Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akifuatilia mchoro unaoonesha namna mfumo wa huduma za Afya unavofanya kazi katika nchi za Asia, Kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi kuu ya Sera ya huduma za Afya
Mhe. Koji Fujimoto akitoa maelezo ya ziada kwa Waziri Ummy.
Balozi wa Japan Tanzania Mhe.
Shinichi Goto akiwa na Mjumbe kutoka Balaza la Huduma za Afya serikali ya Japan, wakifuatilia Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu pindi walipofanya mkutano wa kujadili namna gani Serikali ya Japan inaweza kuisaidia Tanzania katika maendeleo ya Sekta ya Afya.
Maafisa kutoka Wizara ya Afya, wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Waziri wa
Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu pindi walipofanya
mkutano wa kujadili namna gani Serikali ya Japan inaweza kuisaidia
Tanzania katika maendeleo ya Sekta ya Afya.
Wajumbe kutoka Japan na Tanzania, wakiwa katika mkutano mkutano wa kujadili namna gani Serikali ya Japan inaweza kuisaidia
Tanzania katika maendeleo ya Sekta ya Afya, mkutano huo umeongozwa na Waziri wa
Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Japan Tanzania Mhe.
Shinichi Gotowakati baada ya Mkutano wa kujadili namna gani Serikali ya Japan inaweza kuisaidia
Tanzania katika maendeleo ya Sekta ya Afya.
Picha ya pamoja ikiongozwa na aziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Balozi wa Japan Tanzania Mhe.
Shinichi Goto wakiwa na wajumbe wengine wa Serikali ya Tanzania na nchi ya Japan, baada ya kikao cha kujadili namna gani Serikali ya Japan inaweza kuisaidia
Tanzania katika maendeleo ya Sekta ya Afya.
Na WAMJW - DSM
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo akutana na ugeni ulioongozwa na Mkurugenzi Msaidizi Ofisi kuu ya Sera ya huduma za Afya Mhe. Koji Fujimoto aliyeongozana na Balozi wa Japan Tanzania Mhe. Shinichi Goto na wajumbe wengine, Lengo ni kuangalia ni namna gani Japan inaweza kusaidia Nchi ya Tanzania katika Sekta ya Afya, hususani katika kupunguza vifo vya mama na mtoto, kuzuia magonjwa yasiyo yakuambukiza, Saratani na magonjwa ya Moyo n.k
Waziri Ummy ameishukuru Serikali ya Japan kwa ushirikiano wanayoipa nchi ya Tanzania, huku akiakisisitiza kwamba licha ya changamoto zilizopo katika Sekta ya Afya, Nchi ya Tanzania inaendelea kuimarika kwa kasi sana katika Sekta ya Afya, mfano upatikaji wa kutosha wa Dawa muhimu, Vifaa na Vifaa tiba, kupungua kwa vifo vya mama na mtoto, upatikanaji wa chanjo n.k
Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya Serikali ya Japan Bw. Koji Fujimoto amemshukuru Waziri Ummy kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuboresha na kuimarisha Sekta ya Afya na ameahidi kuendeleza ushirikiano ili kuisukuma guruduma la Maendeleo katika Sekta hiyo.
0 on: "WAZIRI UMMY AKUTANA NA UGENI KUTOKA JAPAN"