HALI YA HUDUMA ZA AFYA NCHINI KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2008
3.UPATIKANAJI WA DAWA MUHIMU KATIKA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA NCHINI
#Hali
ya upatikanaji wa Dawa muhimu katika vituo vya kutolea huduma za afya
nchini imeendelea kuimarika tokea kuingia madarakani kwa Serikali ya
awamu ya Tano.
#Serikali
imeongeza bajeti ya dawa kutoka Shilingi Milioni 31 mwaka 2015/16 hadi
kufikia Shilingi milioni 251 mwaka 2016/17 na Shilingi 270 mwaka
2018/19.
#Hali hii
imewezesha takribani vituo vyote vya kutolea huduma nchi kuwa na dawa
zote muhumu na kuwezesha wananchi kupata dawa karibu na maeneo
wanayoishi.
# Mwaka 2015
hali ya upatikanaji wa dawa ilikuwa asilimia 46 kutokana na ongezeko la
bajeti pamoja na usimamizi mzuri wa usambazaji dawa, mwaka 2016/17 hali
upatikanaji wa dawa iliongezeka na kufikia asilimia 89 na mwaka 2018
ilifikia asilimia 94 kwa dawa dawa muhimu zinazosambazwa na Bohari ya
Dawa nchini (MSD).
Imetolewa na;
Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
24/01/2019
0 on: "UPATIKANAJI WA DAWA MUHIMU KATIKA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA NCHINI"