hilo unakamilika ndani ya muda waliokubaliana, kwa ubora na ufanisi wa hali ya juu.
"Mhe. Waziri hawa wanatakiwa kusimamiwa kila siku, hili ndio jengo lililochini, ukiondoa lile la Waziri Mkuu ambalo wameanza kazi jana, hili ndio lipo chini na ndio la wale wale Mzinga, Kamanda lisije lilakuahibisha hili" alisema Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Mbali na hayo, Mhe. Majaliwa amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula na Wakurugenzi wa kuanza kufanya usafi katika maeneo yate ili kupendezesha mazingira ili wanapomaliza ujenzi wa jengo hilo na usafi uwe tayari ili shughuli ziendelee ndani ya muda.
0 on: "WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA KATIKA UJENZI WA MJI MPYA WA SERIKALI IHUMWA, DODOMA"