Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la
watoto wenye magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya JKCI jijini Dar
es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimjulia hali mtoto wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la
watoto wenye magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya JKCI jijini Dar
es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akimjulia hali mtoto aliyefika kupata matibabu katika Taasisi ya Moyo JKCI wakati alipofanya ziara ya kukagua
maendeleo ya ujenzi wa jengo la
watoto wenye magonjwa ya moy.
SERIKALI YAIONGEZEA UWEZO JKCI
Na WAMJW-DSM
SERIKALI
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imeiongezea uwezo wa kutoa huduma Taasisi ya Moyo ya JKCI kwa kuimarisha
jengo la watoto wenye magonjwa ya moyo ambalo litakuwa na uwezo wa
kubeba vitanda 32 kutoka vitanda 11 hapo mwanzo.
Ameyasema
hayo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo
alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa jengo la
watoto wenye magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya JKCI jijini Dar
es salaam.
“Katika jengo
hili kulikuwa na msongamano mkubwa sana wa watoto, sasa hivi jengo hili
likikamilika litakuwa na vitanda 32 kutoka vitanda 11, hivyo kulifanya
jengo hilo kuwa na vitanda vya watoto tu” alisema Waziri Ummy.
Waziri
Ummy amesema kuwa katika jengo hilo kutakuwa na Vyumba maalumu kwaajili
ya Wagonjwa wanaohitaji huduma na uangalizi maalumu 15 (ICU) kwaajili
ya watoto tu, badala ya rika zote kupata huduma hiyo katika chumba
kimoja, kama ilivyokuwa hapo mwanzo, jambo litalosaidia kuokoa maisha ya
watoto wanaohitaji uangalizi maalum.
“kutakuwa
na Vyumba maalumu kwaajili ya Wagonjwa wanaohitaji huduma na uangalizi
maalumu 15 kwaajili ya watoto tu, maana yake tutakuwa tumeokoa maisha
ya watoto ambao wanahitaji uangalizi maalumu, kwasababu watoto wanaweza
wakawa wanahitaji vyumba vya uangalizi maalumu lakini vyumba hivyo
vikawa vimetumiwa na wakubwa” alisema Waziri Ummy.
Waziri
ummy aliendelea kusema kuwa kutokana na ufinyu wa
nafasi JKCI wanauwezo wa kuafanya upasuaji kwa watoto 20 kwa mwezi, hivyo
kwa uwezo huu ambao umejengwa na Serikali kuu kwa kushirikiana na
wafadhili Charity Baptism wataweza kufanya upasuaji kwa watoto 40 kwa
mwezi kutoka watoto 20.
“Kutokana
na ufinyu wa nafasi JKCI ilikuwa na uwezo wa kufanya upasuaji kwa
watoto 20, lakini kwa uwezo huu ambao tumeweza kujengewa na Serikali
kuu kwa kushirikiana na wafadhili Charity Baptism wataweza kufanya
upasuaji kwa watoto 40 kwa mwezi kutoka watoto 20” alisema Waziri Ummy.
Aidha,
Waziri Ummy amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli kwa kuhidhinisha kiasi cha Shilingi 500 milioni kwa
ajili ya kukamilisha ujenzi huo ifikapo Januari 28.
Waziri
Ummy aliendelea kusema kuwa, kitengo hicho kinachotarajiwa kukamilika
mwishoni mwa mwezi huu, kimegharimu Sh2 bilioni ambazo fedha zingine
Sh800 milioni zimetolewa na wafadhili Charity Baptism.
Mbali
na hayo Waziri Ummy amewaagiza Waganga Wakuu wa Hospitali zote na Vituo
vya Afya kujiongeza kwa kufanya maendeleo yao wenyewe kwa wadau mbali
mbali wa masuala ya Afya badala yakusubili kila kitu kufanyiwa na
Serikali.
Kwa upande
mwingine Waziri Ummy amesema mwaka 2018 JKCI ilifanya oparesheni nyingi
zaidi kwa watoto hivyo anategemea mwaka huu zitaongezeka zaidi, “Hii
itakuwa wodi ya kwanza kwa ajili ya watoto pekee kwa Afrika Mashariki
walio wengi wanachanganya watoto na wakubwa.”
Mkurugenzi
Mtendaji JKCI Profesa Mohamed Janabi amesema kitengo hicho kipya
kilichoanzishwa pembeni mwa jengo hilo kitakuwa na vitanda 32 kutoka 11
vya awali.
“Watoto walikuwa na vitanda 11 pekee lakini kwa sasa tutakuwa navyo 32 na vitanda vya ICU vitakuwa 15,” amesema Profesa Janabi
MWISHO.
0 on: "SERIKALI YAIONGEZEA UWEZO JKCI"