WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoani Tanga (CCM) akizungumza na
watumishi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wakati wa ziara
yake ya Jimbo la Tanga
watumishi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa ziara
yake ya Jimbo la Tanga
Na WAMJW - TANGA
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto
Ummy Mwalimu amewaonya madaktari nchini kuacha tabia za kuwa madalali
wa maduka ya dawa kwa kuwaandikia wagonjwa dawa mara mbili mbili huku
akiwaambia kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua kali.
Huku
akiagiza hospitali za Rufaa kote nchini kuhakikisha zinakuwa na maduka
ya dawa litakalokuwa na uhakika wa dawa zote muhimu ili kuondosha kero
hiyo na kuondoa mianya ya madaktari kudalalia dawa kwenye maduka
binafsi.
Ummy ambaye pia
ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani wa Tanga aliyasema hayo wakati
akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo na kauli
hiyo inatokana na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi ambao
walimsimamisha nje ya hospitali hiyo kabla ya kukutana nao.
Wananchi
hao ambao walikuwa wakisubiri kuingia hospitalini hapa walimueleza kero
hiyo ambapo alisema mbali na kero hiyo aliwaagiza madaktari nchi nzima
kuhakikisha wanazingatia mwongozo wa kutoa dawa au matibabu ili kuepusha
lawama kwa wagonjwa wa kubadilishiwa dawa na kila daktari.
Akiwa
kwenye eneo hilo ambalo ni maalumu kwa ajili ya kupumzikia wananchi
ambao wanakwenda kuwatazama wagonjwa wao kabla ya kuingia hospitalini
hapo ndipo wananchi hao walipoamua kumueleza kilio hicho ambacho
kimekuwa kikiwaumiza muda mrefu sana na kumuomba akishughulikie.
“Kwa
kweli hii sio sawa kabla ya hapa nimepata wasaa wa kuzungumza na
wananchi nje ya geti lakini kilio chao kikubwa ni kutokuridishwa na
huduma tunazozitoa likiwemo suala la mgonjwa kuandikiwa dawa na kila
daktari hii sio sawa naaagiza madaktari acheni kuwa madalali wa maduka
ya dawa na sitaki kusikia hili siku nyengine “Alisema Waziri Ummy
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti mbele ya waziri huyo Mmoja wa wananchi Mussa Jangwa
alisema kwamba kwenye hospitali hiyo kumekuwa na changamoto kubwa
ambazo wanakumbana nazo ni kila daktari anayeingia wodini anaandika dawa
zake.
Alisema kwamba
hatua hiyo imepelekea kuingi gharama kubwa huduma bado ni changamoto
kutokana na kutumia fedha nyingi kutokana na kuwepo kuandikiwa dawa kila
wakati na kulazimika kwenda kununua
“Mh
Waziri tunashukuru kwa kuja na tungeomba viongozi wengine waige mfano
wako hapa hospitali ya Bombo kuna tatizo kubwa sana unapo na mgonjwa
wodini unapokuja daktari wa kwanza naandika dawa na mwengine akipita
anaandika dawa kwenye zamu yake sasa mgonjwa hajui anunue zipo na
ghamara zinakwenda “Alisema Mussa.
Alisema
wakati wanapoandikiwa dawa hizo wanaelekezwa duka la kwenda kununulia
huku wakitumia fedha nyingi ndani ya siku nne jambo ambalo limechangia
kujikuta wakiwa hawana la kufanya zaidi ya kubaki kuingia gharama
zisizokuwa za msingi huku mgonjwa akiwa bado hajatumia akizoandikiwa na
hali yake ni mbaya.
“Unapozungumzia
jambo la afya ni uhai wa binadahamu nichukue fursa hii kukupongeza
kutembelea hospitali hii isiwe ni wewe tu viongozi wote wafanye ziara
kama wewe huduma za afya bombo bado changamoto kubwa sana “Alisema
Naye
kwa upande wake Pili Nzoya Alisema wakati mwengine daktari anaweza
kupita wodini na kumuandikia mgonjwa dawa nyingi wakati ni za kununua na
kila wakati wamekuwa wakifanya hivyo na kupelekea kuwepo kwa usumbufu
mkubwa kwao.
Awali naye
mkazi mwengine Amina Mrisho alimueleza Waziri Ummy kwamba wamekuwa
wakiandikiwa dawa wakati bado nyengine walizokuwa nazo hawajazimaliza
kitendo ambacho kinawapa wakati mgumu na kujikuta wakiingia hasara.
Alisema
kwamba jambo ambalo limekuwa likiwashangaza ni kuandikiwa dawa na
daktari halafu wanabadilishiwa dawa nyengine jambo ambalo ni hasara kwao
huku wagonjwa wao wakiwa kwenye hali mbaya na baadae mgonjwa
anafariki.
“Kwa mfano Mh
Waziri umeandikiwa dawa leo za sh.40,000 kabla haujazimaliza
unaandikiwa nyengine hili ni tatizo ambalo limekuwa likituumiza sisi
wananchi tunaomba utusaidie “Alisema.
Hata
hivyo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita alikiri kuwepo
kwa changamoto hiyo lakini walikuwa wanafanya kwa nia njema lakini kama
tukiwabaini ambao walikuwa wanafanya kwa nia binafsi tutawachukulia
hatua.
0 on: "WAZIRI UMMY AWAONYA MADAKTARI..."