Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. faustine Ndugulile akikagua Dawa alizoandikiwa mgonjwa katika Wodi ya wanawake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma, ikiwa ni ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya katika Hospitali hiyo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya Dkt. Dorothy Gwajima
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma, akiwa katika ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya bora kwa Wananchi.
Katika ziara hiyo Dkt. Ndugulile ameuagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha vifaa vyote vilivyoharibika vinatengenezwa na kuanza kufanya kazi mara moja.
Kwa upande mwingine ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha wanatumia Fedha vizuri katika kufanya maboresho ya majengo ya Hospitali hiyo, ikiwemo kutumia Forced account katika ujenzi huo.
Pia, Dkt. Ndugulile ameuagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha kila mtoa huduma za Afya anaandika muda kwa usahihi aliomuhudumia mgonjwa kuanzia anapopokelewa, anapofanyiwa matibabu mpaka anapoandikiwa dawa jambo litalorahisisha kubaini mtenda kosa endapo mgonjwa atapata tatizo.
Aidha, Serikali imeahidi kuwapa gari la kubebea wagonjwa katika Hospitali hiyo ili kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika endapo gari hilo litakuwepo ikiwemo vifo vya mama na mtoto.
Mbali Na hayo Dkt. Ndugulile amewapongeza Watoa Huduma za Afya katika Hospitali hiyo kwa kazi nzuri wanayofanya huku akiwatia moyo kuwa Serikali inafahamu mchango wao na itaendelea kuboresha mahitaji yao.
#TunaboreshaAfya
0 on: "SERIKALI YAAHIDI KUTOA GARI LA KUBEBEA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA RUVUM"