HALI YA HUDUMA ZA AFYA NCHINI KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2018
1. Afya ya Uzazi,Mama na Mtoto
#Katika
mwaka 2018, jumla ya wajawazito 2,086,930 walihudhuria na kuandikishwa
kliniki, ikilinganishwa na wajawazito 2,009,879 mwaka 2017. Mwongozo wa
utoaji huduma za afya ya uzazi na mtoto unaelekeza wajawazito kuanza
huduma mapema kabla ya majuma 12 ya ujauzito na kuhudhuria kliniki
angalau mara nne katika kipindi cha ujauzito ili waweze kupata huduma
zote muhimu.
#Asilimia 25
ya wajawazito nchini waliweza kufanya *hudhurio la kwanza kliniki kabla
ya majuma 12* ikillinganishwa na asilimia 18 mwaka 2017.
#Ongezeko
la *wajawazito kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya*
Mwaka 2018 asilimia 73 ya wajawazito walijifungulia katika vituo vya
kutolea huduma za afya ikilinganishwa na asilimia 70 mwaka 2017.
#Huduma
ya *kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto*
imeendelea kutolewa ambapo mwaka 2018 asilimia 97 ya wajawazito walipima
VVU ikilinganishwa na asilimia 95 mwaka 2017.
#Katika
wajawazito waliopima VVU, asilimia 3.9 waligundulika kuwa na VVU na
kati ya hao waliogundulika asilimia 99 walianzishiwa dawa za ART. Katika
mwaka 2017, Asilimia 4.2 ya wajawazito waligundulika kuwa na maambukizi
ya VVU na kati yao asilimia 99 walianza dawa za ART.
#Hali
ya upatikanaji wa chanjo kwa watoto nchini imeendelea kuwa katika
kiwango cha juu kwa asilimia 85 katika kipindi cha mwaka 2018 na mwaka
2017
Imetolewa na ;
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
Chanzo: District Health Information System 2 (DHIS2).
0 on: "HALI YA HUDUMA ZA AFYA NCHINI KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2018"