Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akielezea jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu hali ya Huduma za Afya mwaka 2018, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akielezea jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu hali ya
Huduma za Afya mwaka 2018, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Wizara
ya Afya jijini Dodoma.Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakar Kambi.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Bw. Macha akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa Waandishi wa Habari wakati wa wakati akitoa tamko mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu hali ya
Huduma za Afya mwaka 2018, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Wizara
ya Afya jijini Dodoma.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali wakifuatilia tamko kuhusu hali ya
Huduma za Afya mwaka 2018 kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu tukio lililofanyika katika ukumbi wa Wizara
ya Afya jijini Dodoma.
SEKTA YA AFYA YAENDELEA KUPAA - SERIKALI
Na WAMJW - DOM
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Sekta ya Afya nchini yaendelea kukua kwa kasi, kutokana na Serikali kuendelea kuboresha Huduma kwa Wananchi zikiwemo upatikanaji wa Dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi, huduma za chanjo, huduma za afya ya uzazi na mtoto na Huduma za Dharura.
Waziri Ummy ameyasema hayo wakati akitoa tamko mbele ya Waandishi wa Habari na baadhi ya viongozi wa Wizara, kuhusu hali ya
Huduma za Afya mwaka 2018, katika ukumbi wa Wizara
ya Afya jijini Dodoma.
Waziri Ummy amesema kuwa Katika mwaka 2018, jumla ya wajawazito 2,086, 930 walihudhuria na
kuandikishwa Kliniki, ikilinganishwa na wajawazito 2,009,879 Mwaka 2017, huku mwongozo wa utoaji huduma za afya ya uzazi na mtoto unaelekeza
wajawazito kuanza huduma mapema kabla ya majuma 12 ya ujauzito na
kuhudhuria kliniki angalau mara nne katika kipindi cha ujauzito.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa, Katika kipindi cha mwaka 2018 jumla ya watoto 1,568,832 walizaliwa
ikilinganishwa na Watoto 1,498,488 mwaka 2017, huku wakipatiwa
huduma mbalimbali za chanjo ili kuzuia magonjwa yanayowaathiri Watoto
ikiwemo ugonjwa Kupooza, Kuharisha, Pepopunda, Pneumonia, homa ya ini na
Surua.
"Katika kipindi cha mwaka 2018 hali ya chanjo kwa Watoto nchini
imeendelea kuwa katika kiwango cha juu zaidi ya asilimia 85 ya kiwango
kilichowekwa na Shirika la Afya Duniani kama inavyoonyeshaa katik hapa
chini" Alisema Waziri Ummy.
Hata hivyo Waziri Ummy amesema mwaka 2018 kumetokea jumla ya vifo 20,087 ikilinganishwa na vifo 19,693
mwaka 2017, huku Katika kipindi cha miaka yote miwili 2017 na 2018, homa ya
mapafu imeongoza kwa kusababisha vifo, ambapo kwa mwaka 2017, imechangia asilimia 18.2 ya vifo vyote na mwaka 2018 imechangia
kwa asilimia 12.9 ya vifo vyote.
Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa Mwaka 2018, ugonjwa usio wa kuambukiza
(shinikizo la damu) umejitokeza katika magonjwa 10 yanayoongoza kwa
kusababisha vifo ambapo umechangia vifo kwa asilimia 1.9 ya vifo vyote.
Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amesema kuwa Hali ya upatikanaji wa Dawa muhimu katika vituo vya kutolea huduma za
afya nchini imeendelea kuimarika, hii ni kutokana na Serikali kuongeza bajeti ya dawa
kutoka Shilingi Milioni 31 mwaka 2015/16 hadi kufikia Shilingi milioni
251 mwaka 2016/17 na Shilingi 270 mwaka 2018/19.
Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa hali ya upatikanaji wa Damu Salama ambapo katika kipindi cha mwaka 2018, huku jumla ya chupa za damu salama 307,835 sawa na asilimia
85.5 ya lengo zilikusanywa ikilinganishwa na chupa 233,933 mwaka 2017, huku akiwahasa Wananchi kujitokeza kuchangia damu ili kuendelea kuokoa maisha ya wahitaji.
"Chupa zote 307,835 zilizokusanywa zilipimwa makundi ya damu pamoja na
magonjwa makuu manne ambayo ni Ukimwi (HIV,) Homa ya Ini B na C (HBV,
HCV) na Kaswende (Syphilis). Jumla ya chupa 262,283 sawa na asilimia
85.3 zilikuwa salama na kusambazwa katika hospitali kwa ajili ya
wagonjwa wenye uhitaji wa damu." Alisema Waziri Ummy.
Hata hivyo Waziri Ummy amesema kuwa, katika mwaka 2018 jumla watu 47,967 waligundulika kuwa na vijidudu vya Kifua
kikuu ikilinganishwa na wagonjwa 44,714 waliogunduliwa mwaka 2017., huku akisisitiza kuwa tatizo la ugonjwa wa Kifua Kikuu limeendelea kuwepo takribani mikoa
yote nchini.
kwa upande mwingine, Waziri Ummya amesema kuwa, hadi kufikia Desemba 2018, jumla ya vituo vya kutolea
huduma za Afya vilifikia 7,768 kutoka vituo 7,435 mwaka 2017 sawa na
ongezeko la vituo 333 kwa mwaka, amedai kuwa Serikali ilikuwa
inamiliki asilimia 71 ya vituo vya kutolea huduma; Mashirika ya dini
asilimia 12, Taasisi za Serikali asilimia 3 na vituo
binafisi asilimia 15.
Sambamba na hilo, waziri Ummy amesema kuwa, hadi kufikia Desemba mwaka 2018, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ulikuwa
na jumla ya wanachama 899,654 na ikihudumia jumla
ya wanufaika 4,219,192 sawa na asilimia 8 ya Watanzania wote.
MWISHO.
0 on: "SEKTA YA AFYA YAENDELEA KUPAA - SERIKALI"