Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 14 Januari 2019

DKT. NDUGULILE AITAKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA KUANZA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA

Mhe. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitembelea eneo la kuchoma taka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakati alipofanya alipoitembelea kuona hali ya utoaji wa huduma za afya. Kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Ibenzi Ernest.

Mhe. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua dripu aliyowekewa mgonjwa (hayupo pichani) wakati alipotembelea Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma kukagua hali ya utoaji wa huduma za afya.

Mhe. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua daftari la kutunza kumbukumbu za wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma wakati alipotembelea Hospitali hiyo kukagua hali ya utoaji wa huduma za afya. Kulia ni muuguzi wa zamu Mary Shayo akitoa ufafanuzi.

Mhe. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua jalada aliloandikiwa mgonjwa kwenda kununua dawa nje ya Hospitali.

Mhe. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wananchi waliofika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma kupata huduma mbalimbali za afya.
Na. WAMJW DODOMA

Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameutaka uongozi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma kuhakikisha inaanza kutoa huduma za kibingwa ili iendane na hadhi ya kuwa hospitali ya rufaa.

Dkt. Ndugulile amesema hayo leo katika kikao cha majumusho ya ziara aliyoifanya hospitalini hapo mbele ya viongozi na watumishi wa Hospitali hiyo baada ya kuona maagizo aliyoyatoa katika ziara ya kushtukiza aliyoifanya mwezi Septemba mwaka jana yametekelezwa.

“Tunataka huduma nyingine zisizohitaji rufaa zianze kutolewa katika vituo vingine badala ya kuleta kesi zote katika Hospitali ya rufaa ya mkoa, kesi zinazotakiwa kufika hapa ni zile zilizoshindikana katika hospitali za wilaya zote”. Amesema Dkt. Ndugulile.
 
Kufuatia hatua hiyo ameitaka hospitali hiyo kuacha kutibu kesi za magonjwa madogo madogo kama Malaria, kuharisha na mengineyo badala yake yakatibiwe katika hospitali za wilaya na vituo vya afya ili kupunguza msongamano wa wagonjwa hospitalini hapo.

Aidha, Dkt. Ndugulile amesema mfumo wa rufaa kwa wagonjwa katika hospitali hiyo bado haujakaa vizuri kutokana na wingi wa wagonjwa walioko wodini hususani jengo la mama na mtoto ambao wengi wao hawahitaji huduma za kibingwa.

“ Nilikua nasikiliza takwimu tulipopita jengo la mama na mtoto naona bado mfumo wa rufaa haujakaa vizuri, ilitakiwa sehemu ya mzigo huu ianze kubebwa na vituo vingine vya afya ikiwepo kituo cha afya cha Makole, hapa zije kesi ambazo ujauzito wa mama umeshindikana au kuhatarisha maisha ndiyo waje hapa”.

Ili kuepuka hali hiyo, Naibu waziri huyo amesema serikali imeanza kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo ambapo hospitali za wilaya 67 zinatarajiwa kujengwa nchini kote, katika mkoa wa Dodoma itajengwa Hospitali ya wilaya ili iweze kusaidia kutoa huduma za matibabu kwa magonjwa ya kawaida.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma Dkt. Ibenzi Ernest amempongeza Naibu Waziri kwa kuitembelea hospitali hiyo mara kwa mara na kumuhakikisha huduma za afya zinatolewa katika ubora unaohitajika kukidhi vigezo vilivyowekwa na serikali ili kuwaridhisha wagonjwa wanaofika hospitalini hapo.

0 on: "DKT. NDUGULILE AITAKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA KUANZA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA"