Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya Wabunge na viongozi
wa Wizara wakati wa kikao cha Bunge cha huduma za jamii, jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiwasilisha taarifa ya Mpango wa taifa wa kudhibiti
Ukimwi katika kikao cha kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii jijini
Dodoma.
Mkurugenzi wa Bohari kuu ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu (Wapili
kushoto) akifuatilia uwasilishwaji wa taarifa ya Mpango wa taiga wa
kudhibiti Ukimwi ulofanywa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine
Ndugulile katika kikao cha kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii jijini
Dodoma.
Baadhi ya Wabunge wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa ya Mpango wa
taiga wa kudhibiti Ukimwi ulofanywa na Naibu Waziri wa Afya Dkt.
Faustine Ndugulile katika kikao cha kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii
jijini Dodoma.
Wabunge na Viongozi wa wizara na baadhi ya taasisi zake wakiwa katika
Kikao cha kamati ya Bunge ya huduma za jamii kilichofanyika leo jijini
Dodoma.
52% YA WATANZANIA WAMEPIMA VVU
Na WAMJW-DOM
SERIKALI
imesema kuwa Watanzania wapatao 2,405,296 hadi kufikia tarehe Oktoba
2018 walipima VVU kupitia Kampeni ya ‘Furaha Yangu’ ambao ni sawa na
asilimia 52 ya lengo la kuwapima watanzania wapatao 4,638,639 hadi
Desemba 2018.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katika kikao cha kamati ya bunge ya
huduma za jamii kilichofanyika leo jijini Dodoma.
“Hadi
kufikia tarehe 31 Oktoba 2018, jumla ya watanzania 2,405,296 walikuwa
wamepima VVU kupitia Kampeni ya ‘Furaha Yangu’ ambao ni sawa na asilimia
52 ya lengo la kuwapima watanzania wapatao 4,638,639 hadi Desemba 2018”
Alisema Dkt. Ndugulile
Dkt.
Ndugulile aliendelea kusema kuwa Miongoni mwa wote waliopima, wanaume
walikuwa ni asilimia 44 huku wanawake wakiwa ni asilimia 56. Kati yao,
watu 70,436 (2.9%) walikutwa na maambukizi ya VVU, ambapo wanaume 27,984
(2.6%) na wanawake ni 42,452 (3.2%).
Aidha,
Dkt. Ndugulile alisema kuwa Wizara kwa kushirikiana na Tume ya
Kudhibiti UKIMWI Tanzania na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
imeandaa mapendekezo ya marekebisho ya Sheria ya UKIMWI namba 28 ya
mwaka 2008 ili kupendekeza marekebisho yatayoruhusu upimaji Binafsi wa
VVU (HIV Self-testing).
Mbali
na hayo Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali ipo katika mchakato wa
kupunguza umri ya kupima VVU kwa ridhaa ya mzazi au mlezi kutoka miaka
18 hadi 15, hii ni kutokana na kasi ya maambukizi kuongezeka katika umri
huo.
Pia, aliendelea
kusema kuwa Wizara imeendelea kutoa huduma za Tohara ya Kitabibu kwa
Wanaume kwa lengo la kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mwanamke kwenda
kwa mwanaume katika mikoa ya kipaumbele ambayo haina utamaduni wa
kutahiri na ina kiwango kikubwa cha maambukizi ya VVU.
“Hadi
kufikia Septemba, 2018 Mikoa kumi na saba (17) inatoa huduma za Tohara
ambayo ni Iringa, Njombe, Tabora, Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Ruvuma,
Shinyanga, Simiyu, Mwanza, Geita, Kagera, Singida, Kigoma, Mara na
Morogoro” Alisema Dkt. Ndugulile
Aidha,
Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali inaendelea kutoa Huduma ya tohara
kwa wanaume bila malipo katika vituo vya huduma za afya na kupitia
huduma mkoba ngazi ya jamii ambapo hadi kufikia Septemba 2018, jumla ya
watu 3,702,387 wamefanyiwa tohara nchini ambao ni wanaume, vijana na
watoto wa kiume.
Mbali na
hayo Dkt. Ndugulile alisema kuwa Hadi kufikia mwisho wa Desemba 2018,
Wizara iliweza kuwaandikisha katika huduma za tiba na matunzo watu
wanaoishi na VVU wapatao 1, 087,382. Watu 68,927 waliandikishwa katika
kipindi cha robo ya mwaka cha Juai hadi Septemba 2018 ambapo kati yao,
1,068,282 wanatumia dawa za kupunguza makali ya VVU, ambapo watoto
walikuwa ni 58,908.
Idadi
ya vituo vinavyotoa huduma na matunzo vimeongezeka hadi kufikia 6,206
Desemba 2018. Sawa na asilimia 72.7 ya vituo vyote vya huduma za afya
nchini. Miongoni mwa vituo hivyo, vituo kamili vinavyotoa huduma za tiba
na matunzo ni 2,103 wakati vituo vinavyotoa huduma ya afya mama na
mtoto (RCH) ni 4,103.
MWISHO.
0 on: "52% YA WATANZANIA WAMEPIMA VVU - SERIKALI"